Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 18

Na kulikuwa na mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi za Afrika na Jumuiya ya Ulaya (AU-EU Summit).

Nilikuwa Ubelgiji, akanitumia ujumbe kupitia watu wake.

Watu wanasema niliomba; hapana, sikuomba. Tuonane yeye ndiye aliomba tuonane.

Wakati huo Mwenyekiti Mbowe yupo gerezani kwa miezi saba.

Nikawapigia simu viongozi wenzangu, tukashauriana na nikaona ni jambo zuri.

Tukaenda, tukaonana, na akasema anataka amalize matatizo aliyoanzisha mtangulizi wake.

Nikamuambia aanze na Mwenyekiti wetu ambaye yupo gerezani kwanza kwa kesi za kina Kingai.

Pia tuzungumze habari ya Katiba mpya na ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwisho nikamwambia kuwa mimi na Mheshimiwa Lema na Wenje tumekimbia nchi kwa usalama wetu.

Naomba utangaze kama tutakuwa salama tukirejea.

Akatangaza Waziri yule anaitwa Hamad Masauni Bungeni kwamba, “Mliopo uhamishoni rudini.”

Na baadaye akamuachilia Mheshimiwa Mbowe, ndipo tukapata faraja mimi na wenzangu kurudi.

Na tuliporudi tukamueleza tunataka wenzetu waliofunguliwa mashitaka ya kisiasa na walifutiwa mashitaka.

Tukaanza mazungumzo na yakaitwa Maridhiano, timu ya CCM chini ya Abdulrahman Kinana na CHADEMA chini ya Mbowe. Mimi nilikuwa sijarudi.

Tukapeleka mapendekezo kuhusu Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kwa maandishi. Hatukuwa tunapiga soga tu.

Na kwa ratiba yetu tuliyopendekeza, ilikuwa Katiba mpya inapatikana mwaka 2024, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi.

Mapendekezo yetu kwa maandishi, wao wanatujibu kwa mdomo.

Tukiuliza kuhusu Katiba mpya, tunapigwa danadana.

Matokeo yake tunapigwa picha tu, na picha wanazipenda.

Mimi nilirudi Januari 2023, nikakaa na wenzangu.

Tukasema tuwaandikie barua rasmi ya mapendekezo yetu.

Tarehe 31 Mei 2023 wakatujibu barua yetu kwa maandishi, wakiwa wamekataa mapendekezo yetu yote.

Tukakaa tukasema, kama wamekataa mapendekezo yetu, maridhiano ni kitu gani zaidi ya kwenda kunywa chai na kukaa na watu wa CCM, hiyo tarehe 31 Mei 2023?

Baada ya hapo, Waheshimiwa Majaji, tukazungumza kama chama, tukasema lazima kampeni ya Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi iwe ya Watanzania.

Tukahamasisha kampeni iwe ya wananchi, wapiganie mabadiliko nchi nzima.

Tuligawana nchi, mimi na timu yangu na Mwenyekiti na timu yake, tukazunguka nchi nzima.

Joto lilipopanda la kisiasa, watu wetu walianza kutekwa na kuuawa na kesi zikaanza upya.

Tumekwenda hivyo mpaka 2024, na Novemba 2024 palikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji.

Tumejadiliana na kuvutana sana katika chama, je, twende au tusiende katika mazingira ambayo hakuna mabadiliko yoyote?

Tukasema twende kwenye uchaguzi.

Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji, Waheshimiwa Majaji, hausimamiwi na Tume ya Uchaguzi. Unasimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, basically na Rais mwenyewe.

Yule Waziri wa TAMISEMI yupo tu, lakini Waziri ni Rais mwenyewe.

Uchaguzi huo maana yake unasimamiwa na Rais mwenyewe.

Anayetunga kanuni za uchaguzi ni Waziri wa TAMISEMI.

Aliyetunga kanuni wakati huo ni Waziri wa TAMISEMI, mkwe wa Samia.

Kwenye uchaguzi ule wa 28 Novemba 2024, wagombea wote wa vyama vya upinzani nchi nzima walienguliwa.

