TUNDU LISSU ANAENDELEA
KESI IMEREJEA
Ameanza kuingia Lissu kabla hajakaa, wakaingia Majaji.
Mahakama imerejesha utulivu wake.
Mawakili wa Serikali wanateta. Majaji wanateta.
Lissu anatabasamu na kuwapungia watu mbalimbali kimya kimya.
Jaji Ndunguru: Tuendelee upande wa mashitaka.
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, baada ya mapumziko mafupi kesi inaendelea na kolamu inabaki vilevile.
Mheshimiwa Lissu amesimama kizimbani tayari.
Jaji Ndunguru: Endelea, shahidi.
Lissu: Asante, Waheshimiwa Majaji.
Waheshimiwa Majaji, masuala ya uchaguzi, masuala ya Katiba na masuala ya uendeshaji wa nchi yasipowekwa sawasawa huwa yanaleta maafa kitaifa.
Lissu anasisitiza:
Huwa yanaleta maafa, na leo mtu yeyote anaposema hivyo hataonekana kichaa.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, ulikuwa ukisema hivyo unaonekana kichaa.
Sisi ni Jamhuri ya Muungano. Wengi wetu, kwa sababu hatufundishwi historia sawasawa, hatuelewi Jamhuri ya Muungano ilikujaje.
Tunafikiri Nyerere na Karume walikaa kwa sababu ya busara wakasema tuungane.
Waheshimiwa Majaji, Zanzibar walifanya mapinduzi makubwa kwa umwagaji damu mkubwa sana kwa sababu ya matatizo ya uchaguzi.
Ushahidi wangu ni ripoti ya Tume ya Jaji Nyarali ya tarehe 17 Februari 1992.
Inasema baada ya Wazanzibari kuchoka kila uchaguzi kuibiwa, watu wakachoka wakafanya mapinduzi, na Tume ya Nyarali inasema mapinduzi yanaambatana na umwagaji wa damu.
Kwa hiyo, hii Jamhuri ya Muungano imekuja baada ya watu kuchoka maonevu ya mambo ya uchaguzi.
Nimekuwa nikisema tangu 1992, tumekuwa tukikataa kuona huo ukweli.
Oktoba mwaka jana, kama hatujajifunza, tutakuwa tuna matatizo.
Tume ya Nyarali na Jaji Kisanga inasema yaliyotokea mwaka jana yanatokana na kutotatuliwa kwa muda mrefu kwa matatizo ya vyama vingi, madai ya tume huru ya uchaguzi, Katiba mpya na madai ya demokrasia.
Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Othman Chande pia.
Kwenye ushahidi wangu nitaonyesha jinsi tulivyofanya na kujitahidi kila namna kuepusha yaliyotokea Oktoba 29 mwaka jana.
Hatukusikilizwa, tukaonekana kuwa vichaa.
Masuala ya uchaguzi siyo masuala ya kuchezea, na ukichezea matokeo yake ni haya.
Naomba nimalizie ya uchaguzi kwa kusema:
Mfumo wetu wa uchaguzi una matatizo mengi ya muda mrefu ambayo yanajulikana.
Yameandikwa na kila tume.
Yameandikwa na wale waliotoka nje kuja kutazama chaguzi zetu kwamba matatizo haya msipoyatatua, mnaenda kubaya.
Waheshimiwa Majaji, baada ya Magufuli kufariki na Samia kuingia madarakani, nilikuwa uhamishoni.
Nikaja kukoswa-koswa hapa, nikakimbilia Ubalozi wa Ujerumani, ikabidi niondoke.
Tarehe 17 Februari 2022, Rais Samia alifanya ziara Ulaya.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI