Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Hahaha 😂
Ningekua yeye ningejikita kwenye uhaini. Lakini sijui kwanini Lissu kaamua kujitetea mwenyewe. Hiyo case ni nzito na tena ya uonevu. Angekuwa na wakili wake kwa maoni yangu angejitetea vizuri zaidi.
Tundu Lissu ni mwanasiasa anajiamini na anaamini kwenye uwezo wake kuliko mtu mwingine yoyote, namna atakavyojitetea mwenyewe ni tofauti na mtu mwingine atakavyomtetea ndio maana akaamua ajitetee mwenyewe.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 22
Nilipakiwa na RCO Mkunja, namkumbuka. Alikuwa mkatili sana, na nilikuwa namwambia, “Usijali, Afande, yataisha.”

Namkumbuka alikuwa awe shahidi, ila hawajamleta hapa. Nilikuwa nije nimseme mbele yenu hapa.

Nilibebwa usiku usiku, na mimi siyo mzima sana.

Nikaletwa Dar es Salaam, nikapelekwa Shimoni. Na pale Shimoni kuna mbu wakubwa kama nzi wa chooni, wana supply ya damu muda wote, lazima wanenepe.

Nilikaa mule kuanzia alfajiri hadi majira ya saa 6 na saa 7, nikapelekwa kwa Deputy ZCO, George Bagyemu (PW1). Ndiyo aliyeniambia nakabiliwa na shtaka la uhaini na shtaka la pili, kuchapisha habari za uongo.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mimi siye niliyeandaa mkutano.

Na kuhusu uchapishaji, shahidi pekee wa kuona mwenyewe na shahidi pekee aliyesikia maneno yangu, na kwa mujibu wa sheria yetu ya ushahidi, The Best Witness ni PW17 pekee.

Wengine wote hawakuwepo katika mkutano.

Na PW17 ndiye aliyesema yeye ndiye amechapisha.

Yeye ndiye amepeleka kurasa za Jambo TV za X na Instagram.

Yeye na wenzake walifanya hivyo kwa kamera 3 za Sony HXR-100, kama sikosei.

Kwa hiyo, kwenye uchapishaji, PW17 amekuja kusema yeye ndiye amechapisha.

He did everything, na siyo mimi.

Kuhusu nani aliyemwalika, amesema siyo mimi.

Aliambiwa na Mkurugenzi wake, John Marwa, “Nendeni mkakave mkutano wa CHADEMA.”

Na John Marwa, kwa maneno yale, anasema aliambiwa na Brenda Rupia.

Haya maneno walikuwa wanayajua polisi na waendesha mashitaka.

Maelezo haya ni ya tarehe 8 Aprili 2025, na walikuwa nayo tangu tarehe hii 8. They knew it.

Nani aliyeandaa mkutano na nani aliyewaalika?

Wananishitaki na kunituhumu kuhusu mkutano ambao wanajua umeandaliwa na Afisa Habari wa chama, na wananishitaki kuhusu kuchapisha wakati wanajua aliyechapisha.

Walichotaka ni mshitakiwa kwa kosa lisilo na dhamana aende magereza. All they want.

Mapolisi wanasemaga, “Mpe kesi ya kichwa, akakae gerezani.”

Sasa mimi nimepewa kesi ya kichwa, nikakae gerezani, na wamefanikiwa.

Kwa ushahidi huu, mimi siyo muhaini.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nilizungumza kitu gani?

Wanawaleteeni maneno ya nusu dakika tu, hawasemi masaa 3 niliyazungumza.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nilizungumza kuhusu masuala ya matatizo ya Tume ya Uchaguzi na Katiba yetu.

Nilizungumza juu ya masuala ya sheria zetu za uchaguzi na matatizo yake katika utekelezaji, uchaguzi baada ya uchaguzi, uchaguzi baada ya uchaguzi.

Na matatizo ya muundo wa Tume. Niliwaambieni hii ni Tume ya Rais, na kwa sababu ni Tume ya Rais, ni Tume ya CCM.

Na mifano nikiwapa kuhusu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Agustine Ramadhani, alitaka kugombea Urais 2015.

Watu wakamwambia, kama ilivyokuwa kwa Jaji Mark Bomani, kwamba wewe ulikuwa Jaji Mkuu, je, umekuwa CCM lini?

Na Jaji Mkuu Agustine Ramadhani alikuwa Meja Jenerali wa Jeshi, je, amekuwa lini CCM?

