Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

MAHAKAMA IMEISHIA HAPA KWA LEO TUKUTANE KESHO

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa muda umeisha, tunaomba Mahakama ihairishe kesi hadi kesho kwa ajili ya maswali ya dodoso.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasemaje?

Lissu: Sawa, Mheshimiwa Jaji.

Jaji Ndunguru: Shauri linapangwa kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuendelea kuulizwa maswali ya dodoso hapo kesho saa 3:00 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.

MUWE NA JIONI NJEMA
Ikiwezekana kaka uje uunganishe episodes zote katika uzi mmoja
 
Hadi hapa Nina imani na Golugwa, kumbe hofu yangu kwake ni bureee, tena huyu ndio ana mengi zaidi ya kuwaonesha umma.
Jamanii mmeona mambo wanayofanya mapolisi? Wakiongozwa na Mafwele? Yaan wanaopelekwa kwa Mafwele wanaitwa mizigo, mmesikia wenyewe hapo leo mahakamani, wanaotekwa huwa wanapelekwa km mizigo kwa mafwele.
Tobaaaaaaah!! Hadi nimeliaaa kwa kweli, machozi yanatoka yenyewee tu, 😢😢😭😭😭
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 14.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mazungumzo yangu.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sioni nia ambayo ingepelekea kuitishia Serikali.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama iwapo haya maneno niliyoyazungumza kama ilikuwa mara yako ya kwanza kuyasikia.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, haikuwa mara ya kwanza. Nilishawahi kuyasikia ukiyazungumza.

Lissu: Waeleze, uliyasikia wapi?

Amani Sam Golugwa: Niliyasikia katika mkutano tuliouandaa Sekretarieti na Wahariri wote Tanzania kupitia Jukwaa lao la Tanzania Editors Forum.

Lissu: Unakumbuka tarehe?

Amani Sam Golugwa: Mpaka nijikumbushe kidogo.

Katika mkutano ule uliokuwa unaongozwa na Mwenyekiti wa TEF, uliyasema.

Siku uliyokutana na Viongozi wa Dini ya Kiislamu (Shura ya Maimamu) mbele ya kiongozi wake, Issa Ponda.

Niliyasikia maneno hayo ukiyazungumza.

Nilisikia katika mkutano wa Legal and Human Rights Centre mbele ya kiongozi wao, Massawa.

Nilikuwapo na niliyasikia uliyasema.

Nilisikia maneno hayo mbele ya Mzee Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, tulikutana na Mzee Warioba wapi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, tulikutana na Mzee Warioba ofisini kwake.

Nilikuwapo na niliyasikia.

Lissu: Nilikuwa nasambaza maneno ya uhaini?

Amani Sam Golugwa: Haukuwa unasambaza uhaini, bali mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.

Ili mabadiliko yatokee kabla ya uchaguzi wowote kufanyika.

---

Lissu: Baada ya tarehe 09 Aprili mwaka jana, baada ya mimi kukamatwa, ni mambo gani yalitokea kwa chama na nyie viongozi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, chama kilifungiwa kesi na viongozi wa chama mbalimbali.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nini kilikutokea wewe mwenyewe?

Amani Sam Golugwa: Tarehe 13 Mei 2025 nilikuwa nasafiri kuelekea Ubelgiji.

Safari ambayo nilikuwa naenda kwenye mikutano kuwakilisha chama katika Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani.

Lissu: Kifupi chake kinaitwaje?

Nassoro Katuga anasimama.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaona ushahidi unatolewa kinyume na kifungu cha 156.

Sasa hivi tunaletewa safari na baadaye atatueleza habari ya ndoa.

Kifungu hiki kinalazimisha ushahidi must relate to the issue.

Relation yake na uhaini ni nini hapa?

Tunarudi katika irrelevant facts.

Watuambie, hicho kina relevance gani?

Tunaomba walete utetezi unaohusiana na kesi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, wakili wa Serikali anapenda kutoa mifano ya ovyo kabisa.

Mfano kwamba shahidi alioa na kuhusuiana na CHADEMA, nitautoa.

Ushahidi wa DW2 ni kampeni ya Jeshi la Polisi kunisakama mimi na kuwasakama viongozi wangu na chama changu.

Kesi hii, kwa mujibu wa ushahidi tulioutoa, ni utetezi dhidi ya sisi tunaonewa kwa mashitaka ya uongo.

Kwa hiyo, anachokisema shahidi juu ya kilichomtokea ni relevant.

Kifungu cha Sheria ya Ushahidi 7, 8 na 9, Relevance of facts.

(Anasoma kifungu cha 09.)

Waheshimiwa Majaji, hili swala la Polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA—

Leo Tundu Lissu, jana Mbowe na juzi Dr. Slaa.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naona hajajibu kifungu cha 156, ame-concede.

Lakini huo ushahidi wa kukamatwa ni fact kwa upande wa utetezi, siyo kesi.

Lissu: Kwani sisi tunatoa ushahidi wa nini? Si utetezi?

Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama tena.

MAJAJI WANATETA.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Mbona wao walimtaja Ishengoma na Tonetone? Lissu hakuwapinga kwamba tonetone na ishengoma haihusiani na ushahidi ktk commital proceedings , iweje sasa wakatae hiyo safari ya Sam Golugwa huko ubelgiji
 
Tayari Mshtakiwa wa kesi ya Uhaini Mh Tundu Lissu amefikishwa mahakamani.

Kaa tayari kufuatilia kile kinachoendelea mahakama kuu ya Tanzania, Mahakama ndogo jijini Dar es Salaam

=======

Soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Leo September 3, 2026, Jana tuliishia Sehemu ya 337


Sehemu ya 338.

Majaji wanaingia.

Mheshimiwa Lissu nae ameingia.

Ajuaye Zengeli anawatambulisha mawakili wa Serikali na Jaji anasema Shahidi apande kizimbani.

Shahidi Amani Sam Golugwa anapanda kizimbani.

Majaji wanateta na kusikilizana pale juu. Shahidi kiapo chako kinaendelea.

Golugwa: Sawa Ahsante anatikisa na kichwa kukubali.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako taarifa ya watazamaji wa SADC ilisemaje kuhusu huo uchaguzi?