Wakarudi yale ya Magufuli ya 2019, ambapo walifuta wagombea wote.

Asilimia 100 ya wenyeviti wa mitaa na asilimia 100 ya wenyeviti wa vitongoji ni CCM hapa tulipo, Waheshimiwa Majaji.

Walifyeka wote; aliyebisha aliumizwa au akauawa.

Mimi nilizika Mwenyekiti wa Kitongoji Manyoni.

Kama unaua kwa sababu ya kitongoji, ubunge na urais utafanya nini?

Ili kushinda vitongoni, ilibidi watoe kafara ya damu ya watu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
so what? :pedroP:
 
Unaiufanya huu uzi uzidi kupata impressions na kwenye algorithm ya JF uonekane “hotcake” bure kwa irrelevant comments zako PSYCHO
tuliza mihemko useless bas gentleman dhidi ya maoni yangu huru na itapendeza zaidi :1Head:
 
Gentleman,

Naona Lissu anamwaga nondo za moto.

Hapa nimeshikwa na tumbo la kuhara najamba sana.

Mungu aingilie kati huyu Lissu amalize tu.
Yes,
ni kweli,
anadai eti mbowe kaonekana kwenye uzinduzi wa bwawa la mwalimu nyerere wakati aliestahili kua pale ni yeye, angalia sifanye hiyo mambo pembeni, jitahidi ulenge maana huko mtwara unakoishi kulenga ni muhimu sana :pedroP:
 
We ndo useless that’s why U know nothing about technology about .3 ya comments kene huu uzi ni zako you know umeusukuma huu uzi kuwafika wangap zaid?
uko pointless, huna maoni ni suala la kukaa kimya tu na itapendeza zaid gentleman,
makasiriko ya nini sasa kwenye maoni huru ya wengine?

wajibu wangu ni kueleza ukweli mtupu kwenye mambo ya msingi tu na kusonga mbele, hayo mengine hayanihusu hata kidogo :1Head:
 
Tarime - Nyamongo, Waheshimiwa Majaji Tarime ni muhimu sio kwasababu ni Ukweni tu lakini kwa miaka 3 nilitoa watu 466 kwenye Gereza la wilaya ya Tarime na Gereza la Butimba Mwanza. Walifungwa kwa makosa ya uongo tu ili wapewe wazungu wachimbe dhahabu. Miaka 3 nilitoa watu 466 akiwemo Chacha Wangwe marehemu akiwa Mbunge.
Huyu Jamaa record yake haitavunjwa kwa miaka 1000 mbele
 
ok.
ishi na hayo maelezo ili isijekua surprise kwako katika wakati muafaka :1Head:

Wewe ambaye una uhakika kuwa atanyongwa ndo ujiandae na mineng'uo na kung'emuka.

Asiponyongwa utang'emuka kwa kula matapishi yako mpaka tone la mwisho.

Akinyongwa mineng'uo itakuwa ya utetezi maana haitakuwa na comeback nyepesi kutoka ndani na nje ya nchi.

Vyovyote vile itapendeza usipoleta porojo.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 19

Tarehe 3 Desemba 2024 tukakaa kutafakari kama CHADEMA, wakati huo mimi sijawa Mwenyekiti wa CHADEMA bado.

Kama wanaua wenyeviti wa vitongoji, uchaguzi Mkuu utakuwaje?

Ndiyo yakazaliwa maneno ya NO REFORMS, NO ELECTION.

Tukasema tutafanyeje? Tukasema tutaenda kwa Watanzania, kwa kila aliye rafiki atusikilize na kila anayetuona adui atusikilize.

Tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti Mbowe akatangaza hadharani kupitia waandishi wa habari kuhusu NO REFORMS, NO ELECTION.

Jaji Ndunguru: Tarehe ngapi unasema?

Lissu: Tarehe 10 Desemba 2024.

Tukajiliuza kwenye vikao vya chama, Kamati Kuu, je, utekelezaji utakuwaje?

Tukasema tuna uchaguzi Mkuu wa chama Januari, mwezi ujao.