Kwa sababu wote hao ni CCM.

Waheshimiwa Majaji, tupo Dar es Salaam, na Dar es Salaam ni mkoa wenye watu wengi kuliko yote, una majimbo 10 ya uchaguzi.

Zanzibar, ambayo haina hata moja ya tano ya wakazi wa Dar es Salaam, ina majimbo 50.

Why? Kwa sababu Tume haina utaratibu bora wa namna ya kutengeneza majimbo ya uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Chawa unayemsema ni Mimi? Wala sipo upande wa serikali hata kidogo. Niliona tu utetezi wake ungejikita kwenye kosa. Lakini wadau wamefafanua vizuri kwamba pale anaeleza mshtakiwa ni nani. Na I agree it make sense.
Kwenye hili jukwaa Kuna upuuzi Fulani upo yaani ukiwa upo kinyume kimtazamo moja kwa moja unaonekana utakuwa kwenye upande mwingine either ni Serikali au Upinzani kitu ambacho ni wrong wengine hawana vyama vya siasa tunahitaji kubishana kwa hoja ni moja kati ya sehemu ya kujifunza na kupata maarifa mapya.
 
Kwenye hili jukwaa Kuna upuuzi Fulani upo yaani ukiwa upo kinyume kimtazamo moja kwa moja unaonekana utakuwa kwenye upande mwingine either ni Serikali au Upinzani kitu ambacho ni wrong wengine hawana vyama vya siasa tunahitaji kubishana kwa hoja ni moja kati ya sehemu ya kujifunza na kupata maarifa mapya.
Exactly 💯. Pia hakuna haja ya kumshambulia mtu kisa mawazo yake! Utasikia huna akili! Mbulula etc
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 23

Kwa sababu utaratibu bora tuliotengenezewa na wakoloni unaosema mbunge awe na uwakilishi wa wananchi uliondolewa.

Badala yake, wanaangalia milima, mapori na eneo la kijiografia. Matokeo yake unakuwa na utaratibu wa wabunge ambao hauna uwiano, na hilo ni jambo la Kikatiba moja kwa moja.

Nikawaelezea watia nia wangu juu ya utaratibu mzima wa uandikishaji wa wapiga kura.

Watu wengi ukiwauliza kama watu wana haki ya kupiga kura, watasema ndiyo, kwa sababu ipo katika Ibara ya 5 ya Katiba.

Kwa nini hawajaweka katika sheria? Huwezi kwenda Mahakamani ukasema umenyimwa haki ya kupiga kura.

Kuna mmoja alienda Mahakamani kuwa amenyimwa haki ya kupiga kura, Mahakama ikamfukuza.

Kwa sababu nchi yetu haina sheria inayosema hivyo juu ya haki ya kupiga kura.

Kupiga kura ni utaratibu uliowekwa na Tume ya Uchaguzi.

Daftari la wapiga kura ni ujinga mtupu, hakuna haki ya kupiga kura mle.

Wameanzisha Daftari la Wapiga Kura kuiba kura za CCM.

Mfumo wetu wa kupiga kura umeharibiwa na CCM.

Haya ndiyo nilikuwa naongea na watia nia.

Nilizungumza na watia nia juu ya matatizo ya mfumo mzima wa nomination of candidates, juu ya engua-engua ya wagombea.

Wagombea wanaenguliwa na huwezi kuishitaki Tume mpaka mara baada ya uchaguzi.

Na kwa mtu ambaye amefanya kesi nyingi za uchaguzi kama mimi, hakuna namna Tume ikishatangaza mtu, kuishitaki na kushinda.

Waheshimiwa Majaji, katika ripoti moja wapo ya watazamaji wa uchaguzi, TEMCO, wamesema haijawahi kutokea katika nchi hii mgombea hata mmoja wa CCM kuenguliwa.

Kwa sababu gani? Tume ni ya CCM.

Kwa hiyo, hutakaa usikie mgombea wa CCM ameenguliwa. It has never happened.

Nikizungumza juu ya matatizo ya mfumo mzima wa kampeni za uchaguzi.

Waheshimiwa Majaji, kwa sisi ambao tumeshiriki katika uchaguzi, tunapoenda katika kampeni ukiwa mgombea wa upinzani, ushindani tu siyo na CCM, bali unashindana na polisi, watendaji wa vijiji na kata, maafisa tarafa, ma-DC na ma-DSO na wakurugenzi, pamoja na mfumo mzima wa kiserikali.