Golugwa: Uchaguzi wa Tanzania haujakidhi vigezo vya chaguzi za kidemokrasia. Pia kulikuwa na vitisho na uonevu kwa viongozi wa vyama vya upinzani kwahiyo mazingira ya kiushindani hayakuwa sawa. Na tatu, hakukuwa na uwazi katika mchakato mzima wa Uchaguzi. Nne, kulikuwa na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi, vurugu siku ya uchaguzi na hivyo uchaguzi wa Tanzania umekosa uhalali wa kuitwa uchaguzi.Mhe. Lissu: Watazamaji wa Jumuiya ya Ulaya (EU) walisemaje kuhusu uchaguzi huo?

Golugwa: Walisema wamesikitishwa na matukio ya vurugu yaliyotokea, kuuwawa kwa watu walisikitishwa nako sana. Uchaguzi wa Tanzania uligubikwa na watu kutekwa kabla ya uchaguzi, kupotezwa na mazingira ya uchaguzi hayakuwa yenye ushindani ulio sawa. Na mazingira yalionekana kupendelea Chama cha Mapinduzi. Na mwisho kutokana na udanganyifu na vurugu zilizotokea uchaguzi wa Tanzania waliona haukuwa huru na haukuwa na uwazi.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji watizamaji wa jumuiya ya madola (Common wealth) walisemaje?

Golugwa: Niliona kauli ya Katibu wa Jumuiya ya Madola niliyoisoma alisema amesikitishwa na amehuzunishwa kwa vurugu na kauli zilizotokea na mauaji yaliyotokea na hivyo jumuiya ya madola itafuatilia kwa karibu kuhusu tukio hili.

Mhe. Lissu: Matokeo ya Uchaguzi wa mwaka jana yakikuwaje ya U Rais?

Golugwa: Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi alitangazwa amepata kura Milioni 31.6 na asilimia 98.6 na wagombea wengine kwa ujumla waligawana kipande kidogo kilichobaki yaani 2.4.

Mhe. Lissu: Ya ubunge yalikuwaje

Golugwa: Sifahamu

Mhe. Lissu: Udiwani yalikuwaje?

Golugwa: Sifahamu

Mhe.Lissu: Thabu Mbeki Fiundation walisemaje kuhusu matokeo ya Uchaguzi huo wa Tanzania?

Golugwa: Thabu Mbeki foundation walisema mambo manne. 1. Uchaguzi wa Tanzania uko chini ya viwango na miongozo ya chaguzi za Kidemokrasia kama zilivyowekwa kwa mujibu wa SADC na umoja wa Afrika. 2. Wapiga kura hawakupata uhuru wao wa kidemokrasia wa kupiga kura kwasababu ya vurugu zilizokuwa zimetokea. 3. Matokeo ya Urais na Ubunge yaliyotangazwa sio ya kweli na hayana uhalisi wa utashi wa watu kwenda kupiga kura. 4. Tanzania hakuna serikali yenye uhalali na hii iliyopo imejiweka kwa kutumia mabavu na udanganyifu kupitia uchaguzi usiokuwa halali.

Mhe. Lissu: Sasa shahidi katika watizamaji wote hao uliowataja. Waeleze majaji kwa ujumla wao walizungumziaje matukio ya mauaji ya wananchi kwenye uchaguzi huo?

Golugwa: Kwa ujumla wake waangalizi walisema vyombo vya dola kwa maana ya askari Polisi waliwapiga risasi waandamanaji na waliwazuia waangalizi kutimiza wajibu wao kwa kuwapiga na kuwanyang'anya vifaa vyao. Mhe. Lissu: Kuhusu mauaji ya wananchi ndio swali langu?

Golugwa: Walisema vyombo vya dola wamehusika katika mauaji ya waandamanaji na hivyo walitaka kuwepo na uwajibikaji kwa waliohusika na masuala hayo.

Mhe. Lissu: Huu uchaguzi ulisimamiwa na kuendeshwa na chombo kinachoitwaje?

Golugwa: Chombo kinachoitwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Viongozi wa hiyo tume wanapatikanaje?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji wanapatikana kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Mkurugenzi je wa hiyo tume anapatikanaje?

Golugwa: Anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.?



Sehemu ya 339

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Returning officers wanapatikanaje? Wale wanaosimamia kwenye majimbo.

Golugwa: Ni watumishi wa umma na wanapatikana kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Wasimamizi wa vituo ni akina nani?

Golugwa: Ni watumishi wa umma na ni watendaji kwenye ngazi ya Kata na Vijiji na mitaa. Na wote wanafanya kazi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanateuliwa na tume huru ya Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Hao watizamaji wote uliosema walisemaje kuhusu Kukamatwa kwangu na kufunguliwa kesi ya Uhaini?

Golugwa: Walisikitishwa kwa kukamatwa kwa kiongozi wa Chama kikuu cha siasa na wakasema kesi hii ni ya uongo na hawakuona mazingira ya uhaini kwa kile walichokisikia katika maneno ya Mh. Tundu Lissu na kuzitaka na kuzisihi mamlaka zimuachilie huru bkla masharti yoyote.Mhe. Lissu: Waeleze Majaji Baraza la Haki za Binadamu la UN limesemaje juu ya kesi hii?

Golugwa: Limesema kukamatwa kwa Lissu haikuwa halali na kitendo cha kukamatwa kwake kulimnyima uhuru wa kujieleza, na shtaka alilogunguliwa ni katili lenye lengo la kumuumiza na hivyo kutaka mamlaka zimwachilie sababu kesi hii ni ya kisiasa kabisa bila kupepesa macho. Commonwealth Ministerial Action Group walisemaje kuhusu kesi hii?

Golugwa: Kesi hii inadhihirisha uminywaji wa Demokrasia, kesi hii ni ya kisiasa, ni batili na Tundu Lissu aachiliwe bila masharti yoyote.

Mhe. Lissu: Turudi kwenye mkutano wa 3/4/2025 uliosababisha yote haya. Jana ulisema Mkutano huu uliandaliwa na Sekretarieti ya chama Makao Makuu kutokana na wazo la Katibu Mkuu kukutana na watia nia, sasa tuanzie hapo. Waeleze majaji, watu wengine waliohudhuria mkutano huuGolugwa: Watu wengine ni pamoja na viongozi wa chama ambao hawakuwa watia nia na waandishi wa habari ambao walikuwepo ndani ya ukumbi wa mkutano.

Mhe. Lissu: Ukisema viongozi wa chama ambao hawakuwa watia nia unamaana gani? Golugwa: viongozi wa chama kwenye ngazi ya Kanda, Mkoa na Jimbo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama viongozi wa chama ni hao tu uliowatajaGolugwa: Walikuwepo pia viongozi wakuu wa chama nikiwemo mimi mwenyewe na viongozi wa Sekretarieti.

Mhe. Lissu: ukisema Viongozi wakuu una maana gani:

Golugwa: Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Zanzibar wote walikuwepo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji, watu wote hao waliokuwepo walipataje taarifa za uwepo wa mkutano huu?

Katuga anasimama, shahidi wa facts ni Golugwa anapaswa aongee yeye hilo swali sio sahihi

Mhezz Lissu: Pingamizi la Katuga halina mashiko kwasababu Mkutano wowote lazima uwe na taarifa

Katuga: wengine huwa wanaota kuwa kuna mkutano

Mhe. Lissu: Nyie mawakili wa Serikali ndo huwa mnaota kwa visomo vyenu vya gizani sio mimi Lissu

Majaji: Twendelee

Mhe. Lissu Golugwa anaendelea: mimi ndio niliwapigia simu viongozi wakuu wafuatao: Mkt Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na niliwaambiwa wanatakiwa kuwepo. Wengine waliokuwepo ukumbini walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama Brenda Rupia ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, maandalizi na hii mialiko wakati inafanyika mimi nilikuwa wapi?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji wakati haya yanafanyika Lissu alikuwa kwenye operation ya Chama ya No Reforms No Election kanda ya Nyasa Shahidi Golugwa anaheshima sana kwa majaji kila akianza kujibu swali anasema WAHESHIMIWA MAJAJI

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama mimi Lissu nilishiriki kuandaa mkutano na kutuma mialiko kwa washiriki

Golugwa: Tundu Lissu hakushiriki kuanzia kwenye maandalizi na hakuwasiliana na hata kutuma mialiko kwa watia nia.



Sehemu ya 340

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: waeleze majaji ushiriki wangu katika kualika waandishi wa habari

Golugwa: Tundu Lissu hakualika waandishi wa habari kabisa hivyo Jamhuri wakidai kuwa ulialika ni uongo kabisa

Mhe. Lissu: Mashtaka yanadai kuwa mimi niliitisha mkutano huu, wewe unasemaje?

Golugwa: Madai hayo ni ya uongo kabisa, hayana nia njema na Lissu, ni upotoshaji kabisa kwasababu Lissu hakushiriki

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa waandishi wa habari Golugwa: waandishi kibao walikuwepo wa online TV, Magazeti, Radio

Mhe. Lissu: Waeleze majaji vyombo vya habari vilivyokuwepo

Golugwa: Nakumbuka uwepo wa Clouds TV, Jambo Online TV, the Chanzo Online TV, ITV, waandishi wa gazeti la Mwananchi na wengine kibao tu.

Mhe. Lissu: waeleze majaji hao waandishi walialikwa na nani kwenye mkutano?

Golugwa: walialikwa na Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa masharti yoyote kwenye mwaliko wa waandishi wa habari

Golugwa: hakukuwa na masharti yoyote na hata kwenye mkutano ukumbini haukuwa na masharti yoyote kabisa walifanya kazi yao kwa uhuru wao wa vyombo vya habari

Mhe.Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maelekezo yoyote kutoka kwangu au kiongozi yoyote wa chama aliyekuwepo juu ya namna ya kufanya kazi yao

Golugwa: Mimi ndio msimamizi wa itifaki na ndio niliendesha mkutano huo hivyo Lissu wala kiongozi yoyote wa chama hakutoa maelekezo yoyote juu ya namna ya waandishi wa habari kufanya kazi yao.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa matangazo ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja kwenye mkutano huo

Golugwa: Kwakuwa waandishi walikuwepo wa Online TV na wa Magazeti, wapo waliorusha live kama online TV

Mhe. Lissu: Watajie majaji vyombo vilivyorusha live mkutano huo

Golugwa: Jambo TV, the Chanzo TV na wengine kibao

Mhe. Lissu: Mimi nimeshtakiwa kuwa nilichapisha hayo maneno kwenye Jambo TV, wewe unasemaje?

Golugwa: Huo ni uongo wa mchana kweupe kabisa, inawezekanaje Lissu achapishwe kwenye Jambo TV wakati sio Mwandishi na hafanyi kazi Jambo TV?

Jaji Nduguru: Shahidi umechomekea na swali la kuwa inawezekanaje kwenye jibu lako Watu kicheko😂😂😂😂

Mhe. Lissu: Machapisho yanayorushwa kwenye chombo cha habari ni mali ya nani?

Golugwa: kwa uelewa wa kawaida kabisa hiyo inakuwa ni mali ya mwenyechombo.

Mhe. Lissu: nani anakuwa na haki ya kufanya chochote kwenye contents za habari kwa mfano hiyo hotuba ya mkutano waliyochukua waandishi?

Golugwa: mwenye haki ya kufanya chochote ni mmiliki wa chombo cha habari.

Mhe. Lissu: nimekaa gerezani zaidi ya mwaka na miezi 5 sasa kwa mashtaka kuwa nilitengeneza nia ya kutenda uhaini dhidi ya serikali na hiyo nia niliidhihirisha kwa kuchapisha maneno kwenye Jambo TV, (Lissu anarejea maneno ya kwenye mashtaka ya kukinukisha), waeleze majaji uhusika wangu kwenye kuchapisha maneno haya kwenye mtandao wa Jambo TV

Golugwa: hakuna uhusika wowote wa Tundu Lissu wa yeye kuchapisha kwenye Jambo TV hivyo mashtaka ni ya uongo kabisa

Mhe. Lissu: kwa ufaham wako maneno hayo yalichapishwa na nani Jambo TV ?

Golugwa: Yalichapishwa na mwandishi wa Jambo TV ambaye alikuwa amealikwa kwahiyo Lissu hahusiki kabisa na uchapishaji

Mhe. Lissu: tuhuma za kuwa mimi ndio nilichapisha haya maneno Jambo TV wewe unaisemeaje?

Golugwa: Ni uongo kabisa, nia yake ni kumtesa tu Tundu Lissu, kudhorotesha kabisa shughuli za chama chetu , hii tuhuma ni ya uongo tena uongo mbichi kabisa.

Watu wamecheka sana jibu la shahidi eti uongo mbichi😂😂😂😂



Sehemu ya 341

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: kuna ushahidi umeletwa mahakamani eti nilichapisha hayo maneno Jambo TV nikiwa na nia ya kuitishia serikali ya JMT, je kwenye maneno ya hati ya mashtaka, kuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Golugwa: Mimi nilikuwepo siku unatoa hotuba, hukutaja kabisa neno Serikali na kwenye hayo maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano

Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa neno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Golugwa: hilo neno halipo kabisa Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT

Golugwa: Waheshimiwa majaji hilo neno halipoMhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT

Golugwa: Hilo neno nalo halipo

Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa neno Baraza la Mawaziri
Golugwa: Hilo neno halipo

Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT au Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

Golugwa: hayo maneno hayapo

Mhe. Lissu: sasa shahidi kuna ushahidi umeletwa hapa eti nilitishia vyombo vya dola, sasa waeleze majaji uwepo wa maneno Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Mgambo, Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, Jeshi la Magereza au jeshi lolote la nchi hiiGolugwa: Maneno yote hayo hayapo kabisa waheshimiwa majaji.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa neno Serikali katika hati ya mashtaka ambayo nimekusomea

Golugwa: Neno Serikali haipo

Mhe. Lissu: Hii tuhuma wewe unaionaje?

Golugwa: ni tuhuma ya uongo, ya kutunga sio ya kweli, imetengenezwa kwa nia ya kisiasa ili kurudisha nyuma jitihada za Tundu Lissu kwenye kudai mabadiliko kwenye mifumo ya kiuchaguzii

Mhe. Lissu: Mtu akisema akisema msimamo huu unaashiria uasi anakuwa ametenda kosa gani?

Golugwa: kwa ufahamu wangu hakuna kosa lolote anakuwa ametenda katika nchi hii Bara na Visiwani.

Mhe. Lissu: Kwa ufahamu wako, mtu akisema tutauvuruga uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani nchi hii? Golugwa: kwa ufaham wangu hakuna kosa lolote atakuwa ametenda katika nchi hii

Mhe. Lissu: mtu akisema tutauzuia uchaguzi huu anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?

Golugwa: Mtu akisema tutauzuia uchaguzi anakuwa hajatenda kosa lolote katika nchi hii

Mhe. Lissu: waeleze majaji, kwa ufahamu wako wa masuala ya uchaguzi uwepo wa sheria inayosema kuwa ni kosa mtu kusema atazuia au kuvuruga uchaguzi

Golugwa: kwa ufahamu wangu hakuna sheria inayosema kuwa ni kosa kuzuia au kuvuruga uchaguzi

Mhe. Lissu: kuna ushahidi uliletwa hapa wa kamusi kutafisiri neno uasi kuwa ni kitendo cha kuvunja sheria, waeleze majaji, kitendo cha kuvunja sheria kama ni kosa la uhaini

Golugwa: kwa ufahamu wangu kitendo cha kuvunja sheria sio kosa la uhaini

Mhe. Lissu: Tumeletewa kamusi inatafsiri uasi kuwa ni kupinga mamlaka, taasisi, serikali au Taasisi je waelezo majaji kupinga serikali au taasisi kama ni kitendo cha uhainiKitendo cha kupinga serikali au taasisi ni kosa kisheria?

Golugwa: kwa ufahamu wangu kupinga serikali au taasisi sio kosa kisheria

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako maana ya neno kukinukisha

Golugwa: waheshimiwa majaji kwa tafisiri ya kawaida tu kukinukisha ni kukifanya kitu kitoe harufu, harufu ya marashi yaani unyunyu, kusababisha harufu itokeWatu wanacheka sana hapo kwenye unyunyu😂😂😂😂😂

Mhe. Lissu: mtu akisema tunaenda kufanya kitu kitoe unyunyu, yanatishiaje serikali ya JMT?

Golugwa: maneno hayo hayawezi kuitishia kabisa maneno ya kutoa harufu nzuuuri au uvundo, kwakweli sioni kabisa mahali serikali inapoweza kutishika

Mhe. Lissu: Serikali ya JMT inatishikaje na maneno tutauzuia uchaguzi, tutauvuruga uchaguzi? ambayo kwa ushahidi wako sio makosa kwa mujibu wa sheria

Golugwa: Sioni kwa namna gani Serikali inaweza kutishika kabisa



Sehemu ya 342

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako, Serikali ya JMT na vyombo vyake vyote inatishikaje na maneno msimamo huu unaashiria uasi ambayo kwa ushahidi wako umesema sio kosa

Golugwa: waheshimiwa majaji sioni namna yoyote serikali kutishika kwa maneno kuwa msimamo huu unaashiria uasi

Mhe. Lissu: Waeleze majaji Serikali ya JMT na manguvu yake yote inatishikaje na maneno tutahamasisha uasi

Golugwa: Sioni ni kwa namna gani serikali na manguvu yake yote inatishikaje na maneno tutahamasisha uasi.

Mhe. Lissu: kuna maneno yalizungumzwa hapa kuwa Oktoba 29 kuna vurugu zilifanyika, mali zilichomwa, vituo vya mwendokasi, kuchoma vituo vya kupigia kura, sasa nakuuliza maswali:

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tunaensa kuchoma vituo vya kupigia kura kwenye hati ya mashtaka

Golugwa: Maneno kuchoma vituo vya kupigia kura hayapo kwenye hati ya mashtaka

Mhe. Lissu: kwenye hati ya mashtaka kuna maneno tunaenda kuchoma vituo vya mwendokasi?

Golugwa: hakuna maneno tunaenda kuchoma vituo vya kupigia kura

Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno kuwa tunaenda kupiga au kukata vidole watu wanaoenda kupiga kura

Golugwa: hakuna maneno tunaenda kupiga au kukata vidole wale wanaoenda kupiga kura.

Mhe. Lissu: waeleze majaji, uwepo wa maneno kuwa tunaensa kuharibu mali, magari, na vitu mbalimbali vya watu binafsi

Golugwa; maneno hayo hakuna kwenye hati ya mashtaka

Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno kuwa tunaenda kuua, au kusababisha watu kufa siku ya uchaguzi kwenye hati ya mashtaka

Golugwa: maneno kuwa tunaenda kuua au kusababisha watu kufa siku ya uchaguzi hayapo kwenye hati ya mashtaka

Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umewahi kusikia hotuba ya jaji chande

Golugwa: ndio niliwahi kumsikiliza akitoa hotuba ya Tume ya Vurugu za Oktoba 29, 2025

Mhe. Lissu: waeleze majaji endapo ulimsikia Jaji Mstaafu Chande kuhusu idadi ya watu kuuwawa

Golugwa: nilismikiliza alisema idadi ya watu waliouwawa ni 518

Mhe. Lissu: waeleze Majaji, kwa ufahamu wako kama ulimsikia Jaji Chande akisema waliosababisha hivyo vifo

Golugwa: sikumbuki kama jaji Chande aliwataja waliosababisha vifo

Mhe. Lissu: waeleze majaji sababu alizotoa Jaji Chande zilizosabisha vurugu za Oktoba 29, 2025

Golugwa: alisema ni madai ya Katiba Mpya, manung’uniko ya muda mrefu ambayo wamedai na hayajatatuliwa

Mhe. Lissu: Kwa wewe na wajumbe wa sekretarieti ya chama kuandaa mkutano wa 3/4/2025 waeleze majaji endapo kuna hatua zozote mlichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa kuandaa na kuwezesha mkutano huo

Golugwa: hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yangu au wenzangu katika Sekretariaeti na Jeshi la Polisi kwa sisi kuandaa mkutano huo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji iwapo ulisikia maneno yaliyopp kwenye hati ya mashtaka kama niliyatamka kwenye mkutano wa 3/4/2025

Golugwa: Niliyasikia hayo maneno ukitamka kwenye mkutano

Mhe. Lissu: Waeleze hatua ulizochukua kwenda kuripoti maneno hayo katika jeshi la polisi

Golugwa: Sikuripoti popote

Mhe. Lissu: waeleze majaji mtu mwingine yeyote aliyekuwepo kwenye mkutano aliyechukua hatua kwenda kuripoti katika Jeshi la Polisi maneno hayo

Golugwa: hakuna mtu aliyeenda kuripoti

Mhe. Lissu: waeleze majaji ufahamu wako juu ya uwepo wa kosa linaitwa kunyamazia uhaini

Golugwa: sifahamu uwepo wa kosa hilo

Mhe. Lissu: waeleze majaji iwapo wewe au watu wengine wote waliokuwepo kwenye mkutano waliosikia maneno hayo kama wamefunguliwa shtaka la kunyamazia uhaini

Golugwa: hakuna mtu aliyefunguliwa kosa la kunyamazia uhaini



Sehemu ya 343

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: shahidi ulisema Jambo TV na Chanzo TV walirusha mkutano huo live, waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa hatua zozote za kuwafungulia Jambo TV na Chanzo TV mashtaka ya kuwezesha uhaini

Golugwa: kwa ufaham wangu sijasikia wala sijaona hatua zozote dhidi ya waandishi wa habari wa Jambo TV na Chanzo TV wakichukuliwa hatua kwa kosa la kuwezesha uhaini au kusambaza maudhui ya mkutano huo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama inawezekana mtu mmoja kufanya kosa la uhaini la kuitishia Serikali yote ya JMT

Golugwa: kwa ufahamu wangu sioni uwezekano wa mtu mmoja peke yake kuitishia serikali, kupanga uhaini, kutekeleza uhaini, kwa ufahamu wangu haiwezekani

Mhe. Lissu: Waeleze majaji iwapo maneno matupu ya mdomo yanaweza kutengeneza kosa la uhaini

Golugwa: kwa ufahamu wangu maneno matupu hayawezi kutengeneza kosa la uhaini.

Mhe. Lissu: Mkutano wa 3/4/2025 ulichukua masaa mangapi?

Golugwa: kama Masaa matatu hivi

Mhe. Lissu: waeleze majaji iwapo Jambo TV na Chanzo TV walirusha masaa yote matatu

Golugwa: Hawakurusha masaa yote matatu kwasababu baadae tuliendelea na kikao

Mhe. Lissu: waeleze majaji Jambo TV na Chanzo TV walirusha kwa muda gani unaoukumbuka

Golugwa: Nakumbuka lisaa moja na nusu hadi masaa mawili

Mhe. Lissu: ngoja nikusomee maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, waeleze majaii muda niliotumia kusoma hayo maneno

Golugwa: umetumia sekunde tu kama 26 hivi haifiki hata dakika moja

Mhe. Lissu: waeleze majaji kwa ujumla wake hoja nilizozungumza

Golugwa: Tundu Lissu alizungumza kuhusu ubovu wa mfumo wa uchaguzi, alielezea matatizo ya uchaguzi yaliyopo katika Katiba yanayoathiri chaguzi zetu, kwenye Sheria, Kanuni na Miongozo, alieleza kuhusiana na Tume mbalimbali kama ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Warioba jinsi ambavyo zilieleza mapungufu yaliyopo katika mifumo yetu ya uchaguzi na mapendekezo ya Tume zote hizi kuhusiana na nini kifanyike ili kurekebisha mfumo wa uchaguzi. Mhe. Lissu alizungumza pia kuhusu taarifa mbalimbali za waangalizi wa uchaguzi kuanzia mwaka 1995 wote wa ndani wa kimataifa, REDET, TEMCO na alifafanua na kuelezea maoni ya waangalizi wa ndani kuhusiana na haja ya kuwa na mabadiliko ili kuwa na chaguzi huru na zinazoaminika.

Mhe. Lissu alifafanua taarifa kwa maana ya ripoti za waangalizi wa nje kwa chaguzi zote kuanzia 1995 akiwataja, SADC, Marekani, Jumuiya ya Ulaya, Umoja wa Afrika madudu yote waliyoyaona na mapendekezo yao juu ya haja ya kuwa na mabadiliko ya kweli kwenye mifumo ya uchaguzi Mhe. Lissu pia alizungumzia kuhusu uzoefu wa chama chetu kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa 2020, uzoefu wa chaguzi ndogo za Udiwani na Ubunge zilizotokea kati ya mwaka 2015 hadi 2019 na kuendelea. Mhe. Lissu pia alizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 kuhusu uzoefu wa matukio ya hovyo na kinyama ambayo wagombea wetu wa Chadema tuliyapitia.

Hayo matukio ya hovyo yalikuwa yanafanywa na wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao ambayo ni pamoja na kuwaengua wagombea wa chadema kihuni kabisa, wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wanakataa kuchukua fomu za wagombea, matukio ya mauaji

Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kusema muda sasa ni wa break tunaomba ahirisho hadi 14:30

Mhe. Lissu: Ni sawa waheshimiwa majaji shahidi nae akapate maji kidogo

Jaji Nduguru: Shauri linaahirishwa hadi saa nane na nusu

Inapigwa High Cooouuurt

Majaji wanatoka.



Sehemu ya 344

Mahakama Imerejea Inapigwa High Coooouuurt

Majaji wanaingia Mahakamani

Wakili wa Serikali Ajuaye anasimama anasema mawakili wa Serikali tuko vilevile

Jaji Nduguru anamuuliza Mhe. Lissu uko tayari?

Mhe. Lissu: Niko niko tayari

Jaji Nduguru twendelee

Mhe. Lissu: Wakati tumenda Break ulikuwa unaelezea kuhusu hotuba ya 3/4/2025 naomba uendelee

Golugwa: Mwenyekiti Tundu Lissu alielezea pia matukio ya mauaji katika chaguzi za nchi yetu mfano wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Mgombea wa Chadema aliuwawa kwa kupigwa risasi , mwingine wakati wa marudio ya uchaguzi mdogo kinondoni,

Mhe. Lissu: Baada ya kuelezea mauaji katika chaguzi zetu nilisema nini?

Golugwa: Ulisema kuliko kupitia mabalaa haya yote, ya watu kuuwawa kwenye chaguzi, vurugu na fujo tupo tayari uchaguzi uahirishwe na usogezwe mbele ili kama taifa tuweze kushughulikia matatizo haya yaliyopo kwenye mifumo yetu ya uchaguzi. Tundu Lissu pia alisema tunamaanisha, tupo tayari na sheria zetu zinaruhusu uchaguzi kusogezwa mbele.

Mhe. Lissu: Jambo lingine nililolizungumzia naomba endelea kuelezea

Golugwa: Jambo lingine Mhe. Lissu alisema ambaye anawaza kugombea uchaguzi huu asahau, aende akafanye kazi ya kuwaelimisha wapiga kura wake juu ya msimamo wetu wa No Reforms No Election ili watanzania wote watuunge mkono. Jambo lingine Mhe. Lissu alisema hata yeye alikuwa anafikiria kugombea Urais ila hatagombea na kuwa upo tayari uchaguzi usogezwe mbele na utakwenda kuwaelimisha watanzania nchi nzima

Mhe. Lissu: Kwa mazungumzo yangu yote ya siku hiyo ambayo umeyasema hapa, mtu akikuletea maneno machache ambayo yapo kwenye hati ya mashtaka wewe unasemaje?

Golugwa: Mimi naona kabisa ni ya kutengeneza na yana nia ovu dhid yako, nia ya kukuonea wewe na chama chetu ili tusifanye siasa tunazoruhusiwa kisheria.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako maneno ya hotuba yangu yote kama kulikuwa na uwepo wa nia ya kutenda uhaini

Golugwa: Kwa ufaham wangu hakuna nia kabisa ya uhaini au kuitishia serikali

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa kumbukumbu zako hayo maneno niliyozungumza 3/4/2025 kama ilikuwa ni mara yako ya kwanza kuyasikia

Golugwa: Kwa kweli umeshayasema mara nyingi sana ikiwemo Mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ulioongozwa na Deodatus Balile y wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ulisema pia ulipokutana na viongozi wa dini ya kiislamu Shura ya Maimamu mbele ya kiongozi Shikhe Ponda Issa Ponda, na mimi nilikuwepo na nilisikia maneno hayo ukiyasema. Golugwa anaendelea kusema kuwa Mhe. Lissu pia ulisema maneno hayo tulipokutana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadmau mbele ya wakili Fulgence Massawe, nilikuwepo na uliyasema.

Vilevile uliyasema mbele ya Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ofisini kwake Masaki na uliyasema maneno hayo nilikuwepo na niliyasikia na Mzee Warioba alituunga mkono kabisa

Mhe.Lissu: Waeleze majaji hizo ziara zote na kusema maneno yote hayo, je nilikuwa nasambaza nia ya kutenda uhaini?

Golugwa: haikuwa kusambaza uhaini ila ilikuwa ni kuwaelimisha msimamo wetu ili watuunge mkono ili mabadiliko yatokee kabla ya uchaguzi kufanyika , wote walituelewa isipokuwa Serikali

Mhe.Lissu: Baada ya tarehe 09/4/2025 mimi kukamatwa, waeleze majaji mambo gani yalitokea kwa chama na nyie viongozi mliobakia

Golugwa: Chama kilifunguliwa kesi na kuzuiwa kufanya kazi za chama, viongozi tulikamatwa na kutuhumiwa kwa makosa ya kubambikiza kama ugaidi n.k

Mhe. Lissu: wewe kilikutokea nini binafsi?

Golugwa: Tarehe 13/05/2025 nilikuwa na safari ya kwenda Ubeligiji kukiwakilisha chama kwenye mkutano wa vyama vya kidemokrasia duniani (IDU)

Katuga anasimama: Mhe Jaji shahidi anachosema ni kinyume cha kifungu cha 156 cha Sheria ya Ushahidi kwasababu hauhusiani na kesi, shahidi atakuja pengine kutoa mifano kama alioa au hakuoa


Sehemu ya 345

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Shahidi endelea kuhusu kilichokutokea 13/05/2025

Golugwa: Tarehe 13/05/2025 nilipokuwa Airport wakati tayari nimeshapewa boarding pass, nikiwa kwa afisa uhamiaji nilifuatwa na watu wawili wakasema twende ofsiini tuzungumze, wakati tunaelekea ofsini kwenye kibaraza walisema niko chini ya ulinzi, mmoja hakuwa na kitambulisho na alikuwa amevaa nguo za kiraia ndio alisema niko chini ya ulinzi, waliniingiza kwenye chumba na kuniacha. Kabla ya hapo walitaka simu zangu na huyu ambaye hakuwa na unifomu wala kitambulisho alizichukua zote.

Waheshimiwa majaji baada ya dakika kama 5 nikiwa kwenye chumba walikuja watu zaidi ya watano mmoja akiwa na bunduki, walifungua mlango wakapekua begi langu na wakachukua karasi mbili ambazo zilikuwa na hotuba ambayo nilipanga kwenda kuzungumza kule kwenye mkutano. Waheshimiwa majaji pamoja na kwamba niliwauliza kwanini wamenikamata, kwanini wananipekua, kosa langu nini?

Hawakunijibu kabisa, walinishusha underground pale airport , mwendo ulikuwa wa kasi sana, walinitukana sana “naomba nisiyaseme maneno haya mbele ya mahakama tukufu” mmoja aoiyekuwa na bunduki aliniwekea kwenye sikio la kulia na akasema “nyie wajinga ndio mnapanga safari zenu kwenda kuichafua nchi huko nje, sasa leo ndio utaelewa”.

