Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

Kuna famba moja Golugwa ameifanya leo, I hope wale wahuni hawaitumia kumkaanga kesho. Nadhani timu ya utetezi wakifanya mapitio kwa ajili ya kujiandaa na dodosa wataiona na kujiandaa nayo
 
Kwakifupi Lissu anawapanga kimkakati sana. Tusijeshangaa akina Warioba akina Mafwele akina Mbowe wanaombwa kuja kutoa ushahidi
Sidhani kama atamuita Warioba ila huyo Mafwele leo ametajwa kimkakati sana na kina Katuga wanaweza kuingia mkenge kutaka kumsafisha kupitia kesi hii kwa kuwa Golugwa amemuongelea kwa uzuri. Wakijichanganya tu, wakajifanya kulitajataja jina lake katika dodoso, Lissu atapata sababu ya kumuita.

Lissu aliwataja kina Warioba kimkakati sana maana ukisema wote hao walikuwa wanajua mpango, ni kesi nyingine kabisa nzito ya kupanga njama na inabidi ukamate watu wengi sana wazito na uhusishe hadi mabalozi!
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA

SEHEMU YA 15.

Jaji Ndunguru: Sasa tumesikia hizo hoja. Mahakama inaelekeza tuwe focused.

Pande zote mnakuwa guided na hati ya mashitaka. Hata sisi Mahakama tunakuwa guided na hati ya mashitaka.

Sheria inasema mshtakiwa hana duty ya kuthibitisha innocence.

Sisi tukapoamua, tutaamua kama upande wa mashitaka umethibitisha kesi na kama ushahidi unajitosheleza.

Hii ya kuyumbishana, twende huku, twende huku, haina maana. Siyo yote Mahakama itayachukua.

Hatujui upande wa utetezi dimension yako iko aje, ndiyo inatuletea shida.

Kama ataona ushahidi wake unaenda huko, basi mtapata haki ya kufanya cross-examination.

---

Lissu:

Amani Sam Golugwa: Asante. Nitaendelea nilipoishia.

Tarehe 13 Mei 2025, nilipokuwa naelekea Airport hapa Dar es Salaam, nilipokuwa kwenye pointi ya Idara ya Uhamiaji hapo uwanjani, nikiwa tayari nimeshapewa boarding pass, nilifuatwa na watu wawili nikiwa katika kizimba cha Uhamiaji.

Hao watu waliniambia twende ofisini tukazungumze. Tulipokuwa tunaelekea katika hizo ofisi, watu hao waliniambia niko chini ya ulinzi.

Lissu: Watu hao ni akina nani?

Amani Sam Golugwa: Mmoja alikuwa amevaa nguo za Uhamiaji na mmoja alikuwa amevaa kiraia.

Mmoja aliyekuwa amevaa kiraia kabisa aliniambia niko chini ya ulinzi. Huyu ambaye hana uniform akaniambia nimpe simu zangu, na wakazichukua simu zangu zote.

Baada ya dakika takribani tano, wakaja watu watatu wakiwa na bunduki. Mmoja ni yule aliyeniambia niko chini ya ulinzi na mtu mwingine ambaye alikuwa na kitambulisho cha Uhamiaji.

Wakafungua mlango, wakachukua begi langu dogo na kulipekua ndani.

Wakachukua karatasi mbili ambazo zilikuwa na hotuba nilizopanga kwenda kuzungumza katika kikao.

Nilipowauliza tatizo ni nini, kwanini mnanifanyia hivi, kwa sauti kubwa ili watu wasikie, walipomaliza kupekua begi wakanishusha chini. Pale Airport kuna njia za chini, tukapita kwenye tunnel.

Waheshimiwa Majaji, huo mwendo siyo kwamba ulikuwa mwendo rahisi wa kutembea kwa upole.

Wakanisemesha maneno ya kunikosea heshima na kuniudhi. Nachelea kusema, sitayasema mbele ya Mahakama yako Tukufu.

Mmoja aliyeshika bunduki aliniwekea bunduki kwenye sikio la kulia na kuniambia maneno haya:

“Nyie wajinga ndiyo mnapanga safari zenu kwenda kuichafua nchi huko nje, sasa leo ndiyo utaelewa.”

Waheshimiwa Majaji, sikupigwa, ila nililazimishwa kutembea, na kulazimishwa kwenyewe. Naomba mniangalia niwaonyeshe Waheshimiwa Majaji.

Mmoja aliyeshika bunduki alishika hapa. (Anaonyesha kushikwa suruali kwa nyuma.)

