Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 15
Ndiyo imetufikisha leo hii hapa na kesi ya uhaini.

Ijumaa nilisahau kuwaambia kuwa mwaka 2020 nilirudi kutoka uhamishoni kuja kumkabili Magufuli.

Nikagombea Urais mwaka 2020, na ni wazi sikuchaguliwa. Ningechaguliwa, leo nisingekuwa hapa.

Sheria ya uchaguzi wakati ule palikuwa na kifungu kwamba matokeo ya uchaguzi yatatangazwa jimbo kwa jimbo na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.

Ninachotaka kusema, zamani Tume ya Uchaguzi ilikuwa inatangaza matokeo ya uchaguzi katika Gazeti la Serikali, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo na ya Urais.

Mwaka 2020 kuna matokeo ya uchaguzi kata kwa kata na jimbo kwa jimbo.

Lakini hakuna matokeo ya Urais ya 2020 yanayoonyesha Magufuli alipata kura ngapi.

Na kamwe hamtokuja kuyaona. Kwa nini? Ni kwa sababu Tume ni ya ki-CCM.

Na sina uhakika kwamba matokeo ya mwaka jana, kama yenyewe yalichapishwa gazetini.

Kuna mambo ya ajabu nchini yanaendelea.

Soma ripoti ya Tume ya Uchaguzi kila mwaka, lazima kuna wadudu.

Uchaguzi wa 2020 ulitia fora kwa wabunge 28 kupita bila kupingwa baada ya wapinzani wao kuondolewa na Tume, wengi wao wakiwa ni CHADEMA.

Tume ambayo Mkurugenzi wake leo ni Mbunge wa CCM.

With Magufuli, ikawa ilikupambana na CHADEMA ni kuwaengua wagombea wa CHADEMA nchi nzima.

Mwaka 2019, wagombea wote wa Serikali za Mitaa wa CHADEMA walienguliwa.

2020 palikuwa na mass disqualification. Walikuwa wagombea 68, wakabaki 34 baada ya kupambana.

Madiwani pia mass disqualification, na mara nyingine mwaka 2020 pakawa na mauaji sana.

Kwa uchaguzi wa 2020, ukisoma taarifa za watazamaji wa uchaguzi wa kimataifa, wakiongozwa na watazamaji wa Umoja wa Afrika, utakubaliana nao kuwa hapakuwa na uchaguzi.

Palikuwa na vurugu, vurugu za Polisi na usalama wa taifa.

Wagombea wetu wanatekwa na Polisi pamoja na Usalama wa Taifa.

Niliposema Polisi wanatembea na vibegi migongoni, huo ni ukweli kutoka moyoni mwetu.

Ripoti ya uchaguzi 2020 ilikabidhiwa Rais Samia Agosti 2021.

Na katika sherehe ya 2021 ya kukabidhiwa ripoti, Samia alisema hivi: “Tuliwapiga fiksi, tukawaengua.”

Watazamaji wa kimataifa wa uchaguzi wakasema bila mabadiliko ya Katiba mpya na sheria ya uchaguzi, 2025 itakuwa maafa.

Ripoti ya watazamaji wa kimataifa kutoka Afrika ilikuwa bora sana.

Walisema Tanzania haina uwezo wa kuendelea kuendesha uchaguzi bila maafa kama hawatakuwa na Katiba mpya, tena ya Warioba, na Tume huru ya uchaguzi.

Hao ni waangalizi wa Afrika.

Magufuli akafa, akaja Samia.

Mwenyekiti wetu akadai Katiba, akafunguliwa kesi ya ugaidi, akakaa Ukonga miezi 8, pale ninapokaa mimi.

Tukapambana na kesi ya uongo.

Siku ya kutakiwa kujitetea hatukumuona, bali akatokea Mahakamani Ikulu.

Na jana nimeambiwa alikuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere wakati Mwenyekiti wake nikiwa Magereza.

MAHAKAMA: Kicheko.

Wakili wa Serikali Mkuu anasimama.

“Samahani, Waheshimiwa Majaji, muda wa mapumziko.”

Lissu: “Hilo naliunga mkono, Waheshimiwa Majaji. Nilisahau kidogo.”

MAJAJI: Wanateta.

Askari Magereza wanasogea katika kizimba cha shahidi.

Lissu amebadilishiwa kizimba kutoka kile cha mshtakiwa; siku hizi 2 anatumia kizimba cha shahidi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
Nimecheka,mahakamani ikulu na Jana nasikia alikuwa kwenye uzinduzi wa umeme,Wakati mwenzake nipo Gerezani!mmmh
 
Yule mahakama "Yuda" nilidhani ndiye bosi wenu kumbe naye ni kidampa tu.

Kile kigazeti chake nasikia hata Lumumba hawakitaki... Sijui nani anakifadhili.
hivi gentleman,
yale mabegi yote yaliyojaa matakataka tupu ya huyo mtuhumiwa anaesubiri kunyongwa, hua yanamsaidia nini haswa au ni mazoezi tu ya kubeba mizigo isiyo na faida yoyote?🐒
 
Hahaha 😂
Ningekua yeye ningejikita kwenye uhaini. Lakini sijui kwanini Lissu kaamua kujitetea mwenyewe. Hiyo case ni nzito na tena ya uonevu. Angekuwa na wakili wake kwa maoni yangu angejitetea vizuri zaidi.
Kwenye ushahidi unatakiwa ueleze facts tu siyo ufanye submissions, hatutegemei aanze kutaja vifungu vya sheria na case laws katika hatua hii. Hivyo ni hiyo historia inafaa sana itafika wakati wa final submission baada ya mashahidi wote kwisha ndipo tunategemea atakuja na submission ndefu ya kisheria kuonesha ni jinsi gani elements za uhaini hazijatimia. Kumbuka mwenye jukumu la kuthibitisha ni jamhuri. Kwa kesi ilivyo hata asingejitetea kwenye mahakama huru hakuna hatia
 
Naona kiongozi wa jopo la majaji (Jaji Ndunguru) anamkazania mtuhumiwa amalize ushahidi wake haraka! Ni kwamba anawachosha, kumsikiliza au tayari wana hukumu yake wameshamuandalia pembeni?

Mbona kule nyuma mawakili wa serikali walipo poteza muda kupitia njia mbalimbali, hatukona akiwakazania kiasi hiki cha leo!
Na aliponichanganya nikusema hiyo historia Lissu atawaandikia kitabu watu wasome. Kama mtoto wa falsafa najiuliza maswali kadhaa.

Je majaji washaandaa hukumu mapema kuwa Lissu hajatiwa hatiani?.
Je Lissu anawachosha hawa majaji wanatamani amalize haraka?.
Je majaji wanaona Lissu ni kichwa kiasi kwamba wanataka awaandikie raia wote wa nchi hii madini yahusuyo historia ya nchi yetu na mfumo wetu wa hovyo wa uchaguzi?

Anyway wale vilaza kina Lia Lia na Mwashamba wajifunze mengi kutoka kwa Lissu waache kukaza mafuvu yao.
 
Hii nchi ukiwa mtetea haki za raia tayari unakuwa adui wa nchi.
wapo watu duniani wamezaliwa kwa ajili ya watu wengine. huu ni utumishi kwa Mungu kabisa! T.L ni mmojawapo wa watu hao.

unadhani angeamua kuwasaliti WANANCHI kwa kuzichukua zile pesa alizopelekewa na Abduli haya yote yangemkuta? Aliamua kusimama upande wa WANANCHI kwa gharama zake. hivyo hateseki bali anamtumikia Mungu. Ndivyo utumishi ulivyo kuteseka kwa hiyari yako kwa ajili ya watu wengine.

God bless u servant of A living God. AMEN.
 
Back
Top Bottom