Sikupigwa ila nililazimishwa kutembea , naomba majaji mniangalie niwaonyeshe Amani Golugwa anawaonyesha Majaji jinsi alivyoning’inizwa kwa kushikwa maeneo ya maungoni miguu ikawa haifiki chini ameonyesha kwa umaridadi kabisaWaheshimiwa majaji baada ya hapo niliingizwa kwenye gari nikazungushwa kwa zaidi ya masaa mawili Airport na baadae nikapelekwa Stakishari Police station, niliwahoji kwanini mnanileta huku?

Wakasema wewe ndio Lissu huwa anakutuma kwenda kuisema serikali huko nje na kupewa hela chafu kutoka nje hivyo wewe cybercrimes inakuhusu na money laundering.

Golugwa anaendelea kusema ilipofika saa nane usiku watu 10 walikuja kunichukua na walikuwa wote wapya nikawauliza mnanipeleka wapi wakawa hawajui na wakawa wananishangaa, walikuwa na radio call wakawa wanaongea wanasema tuko na mwewe, tulielekea kushoto kutoka Stakishari mimi nikiwa nimelala chini kwenye gari, baada ya muda tulifika Central Police Station Dar es Salaam na yule aliyekuwa anaongea na radio call akamwambia ZCO Mafwele kuwa mzigo huo.

Waheshimiwa majaji sikuwa sawa wakati huo kutokana na magumu niliyopitia na ZCO aliniongelesha kwa lugha nzuri ingawa mimi nilikuwa katika hali ngumu sana maana nilikuwa sielewi hatima yangu na nilipofikishwa tu wakasema cybercrimes na money laundering.

Waheshimiwa majaji niliulizwa kuhusu safari zangu mbili za huko nyuma za Mombasa na waliniambia kuwa nimekuwa nasafiri na kurudi bila kufuata taratibu na sheria za nchi, walinitaka nitoe maelezo, nilihoji sana na sikuwa tayari kutoa maelezo lakini mwishoni nilitoa maelezo na nikatakiwa nilete uthibitisho wa safari ya Mombasa ambayo nilisafiri na familia na wazazi wangu na nilipeleka uthibitisho kwa kupeleka nakala za passpoti.

Mhe. Lissu: mambo yote haya yaliishia wapi?

Golugwa: nilidhaminiwa na viongozi wa chama na nikaambiwa nenda nyumbani kwa amani. Hivyo safari ya kikazi ilivurugika na sikufanikiwa kusafiri.

Mhe. Lissu: waeleze kuhusu ukweli wa tuhuma hizo kama ni kweli au sio kweli

Golugwa; tuhuma hizo sio za kweli

Mhe. Lissu: waeleze majaji kama kuna sheria inazuia wewe kusafiri kwenda nje ya Nchi

Golugwa: Hakuna sheria



Sehemu ya 346

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali Katuga anapenda kutoa mifano ya hovyo kabisa yani, kama shahidi alioa na akaingiliwa na Polisi ni ushahidi unaohusiana na kesi. Ushahidi wangu na ushahidi wa Mnyika unahusu kampeni ya uonevu wa Serikali dhidi yetu na Chama chetu.

Kesi hii ni ya uonevu, ni ya uongo ni ya kisiasa na Serikali wamekuwa wanakamata watu na Viongozi wetu bila kufuata sheria, bila kuwafungulia mashtaka kwa nia ya kudhoofisha Chama chetu. Kifungu sahihi ni cha 7 , 8 , 9 cha Sheria ya Ushahidi.

Hawa mawakili wa Serikali hawataki Jeshi la Polisi la Serikali wanayoitumikia liwe exposed, uchafu wao wanaoufanya kunyanyasa watu hawataki uwe exposed, sisi hatutakubali maana tumenyanyaswa sana mimi binafsi, Mbowe, Mnyika, Dr. Slaa na viongozi wengine.

Katuga: Anachokisema Lissu ndio maana ya kukinukisha sasa ; sisi tunaomba maelekezo ya Mahakama ila kama ushahidi huo ni wa muhimu kwa upande wa utetezi hatuna shida kwasababu tutapata nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso.

Jaji Ndunguru anashauriana na majaji wenzake ameanza na Jaji Kareyamaha leo, kaenda kwa Jaji Kiwonde ngoja tuona, ila wamechukua dakika nyingi sana ni zaidi ya 10. Jaji Nduguru baada ya majadiliano ya muda mrefu anasema tumesikia hizo hoja, tunaelekeza tuwe focused, wajibu wa prosecution ni kuthibitisha kesi, Mshtakiwa hana wajibu wa kuthibitisha utakatifu wake, shida ni kwamba upande wa utetezi huwa hawana statement kwamba labda ina guide upande wa utetezi. Jamhuri mna haki ya kufanya cross examination na hiyo ndio fair trial.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji tukio jingine la kukamatwa kwako.

Golugwa: Tarehe 08/11/2025 nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu Arusha nilikamatwa na Polisi na nilipohoji kwanini wananikamata wakanitajia makosa matatu: ugaidi, kula njama ya kuharibu miundombinu ya umma na mali ya umma, kula njama ya kuwapiga askari wa vyombo vya dola, eti mimi huyu nipange kupiga askari? Shahidi anaongea kwa hisia na kujiuliza swali

Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya hapo?

Golugwa: Nilikaa Central Police Arusha kama masaa mawili na baadae nilisafirishwa hadi Oysterbay Police Dar es Salaam majira ya saa moja usiku, nilikataa kutoa maelezo hivyo niliwekwa lock up. Ilipofika saa nane usiku tena nilitolewa nikaambiwa kutoa maelezo, sikutoa maelezo na niliwaambia aje ZCO Mafwele ambaye nimefahamiana nae akiwa Arusha aje aseme kwa anavyonifaham kama mimi huyu Golugwa ninaweza kuwa gaidi.

Waheshimiwa Majaji kesho yake ZCO Mafwele alikuja akanishawishi nitoe maelezo na wakili Hekima alikuja nae akanishawishi nitoe maelezo, sikutoa maelezo na niliowaona na wenzangu hapo Lema, Boni Yai na John Heche. Tuliambiwa nendeni na kesho yake tulitakiwa kwenda kwa ZCO Mafwele Central Police station na baada ya kuripoti tuliambiwa nendeni na ikawa hivyo hadi leo

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hatua gani Jeshi la Polisi limeshachukua hadi leo

Golugwa: hakuna hatua yoyote mpaka leo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji hii kamatakamata inamaanisha nini kwako

Golugwa: nia yake ilikuwa kunitisha mimi na viongozi wenzangu ili tusifanye kazi yetu ya chama.