Lissu: Baada ya hapo?

Amani Sam Golugwa: Tukatokea uwanjani Airport, wakanizungusha kwa gari kama masaa mawili ndani ya uwanja.

Wakanipeleka kituo cha Polisi kilicho karibu na Airport. Nadhani ni Stakishari. Nilikuwa nimeshachanganyikiwa.

Nilipofika pale nikawauliza, nimefanya nini? Mbona sielewi chochote?

Wakaniambia, wewe unachafua Serikali nje ya nchi.

“Wewe ndiyo inaonekana Lissu anakutuma kuingiza pesa chafu, kwa hiyo Cybercrime inakuhusu na Money Laundering inakuhusu.”

Baada ya hapo, pyuuu, ndani.

Baada ya hapo asubuhi nikachukuliwa na gari. Silioni hata nikiwauliza, na wao walikuwa wananishangaa.

Kwenye gari wao walikuwa saba, katika gari ya Land Cruiser.

Wanne nyuma na bunduki, wawili katikati waliponimiweka.

Mbele kiongozi wao na dereva.

Tukatoka Airport kuelekea kushoto kwake.

Baada ya kupitia Radio Call nikasikia wakisema, “Tupo na Mwewe.”

Waheshimiwa Majaji, katika gari ya kawaida hofu iliniingia. Nikawa nimelala nimeinama, ninalia na sijui kinaendelea nini.

Tukatembea mpaka nikaona tunaingia Central Police.

Lissu: Central Police ya wapi?

Amani Sam Golugwa: Central Police Dar es Salaam.

Kwenye ngazi tukakutana na ZCO Mafwele, na akawa anamwambia Mafwele, “Mzigo huo ni Cybercrime na Money Laundering.”

Mafwele alikuwa ananisemesha kwa lugha nzuri kwa sababu tunafahamiana kutoka Arusha, ila mimi nilikuwa nalia tu huku tunapanda ngazi.

Tulipofika ofisini kwa Mafwele, pakawa na watu wengine na Maafisa wa Uhamiaji.

Wakawa wanahoji safari zangu mbili walizoziiona katika passport.

Nilienda Morocco wakati fulani na nyingine nilienda Mombasa, Desemba 2022.

Waheshimiwa Majaji, niliwaelezea na baadaye nikaambiwa nitoe maelezo kwa kosa kwamba nimekuwa na tabia za kusafiri kutoka nje ya nchi, halafu narudi bila kufuata taratibu na sheria za nchi.

Kabla ya kutoa maelezo, nilihoji sana kuhusu hilo jambo na sikuwa tayari kuhusu jambo hilo.

Nikaambiwa, “Wewe toa maelezo tu, hili jambo litaisha.”

Kwa hiyo nikatoa maelezo na nikatakiwa kuleta uthibitisho wa hiyo safari ya Mombasa ambayo nilikuwa nimesafiri na familia yangu na wazazi wangu.

Hivyo nikaleta uthibitisho wa passport nyingine za familia kuthibitisha kama nilienda na nikarudi.

Lissu: Iliishia wapi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, baada ya hapo nilidhaminiwa na viongozi wa chama waliokuja kunidhamini na kuambiwa, “Nenda nyumbani kwa amani.”

Safari ya kikazi ikawa imevurugika.

Lissu: Hiyo tuhuma ya kwenda nje ya nchi ni ya kweli?

Amani Sam Golugwa: Tuhuma hiyo haikuwa ya kweli, maana Maafisa wa Uhamiaji wakaniambia sikuwa na shida.

Tuhuma hiyo haikuwa ya kweli.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna uwepo wa nchi yoyote ambayo raia wa Tanzania anakatazwa kwenda.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, sina nchi ambayo raia wa Tanzania anakazwa kwenda.

Lissu: Kuna siku nyingine pia ulishawahi kukamatwa?

Amani Sam Golugwa: Novemba 2025, nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu.

Nilipokamatwa, niliwauliza Polisi, nina kosa gani?

Polisi wakaniambia natuhumiwa kwa kosa la ugaidi.

Kosa la kwanza ni ugaidi.

Kosa la pili, kula njama kuharibu miundombinu ya umma.

Tatu, kupanga kuwapiga na kuwadhuru askari wa vyombo vya dola.

Lissu: Ikawaje?

Amani Sam Golugwa: Nikachukuliwa kwenda Central Police Arusha na baada ya masaa mawili nikasafirishwa kuja Dar es Salaam, Oysterbay.

Baada ya muda nilipofika, nikatakiwa kutoa maelezo. Nikakataa kutoa maelezo, kuanzia jina mpaka chochote.

Siku ya pili wakanitoa shimoni na kunitaka kutoa maelezo. Nikakataa pia.

Siku nyingine nikawa mkweli kwamba ili nitoe maelezo, naomba Afande Mafwele na Camilius Wambura waje waniambie ni mimi au la.

Kwa sababu nilikasirika sana.

Kesho yake Mafwele alikuja akaniambia nikubali kutoa maelezo, na wakili niliyemhitaji aje naye alikuja akanishauri kutoa maelezo.

Nikatoa maelezo, na wenzangu nao nikijua kuwa wamekamatwa: Godbless Lema, Boniface Jacob na John Heche.

Tukatoa maelezo, halafu wakaturuhusu wote twende nyumbani.

Na kesho yake tukatakiwa kwenda kwa Mafwele.

Tulipoenda kwa Afande Mafwele, akatuambia, “Nendeni, tutawaita tukiwahitaji.”

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna hatua zozote zimechukuliwa dhidi yako.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna hatua yoyote niliyochukuliwa hadi leo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Duh! Kwa kweli inasikitisha kwa kweli Tanzania hakuna demokrasia vyombo vya Dola vinatumika na Chama tawala kama toilet paper
 
Kwakwel sijui mkuu, nimeongea tu. Hivj haiwezekani eti??
Hata mi sijui sheria mkuu, ila nahisi haiwezekani. Sababu niliwahi kumsikia lissu anawakatalia jamaa mawakili wa serikali ombi lao la kuongeza ushahidi wa october 19, mahakama ndio ikawakatalia. Hivyo nafikiri pia na mashahidi huwezi kuongeza. Pia kuna mahali huwa unwataja mashahidi wako sijui ndio kwenye comittal wanaita, kwenye mabishano yao ya raisi kuwa shahidi ndio nikisiiia maelezo kama hayo kwa lissu kuwa mashahidi wanatajwa hiyo sijui ndio hatua ya comittal baada ya hapo hakuna kitachoongezwa mbele ya safari.
 
Kwakifupi Lissu anawapanga kimkakati sana. Tusijeshangaa akina Warioba akina Mafwele akina Mbowe wanaombwa kuja kutoa ushahidi
Hivi mfano kama hivi walivyomaliza Kuna muda Lissu atapata wasaa wa kuwa na shahidi huyu wa Leo kumuandaa kabla ya kesho siku ya dodoso
 
Hivi mfano kama hivi walivyomaliza Kuna muda Lissu atapata wasaa wa kuwa na shahidi huyu wa Leo kumuandaa kabla ya kesho siku ya dodoso
Kuna namna tu ya kumuandaa lazima iwepo, hatakama kazi hiyo hatafanya yeye sababu na muda na nafasi inawezekana wapo wanaofanya. Wako wana sheria wengi wanaosimamia kesi hii upande wa Lissu
 
Kwa maslahi mapana ya haki sitaitaja ingawa sioni kama inamu incriminate Lissu. Ni kwamba kuna kitu alisema kidogo imeenda na maelezo aliyotoa Lissu na Mnyika.
Wapi ambapo maelezo ya Shahidi yametofautiana na yale ya Lissu na Mnyika?
 
Hatua hii ilipofikia kesi waitwe mashahidi wapya tena?
Upande wa Jamhuri walishafunga ushahidi wao ila upande wa utetezi bado una nafasi na haki ya kuongeza mashahidi zaidi ya wale iliotaja awali.

Tafuta maelezo aliyotoa siku ile Lissu wakati anawataja kina Mpango na Majaliwa kabla hajaanza kutoa ushahidi wake. Alisema ana haki ya kuongeza mashahidi zaidi ya wale aliowataja siku ile.

Wanaojua sheria watatusaidia.
 
MAHAKAMA IMEISHIA HAPA KWA LEO TUKUTANE KESHO

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa muda umeisha, tunaomba Mahakama ihairishe kesi hadi kesho kwa ajili ya maswali ya dodoso.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasemaje?

Lissu: Sawa, Mheshimiwa Jaji.

Jaji Ndunguru: Shauri linapangwa kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuendelea kuulizwa maswali ya dodoso hapo kesho saa 3:00 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.

MUWE NA JIONI NJEMA
Ahsante Manyanza,usiku Mwema na tukutane asubuhi njema!
 
Back
Top Bottom