Tumalize kwanza uchaguzi wa chama, kisha tuwapelekee wajumbe wa Mkutano Mkuu, tupate mandate, halafu tupate mkakati wa utekelezaji.

Waheshimiwa Majaji, tarehe 20 Januari 2025 tukafanya kikao cha Baraza Kuu la chama.

Baraza Kuu la CHADEMA, kwa haraka haraka Waheshimiwa Majaji, ni equivalent ya Halmashauri Kuu ya NEC ya CCM.

Na Kamati Kuu ya CHADEMA ni equivalent ya Kamati Kuu ya CCM.

Na Baraza Kuu ndiyo linatengeneza ajenda ya Mkutano Mkuu.

Kwa hiyo, Kamati Kuu ya tarehe 20 Januari tulipeleka ajenda ya NO REFORM, NO ELECTION ili iende Mkutano Mkuu.

Na ilipita Mkutano Mkuu iwe sera rasmi ya chama.

Na Baraza Kuu la chama likapitisha kwa moyo mmoja NO ELECTION, NO REFORM, na kukubali kuipendekeza kama ajenda katika Mkutano Mkuu uliokuwa unafanyika kesho yake, tarehe 21.

Kwa hiyo, tarehe 21 Januari 2025 kwenye Mkutano Mkuu wa chama yalifanyika mambo mawili:

1. Mkutano Mkuu ulijadili na kupitisha hoja ya NO REFORM, NO ELECTION.

Baraza Kuu jana na Mkutano Mkuu ule, Mwenyekiti alikuwa Freeman Aikael Mbowe, mimi nilikuwa sijachaguliwa.

2. Jambo la pili, tukafanya uchaguzi wa kihistoria ambao haujawahi kutokea Tanzania na nchi yoyote Afrika.

Completely free and transparent election haijawahi kutokea, na tuliita mabalozi waje kushuhudia.

Na mimi nikashinda na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Kwa Katiba yetu, Mwenyekiti anayeshinda anateua Katibu Mkuu, manaibu Katibu Wakuu na Wakurugenzi 5 wa chama.

Kama Mwenyekiti mteule, nilimteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu na Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Na samahani, nilimteua Wakili, sikumbuki vizuri jina, kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Kwa hiyo, baada ya hapo tukaanza kuandaa mkakati wa utekelezaji wa NO REFORM, NO ELECTION.

Tarehe 31 Januari 2025 tukaita Kamati Kuu Bagamoyo, tukapitisha mkakati mkuu wa Bagamoyo.

Kwamba tunaenda kuhamasisha nchi nzima kutumia njia za kidemokrasia.

Njia za kidemokrasia ni maandamano, boycott (kususia), njia za kidemokrasia zinazoruhusiwa na sheria Tanzania.

Tutaenda nchi nzima kutumia njia za kidemokrasia za amani, wala hatukusema tunaenda kumpiga mtu au kuchoma gari ya mtu.

Tunaenda kuhamasisha, na ili umma uhamasike tulisema tutaenda nchi nzima.

Na nchi nzima kwa njia za kidemokrasia za amani.

Lazima tuzungumze na Watanzania kujua hatua katika kuleta mabadiliko.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Wewe ambaye una uhakika kuwa atanyongwa ndo ujiandae na mineng'uo na kung'emuka.

Asiponyongwa utang'emuka kwa kula matapishi yako mpaka tone la mwisho.

Akinyongujiujimineuo itakuwa ya utetezi maana haitakuwa na comeback nyepesi kutoka ndani na nje ya nchi.

Vyovyote vile itapendeza usipoleta porojo.
gentleman,
wajibu wangu daima tangu nijiunge JF ni kueleza ukweli mtupu kwenye mambo ya msingi tu.
porojo na mambo mengine useless kama hayo anayoeleza huyo kibaraka mengi hua nayapuuza tu.

na vyovyote itakavyo kua,
nitakua hapa JF tena nikiwa mwenye nguvu zaidi na kitofati zaidi gentleman :1Head:
 
Back
Top Bottom