Mhe. Lissu: Waeleze ufahamu wako kuhusu matukio ya mimi kukamatwa ukichilia tukio hili lililoniweka gerezani

Golugwa: Mwaka 2012 nakumbuka tulikamatwa wote na kumwagiwa maji ya washawasha na kipigo Arusha, nakumbuka mwaka 2024 tulikamatwa Mbeya ulipoenda kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana, tukio jingine lilitokea Arusha ulipokuja kumtetea Lema nakumbuka ulikamatwa, ulipotoa maoni yako kuhusu utawala wa Magufuli pia ulikamatwa uliposema Magufuli ni Dikteta Uchwara.


Sehemu ya 347

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Katika Matukio yote ya mimi kukamatwa uliyoyasema, waeleze majaji kumbukumbu zako za mimi kutiwa hatiani kwa kosa lolote nililowahi kukamatwa nalo

Golugwa: sina kumbukumbu yoyote ya wewe kutiwa hatiani kwa matukio yote uliyokamatwa wala kushtakiwa nayo

Mhe, Lissu: Umenifahamu kwa muda gani?

Golugwa: Nimekufahamu kwa miaka 20

Mhe. Lissu: leo nashtakiwa kwa uhaini, kosa kubwa kuliko yote nchi hii, waeleze majaji kwa ufahamu wako uwezekano wa mimi kuwa mhanini kwenye nchi yangu

Golugwa: Waheshimiwa majaji kwa namna ambavyo namfahamu Lissu kwa hiyo miaka 20, ni mtu mwema sana na sioni uwezekano wa Tundu Lissu kuwa mhainiHapa shahidi ametiririka sana mpaka Majaji wamefurahi.

Jaji Nduguru amesema CV yake Lissu ameshaitoa hapa Mahakamani. Watu wamefurahi sana hizi dakika za jiooooni kabisa.

Mhe. Lissu: Kwa shahidi huyu nimemaliza maswali

Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama anasema hivi sasa ni saa kumi na moja kamili na kwa vile muda umeisha tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi kwaajili ya maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.

Jaji Nduguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.

Inapigwa High CoouuuuuurtMajaji wanatoka nje.

Mhe. Lissu anapack makablasha yake huku akiagana na Viongozi, Wanachama na Wafuasi wa CHADEMA waliokuja Mahakamani siku ya Leo.
MaCCM ni majitu ya kiquma na kichoko sana. Hayajui kuwa nguvu ya umma hainyamazishwi kwa kutumia hizi kangaroo courts za gacaca (CCM). Utawala huu umejaa mitutusa kuanzia chini hadi juu.
 
Jamani nina wasi wasi na Golugwa, ni yuko vizuri ktk kutoa majibu, ila uwasilishaji wakw unanipa hofu, afu anakua km hajiaminii.
Basi mtazamo wangu unaona hivyo.
Sikiliza Dada yangu hata kama shahidi ana kigugumizi,hajui kabisa kuongea kiswahili vizuri n elimu yake ni ya darasa la pili,ikiwa TU anatoa ushahidi upande wa haki hakuna kitu kitaharibika.
Ikiwa anashuhudia ukweli ushahidi wake utakua na nguvu TU.
Usiombe kushuhudia uongo hata kama ni profesa utaaibika TU.
 
Nilikua namchukulia Poa Golugwa kumbe yeyw ndio anapiga penyewe kabisa panapouma, hadi Katuga kaanza kupoteana na kupanick mapema kabisaa hata dodoso hajafanyaa.
😂😂😂😂
nami nilikuwa na wasi wasi naye sanaaaaaaaaaaaaa, kumbe he can do it!
 
MaCCM ni majitu ya kiquma na kichoko sana. Hayajui kuwa nguvu ya umma hainyamazishwi kwa kutumia hizi kangaroo courts za gacaca (CCM). Utawala huu umejaa mitutusa kuanzia chini hadi juu.


Kukinukisha kakinukisha Mwenyekiti wa CHADEMA

Wakafa Watu wa Jamhuri mwenye watu watu wake Jamhuri imechukua hatua kumshikisha adabu Uyo chanzo cha tatizo

Sasa badala mshikamano na Jamhuri ❗️

nyinyi mpo upande wa yule chizi kichwani Bob w Singida
ndani ndani

Akitoka kama ajanyooka❗️ yule atawaingiza tena
Vitani na Mapolisi!!

wkt
MITOTO yake kaificha sehemu salama uko Marekani yule mwehu tunatakiwa tumkazie kweli kweli ✍️
 
Kwamba hata Jamhuri wanaogopa kumwita shahidi aliyeanzisha "Kampeni ya NO REFORM, NO ELECTION"; aje kutoa ushahidi mahakamani kuhusu uasi wa Tundu Lissu; hili pekee linashangaza sana.

Sasa utamnyonga vipi mtu ambaye hata hakubuni uasi wenyewe!
Ahahahahahah..kweli bwana aisee. Hii inafikirisha
 
Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama tena.

Ametambua kilichomfanya anyanyuke, hakin maana mbele ya mahakama, anaamua kukaa kinyonge.
Yani kwakifupi kajiona mjinga kabisa
 
JAMHURI uyo mjomba fungeni tuwaze mengine Watanzania

Ili tusipitie tena kule
tumepitia Mo29 kuzika Watoto vijana inauma sana.
 
Kukinukisha kakinukisha Mwenyekiti wa CHADEMA

Wakafa Watu wa Jamhuri mwenye watu watu wake Jamhuri imechukua hatua kumshikisha adabu Uyo chanzo cha tatizo

Sasa badala mshikamano na Jamhuri ❗️

nyinyi mpo upande wa yule chizi kichwani Bob w Singida
ndani ndani

Akitoka kama ajanyooka❗️ yule atawaingiza tena
Vitani na Mapolisi!!

wkt
MITOTO yake kaificha sehemu salama uko Marekani yule mwehu tunatakiwa tumkazie kweli kweli ✍️
Ni lini utamaliza matibabu yako huko Milembe mkuu.
 
Back
Top Bottom