Watakuvurugia mikutano yako, watafanya kila aina ya uchafu na kuhakikisha kila namna kampeni haifanyiki sawasawa.

System nzima ipo stacked, na mfumo wa uchaguzi ukishinda, hujashinda CCM peke yake; mara nyingine umewashinda mahakimu.

Kwa sababu mahakimu wanatakiwa waapishe wagombea, na mahakimu wanajificha wasiapishe wagombea wa upinzani.

Aliyekuwa mgombea wetu wa Jimbo la Mrimba, anaitwa Suzan Kiwanga wa Mrimba, anarudisha fomu, akakuta Mkurugenzi kafunga ofisi, hayupo.

Ilipofika saa 11, Mkurugenzi kajitokeza, kasema, “Umechelewa, Mama,” na mgombea wa CCM kapita bila kupingwa.

Kwa hiyo, mfumo mzima wa uchaguzi umekaa kuipendelea CCM.

Mimi nimegombea urais, nimepigwa mabomu na polisi Kilwa Kivinje, Tarime, Mugumu Serengeti.

Nimesimamishwa kampeni na Tume siku 10.

Kuna wakati Magufuli alikuwa anakata pumzi, wanabidi waanze kumpepea-pepea. Hivi mimi nimesimamishwa kampeni kwanza.

MAHAKAMA KICHEKO 😀😀😀

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Shauri la uhaini namba 19605/2025 dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, kuendelea leo Agosti 24, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, ikiwa katika hatua ya uwasilishaji wa ushahidi wa mshtakiwa mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru

Ikumbukwe Agosti 21, 2026 Tundu Lissu alikutwa na kesi ya kujibu, ambapo alipewa nafasi ya kujitetea na akatumia nafasi hiyo kuwataja mashahidi wake.

Lissu anatarajiwa kuendelea kutoa maelezo yake huku akisubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu baadhi ya mashahidi aliopendekeza ambao upande wa mashtaka umewawekea pingamizi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Kesi imeanza

Mwenyekiti Mhe. Lissu anaingia.

Majaji nao wanaingia muda huo huo.

Mwenyekiti Mhe. Lissu amevaa Tshirt nyeupe ya Stronger Together, No Reforms, No Election na Jeans ya Dark Blue kama kawa halafu Dread zake zinamea kwa kasi sana.

Majaji wanateta kidogo na kujiandaa na kesi kuanza.

Karani anawasha MIC na kusoma namba ya kesi, Jamhuri vs Tundu Lissu.

Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye Zengeli, Nasoro Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri. Na wanadai wako tayari.

Jaji Ndunguru: Sasa shahidi endelee au nikukumbushe ulipoishia?

Lissu: Naomba nikumbushe.

Jaji Ndunguru anasema uliishia pale uliposema kuanzia 2020 umefanya utafiti wa masuala ya uchaguzi toka ukoloni.

Lissu: asante, sasa naomba niendeleeee.

Waheshimiwa Majaji siku ya kwanza nilisema hii ni kesi ya kisiasa na kusema Taasisi mbalimbali zimelaani ikiwemo Jumuiya ya Ulaya, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola.

Hizo zote ni taasisi za kimataifa na bado zipo zingine taasisi za kikanda zipo na taasisi za Waafrika wenzetu sio wazungu peke yake.

Kesi ilipofunguliwa mwaka jana Taasisi za Kisheria za nchi yetu wenyewe na nchi jirani na sisi zilitoa matamko hadharani za kulaani mashtaka haya na kuyaita mashitaka ya uonevu. Na matumizi mabaya ya mfumo wa uendeshaji wa Mahakama.

Taasisi hizo ni pamoja na-;

1. Chama cha Mawakili wa Afrika ya Mashariki

2. Chama cha Wanasheria wa nchi wanachama wa SADC

3. Muungano wa Wanasheria Afrika (Pan African Lawyers Union)

4. Chama cha Mawakili wa Zambia

5. Chama cha Mawakili wa Kenya

6. Chama cha Mawakili wa Tanganyika. ambacho nilikuwa Rais wake mwaka 2017 kwa muda mfupi.

Taasisi zingine zilizotoa matamko kuhusu mimi kuonewa na kuwekwa ndani visivyo

1. Tume ya wanasheria Duniani, International Commission of Juris Kenyan Chapter

2. Armnest International Regional Office for Estern and Southern Africa

3. Ugandan Law Society

Waheshimiwa Majaji pia kauli za kulaani mashitaka haya zimetolewa na

1. Democratic Union of Africa, inayojumuisha vyama barani Afrika vyenye mrengo wa kisiasa Afrika sawa na CHADEMA.

2. Platform of African Democracy (PAD) ambalo ni jukwaa la vyama vya kidemokrasia kutoka nchi 17 hapa Afrika.

Waheshimiwa majaji kwa kipekeee kabisa.

Tarehe 30/07/2025 Tume ya Haki za Binadamu na Haki za Wananchi ya Afrika, ambayo ni chombo cha Umoja wa Afrika cha kusimamia haki za binadamu yenye Makao yake Arusha, Tanzania. (ACHPR)

Ambacho ni chombo mahsusi kilifanya kikao cha dharula kujadili mashitaka haya na katika kikao chake ikapitisha azimio linaloitwa AZIMIO KUHUSU HALI YA HAKI ZA BINADAMU KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Azimio HACHPR/RES.640 (LXXXIV) Kikao cha 84 cha Tume/2025. Azimio hilo linazungumzia kwa masikitiko makubwa kwa kufunguliwa kwa kesi hii na kukamatwa kwangu.

Tume ya Umoja wa Afrika ilisema Serikali ya Tanzania ina wajibu wa kufuata matakwa ya haki za binadamu kama ilivyoridhia mwaka 1984. (Bill of right). Sasa nilitaka kuongezea haya kuhusu mimi ni nani? Na kwanini kesi hii imeletwa.

Sasa kwa leo naomba nianze kwa kuzungumza juu ya mchango wangu kama Mwanaharakati wa Haki za binadamu na Demokrasia kwa nchi hii.

Na ushahidi huo utathibitisha kuwa kesi hii ni kwasababu hizo za msimamo wangu wa miaka mingi ni kazi niliyoifanya kwa miaka mingi sana.

Kwahiyo ni Political Persecution kwasababu ya msimamo wangu katika masuala ya haki na utawala bora. Sio kwasababu mimi ni MHAINI ni kwasababu ya kazi niliyoifanya na nitakayoendelea kuifanya.


Tundu Lissu anaendelea kutoa utetezi wake.

Nimetumia maisha yangu karibu yote ya utu uzima nikipigania Haki za wananchi. Sikuanza juzi certainly sikuanza Tarehe 03/04 mwaka jana.

Nilianza nikiwa Sekondari 1988 karibu nifukuzwe shule kwasababu ya kutetea Wanafunzi walioko form 4 na mimi niko form 6 kuna Majaji wa Mahakama ya rufani na Mahakama Kuu wanajua kwasababu nimesoma nao sitawataja.

Nikaambiwa kwanini unawatetea hawa form 4 wakati wewe ni form 6.?

Waheshimiwa Majaji mwaka 1989/1990 nikiwa jeshini, sijui kama siku hizi wanaenda Jeshini, nikiwa huko Jeshini mjadala wa vyama vingi ukaanza.

Majeshi yetu haya Polisi, Magereza, JW wote hawa walikuwa ni MA CCM, naamini hadi leo hawajakomboka kwa matendo yao wamekaaa ki CCM CCM.

Kwahiyo msimamo wa Jeshi ulikuwa ni Vyama Vingi HAPANA, na mimi nilikuwa 841 Itende, Mbeya. Niligombana sana na wakubwa wa jeshi waliokuwa wanasema hatutaki vyama vingi.

Niliwaambia akina Omary Mahita kuwa Mwalimu nyerere amesema ambao hawataki mabadiliko ni wajinga nyie hamjasikia hii kauli?? Nikiwa Service Man nilipigania nchi hii kuwa ya kidemokrasia, Mfumo wa Chama kimoja haukuwa wa kidemokrasia.

Rais Mwinyi alipoteua Tume yake kuhusu kuuliza wananchi mfumo wa Chama kimoja au wanataka vyama vingi.

Tume ya Rais ya Chama Kimoja au Vyama Vingi Tanzania, almaarufu kama Tume ya Jaji Francis Lucas Nyalali, tume hiyo ilipoundwa February 1991 mimi nilikuwa mmoja ya Watanzania kwenda kutoa ushuhuda kuhusu haja ya Tanzania kurudi kuwa nchi ya Vyama vingi kama tulivyokuwa huko nyuma tulipopata uhuru.

Prof. Haroub Othman aliongoza jopo ambalo nilienda kutoa maoni na Sekretari wa Tume alikuwa January Msofe ambae baadae alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kwahiyo nilidai mabadiliko na kwenda kutoa ushuhuda kwa tume ya Rais, Nilipigania Demokrasia kwa njia hiyo.

Na Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi niligombea na nilirudi kutoka Uingereza kwasababu nilikuwa concerned na suala hilo.

Waheshimiwa Majaji kwa miaka yote iliyofuata mpaka leo. Nimepigania Demokrasia, Katiba Mpya, Mfumo huru na wa Haki wa Uchaguzi. Sijawahi kupumnzika kufanya kazi hii ya kitume.

Nje ya kupigania Demokrasia nimepigania haki za wananchi wa kawaida miaka yangu mingi sana. Mwaka 1997 Serikali ya Rais Mkapa iligawa eneo karibu lote la Delta ya mto Rufiji kwa mwekezaji mmoja wa ki Irish ili alime Kamba (Proms) wale wadudu wa baharini lakini wanafugwa na huyu Reginald Mu Irish.

Sasa Mkapa na Serikali yake wakamgawia hector 120 za msitu wa mikoko wa Rufiji afanye hiyo Industrial farming. Hilo lingefanikiwa huo msitu usingekuwepo leo hii na ingeathiri watu laki na 20 wa bonde la mto Rufiji.

Mimi na wenzangu wa Chama cha Wanasheria wa Mazingira LEAT Dr. Nshala simuoni hapa.

Mimi na wenzangu tuliingia kutetea jambo hilo, Mkapa Mwenyewe na Waziri Wake Omary Juma, tuliitwa Majahidina wa Mazingira.

Tulifanikiwa na kuokoa msitu wa mikoko na Mu Irish akakimbia nchini hiyo ilikuwa 1997/1998.

Waheshimiwa Majaji sio Rufiji tu nimekuwa mstari wa Mbele kupigania haki za Ardhi za wafugaji na wananchi wanaoishi katika hifadhi za Ngorongoro mnakosikia wanapelekwa Handeni, Loliondo, Tarime, Meatu, Maswa Mashariki, Bariadi Mashariki. Huko kote nimefika na kupigania haki za wananchi.

Miaka 3 iliyopita 2023 nilikamatwa ili nisiende Ngorongoro nisiende kuwaona Wamaasai niliowapigania toka mwaka 1996.

Nimepigia kelele matukio mabaya kabisa ukanda wa Ziwa Tanganyika, maeneo mengine ya Nkasi na ukanda wa Pwani wa Mkoa wa Kigoma.

Maeneo ya wavuvi kutoka kule ukanda wa Ziwa Victoria kwenye mpaka na Uganda hadi mpaka na Kenya kumekuwa na ukiukwaji wa haki za wavuvi na wanauawa na vyombo vinavyoitwa vya Ulinzi kwenye Taifa hili. INATISHA.

Lissu anaendelea kutoa Utetezi.

Lakini Waheshimiwa Majaji kipekee kabisa najulikana ndani na nje ya Taifa hili na nafahamika kwa kupigania wananchi wenye madini. DHAHABU ndani ya Taifa hili.

Takribani miaka 10 kuanzia 1999 mimi ndo nilikuwa nazungumzia masuala ya madini ndani ya nchi hii na Serikali ya Mkapa namna ilikuwa inawaonea, Mgodi wa tatu kwa ukubwa afrika GGM kule Geita, maelefu ya Wananchi waliondolewa, Bulyanhulu ambako July na Agost 1996 kulitokea mauaji makubwa ya wachimbaji wadogo wadogo wakati Mkapa amewapelekea majeshi wananchi ili kuukabidhi mgodi kwa wa CANADA.

Bulyanhulu ndo ilitupa mimi na Dr. Nshala kesi yetu ya kwanza ya jinai mwaka 2002, tulifanya kampeni ya uchunguzi huru Tanzania, Marekani na maeneo yote na hatimaye tukapata kesi ya jinai.

Eneo la nusu Nzega kulikuwa na mgodi Golden Prime Mine watu maelfu walifukuzwa ili kuwa kabidhi wa Australia mgodi hu lakin mimi na wenzangu tulipambana.

Tarime - Nyamongo, Waheshimiwa Majaji Tarime ni muhimu sio kwasababu ni Ukweni tu lakini kwa miaka 3 nilitoa watu 466 kwenye Gereza la wilaya ya Tarime na Gereza la Butimba Mwanza. Walifungwa kwa makosa ya uongo tu ili wapewe wazungu wachimbe dhahabu. Miaka 3 nilitoa watu 466 akiwemo Chacha Wangwe marehemu akiwa Mbunge.

Hata Tarime nayo ilinipa kesi ya Jinai kwa serikali ya Jakaya Kikwete.

Nimepigania haki za wanachi Buhemba siku hizi inaitwa Wilaya ya Butiama nako kulikuwa na Mgodi.

Hata Mererani wilaya ya Simanjiro, Mang'onyi Ikungi Mashariki Jimboni kwangu kwenye dhahabu kumekuwa ni maafa kwa wananchi na kwa muda mrefu tumekuwa ni sauti kwa wananchi waliopelekewa hayo maaafa.

Nataka nimalizie kwa kusema hivi katika eneo hilo, ambako pamekuwa na ukandamizaji kwenye Taifa hili nimejitahidi kuwa sehemu ya mapambano ya kupinga huo ukandamizaji.

Kauli mbiu yang, My Motto imekuwa UPINZANI DHIDI YA UKANDAMIZAJI NI UTUKUFU KWA MUNGU.

Sasa Waheshimiwa Majaji Maisha ya aina hii na msimamo wa aina hii umekuwa na gharama kubwa kwanu na naomba nizungumzie hilo.

Waheshimiwa Majaji kesi hii ni kesi ya Uhaini na kama ambavyo nimesema mara nyingi mbele yenu. Uhaini kama ilivyotafsiriwa kwenye Kanuni ya Adhabu ndio kosa kubwa kuliko yote kwenye Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 28(4) ya Katiba.

This is the greatest offence of them all in the United Republic of Tanzania. Kama mkishawishika adhabu pekeee mna mamlaka ya kuitoa ni KIFO, It doesn’t get more serious than this.

Sasa waheshimiwa majaji ninachotaka kusema leo nakabiliwa na kesi kubwa kuliko zote hapa Tanzania lakini hii ni mwendelezo wa kesi nyingi za jinai ambazo nimepewa na Serikali ya nchi hii na Mapolisi na mawakili wake.

Waheshimiwa Majaji sina hakika na watu wengine nje ya Chama changu lakini naweza kusema ndani ya Chadema Mimi ndie Mwanachama na Kiongozi nimeshitakiwa mara nyingi kuliko kiongozi mwingine yeyote.

Na kesi zote ambazo nimefunguliwa na Serikali na Mawakili na Mapolisi wake ni kesi za kisiasa na zilitokana na misimamo yangu na matendo yangu ya kisiasa.

Waheshimiwa Majaji.

Tuanze na Utawala wa Rais Mkapa.

Mwaka jana wakati wa Christmas, mke wangu alinitumia ujumbe “Baba uko Gerezani Christmas unatukumbusha Christmas ya kwanza ya Maisha yetu ulikuwa Gerezani wakati wa Mkapa.”

Nimekamatwa Tarehe 23/12/2002. Siku mbili kabla ya Christma, kwa kosa la Uchochezi, wanapenda sana hilo kosa watu hawa kwasababu ya kuongoza kampeni ya kudai mauaji ya Bulyanhulu yachunguzwe.

Walikufa watu zaidi ya 60 sio vifo vya bahati mbaya, nilidai yachunguzwe sawasawa. Nikatengenezewa kesi ya Uchochezi.

Makao Makuu ya Polisi Central panaitwa Shimoni, kuna Gereza hapo chini wanajaza watu mle wengine wanakaaa miezi.

Nilikaaa shimoni siku 2 na kelele zikawa nyingi nikapelekwa mahakamani siku ya Christamas. Sijui walimpata wapi hakimu Lugulu lakini nilisomewa na nilikaaa na kesi hiyo kwa miaka 6. Hawaleti shahidi. Kila siku tunachunguza, upelelezi unaendelea.

Washitakiwa wenzangu ni Agustino Mrema, Dr. Nshala tulishtakiwa kwa kudai uchunguzi wa matukio ya mauaji. Baada ya miaka 6 Mahakama ya Kisutu for want of prosecution kwa kukosekana mashahidi. Hiyo wakati wa Mkapa.

Mkapa akaondoka 2005 akaingia Jakaya Kikwete.

July 2011 nikiwa Mbunge Polisi wakafanya mauaji eneo la Mgodi wa Nyamongo wakaua watu. Nikiwa Bungeni wananchi wa Nyamongo walinipigia simu inabidi uje. Njoo utusaidie. Nikaondoka Bungeni hadi Tarime kwenda kusimama na Wananchi. Kudai uchunguzi wa mauaji yale ufanyike.

Nilipofika Tarime Polisi wanataka kwenda kuvunja Mochwari ili waibe maiti na kwenda kuzika. Tukapiga kambi mochwari. Tukavamiwa na Polisi na kupigwa sana kuna ile picha maarufu nimechaniwa Kombati yangu. Tukaenda kuwekwa lockup baada ya kupigwa sana.

Kesho yake mimi na wengine tukashitakiwa kwa kosa la Criminal Trespass na kukaa jela ya Tarime siku 4 ambako zamani nilikuwa natoa wafungwa sasa nikawa mfungwa mwenyewe. Baada ya hapo kesi. Miezi mingi ikapita hadi hakimu wa wilaya ya Tarime kuifuta. Hawakuleta mashahidi.

Mwaka 2012 Polisi wakaua Wananchi wetu Arusha Mjini kwenye Maandamano, Sheria za nchi hii zinaruhusu Maandamano. Tumefanya Maandamano watu wakauawa. Tukaenda kushinikiza haki itendeke. Mimi, Dr. Slaa tukakamatwa na watu wengine. Tukadhalilishwa na kupelekwa mahakamani kwa kufanya mkusanyiko usio wa halali.

Hiyo kesi nayo ilikaaa bila kuletea mashahidi hadi ikafutwa.

Mwaka 2013 kulikuwa na uchaguzi ndogo za Madiwani. Maeneo tofauti nchini ikiwemo Arusha. Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mbowe mkutano wake ukashanbuliwa kwa mabomu ya kurusha kwa mkono na watu kadhaaa wakafariki.

Tukarudi tena kuandamana kudai haki itendeke. Tukakamatwa tena. Mimi, Dr. Slaaa na wengineo.

Sikuwahi kuona Mwenyekiti wangu alikuwa na mbio kali nilimuona siku hiyo. Tukashitakiwa tena na mkusanyiko usio halali.

Polisi kama kawaida yao walitupa mafile wakaendelea na shughuli zingine. Kesi ikafutwa. Kwahiyo kesi tatu za Kikwete ndio hizo.

Akaingia Magufuli na Samia sasa.

Magufuli na Samia nao mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar alishinda Maalim Seif na Jecha akafuta matokeo , huyo Jecha Salim Jecha akasema kwamba mwezi March 2016, Uchaguzi huo utarudiwa , nikaulizwa na waandishi kuwa unasemaje? Nikasema wanataka kuleta maafa.

Tarehe 29/06/2016 nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi, mtu aliyenikamata anaitwa Ramadhani Kingai alikuwa Deputy ZCO leo ndio DCI wa leo.

Walinipeleka Central Dar es salaam kabla hawajanipeleka shimoni wakanipeleka kwa ZCO Camilius Wambura ambae leo ndio IGP, Mkuu wa Jeshi la Polisi ili kwenda kujaribu kunitisha.

Nikawaambia, Wambura tutakutana Mahakamani.

Nikapelekwa Mahakamani for once walileta mashahidi na mmoja wa hao mashahidi alikuwa Ramadhani Kingai na nilimtamani sana angekuja kwenye hii kesi ila hakuja.

Nilipomfanyia tu Cross Examination huyu Ramadhani Kingai, Jamhuri hawakuwahi kuleta shahidi mwingine.

Siku tatu baadae 29/06 ilipofika tarehe 01/07 nilikamatwa tena Ikungi kwa kosa la kumuita Magufuli DIKTETA UCHWARA kwamba akabiliwe na kila mwananchi mwenye akili timamu.

Nilikamatwa siku tatu baadae. Nikasafirishwa usiku kwa usiku kuletwa Dar es salaam, nililazwa kituo cha Polisi Chamwino karibu na Ikulu kuna mbu wengi sana badae nikashitakiwa kwa uchochezi.

Around September 2016 nikakamatwa eneo la Bunge na kuletwa tena Dar es salaam.

Mwaka 2016 uliiisha nilikamatwa mara 4 na Polisi wa Magufuli na Mahakama yao huwa ni Kisutu tu, ndani ya huo mwaka nilikuwa na kesi nne.

Kesi ya nne ilikuwa around December Waheshimiwa Majaji na ikaanza mwaka 2017 na nilikamatwa Dodoma, February na kuletwa Dar es salaam.

Mwezi April 2017 kulikuwa na Uchaguzi wa TLS nikawa mgombea, Dr. Mwakyembe na Magufuli walisema hawezi kugombea, siku nne au tano kabla ya Uchaguzi nilikamatwa na kuletwa Dar es salaam.

Nikakaaa Segerea siku nne, siku moja kabla ya uchaguzi nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaaa nikapelekwa kwa Hakimu mkazi kisutu. Mh. Mwijage yule alikuwa mrefu kuliko Majaji na Mahakimu wote nchini akasema nenda kagombee Urais wa TLS Mh. Lissu, Nikaenda na kushinda.

Between April to August 2017 nilikamatwa mara mbili, April na August.

Walinikamata na kutaka kwenda kunipima mkojo, nikasema kwendeni zetu mkojo na Uchochezi vinahusiana na nini?

Sababu nilikamatwa kusema Bombadier imekamatwa huko Canada kutokana na Magufuli kuisababishia hasara nchi alipokuwa Waziri.

Niliposema hayo maneno likawa kosa kwahiyo June 2016 na Agosti 2017 nilikamatwa mara 8 na kufunguliwa kesi 6 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Baada ya hapo wakasema anatusumbua, Mahakamani hatumuwezi wakatuma watu Wanaoitwa WASIOJULIKANA kuja kuniua ilikuwa Tarehe 07/09/2017

Sasa Waheshimiwa Majaji ya mambo ya Tar. 07/09/2017 nahitaji kuyapa Contest kidogo.

Kama nilivyosema nilikuwa mnadhimu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na nilikuwa nakaa na Merdadi Kalemani ndugu yake na Magufuli, pale tulipokuwa tunaishi ni makazi ya Viongozi wa Serikali na jirani yangu mwingine alikuwa Tulia Ackson.

Anasimama Katuga anasema sio sawa hadhara inayotoa ushahidi ........

Mh. Lissu basi naomba radhi niendeleee.

Katuga ana kihehere sana na mropokaji sana.

Sasa yale Makazi yanalindwa na walinzi wenye silaha muda wote.

Siku nashambuliwa wale walinzi wote hawakuwepo na mageti yalikuwa wazi, na nilikuwa nimetoka Bungeni wale watu wanifuatilia tangu natoka Bungeni hadi nafika nyumbani.

Nikiwa kwenye Parking hapo ndo walinipiga Risasi 16, hizo risasi 16 ndizo zilizozaaa operation 25 na natembea na risasi 1 kwenye uti wa mgongo na Madaktari wamesema ni hatari kuitoa hivyo naishi nayo.

Hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa na hadi leo sijawahi kuitwa na Polisi kwenda kuhojiwa lolote kuhusu tukio hilo.

Nilikuwa mtu wa kufa.

Sasa Waheshimiwa Majaji, Mungu sio Athumani. SIKUFA.

Badala ya Mimi, Magufuli AKAFA yeye na Magufuli alipokufa zile kesi 6 zilizofunguliwa nilizosema hapa. Magufuli alipokufa miezi 6 baadae nazo zikafutwa.

Akaingia SAMIA na zile 4R zile.

Katika kutekeleza hizo 4R Tarehe 12/08/2024 nikaalikwa kama Makamu Mwenyekiti na Baraza la Vijana wa CHADEMA.

Jeshi la Polisi likapiga marufu maadhimisho hayo, tukasema haiwezekani.

Nikasafiri kwa ndege kwenda Mbeya, Tarehe 11/08 nilipowasili jioni nikaenda kwenye ofisi za Chama Mbeya mjini, nikavamiwa na kundi kubwa la askari wa Polisi wakiongozwa na AWADHI JUMA ambae ni Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi.

Mimi na Viongozi wenzangu tulipigwa sana na kukamatwa na mimi nilichukuliwa na Polisi usiku ule nikapelekwa hadi Vwawa ipo Mkoa wa Songwe, nikaenda kufungwa huko.

Kesho yake nikapakiwa kwenye gari na kusafirishwa na kurudishwa Dar es salaam. Nikaletwa Central tena alfajiri ya siku iliyofuata, nikakabidhiwa kwa askari Polisi wa Central nikawauliza kosa ni nini?

Wakaniambia tunakupeleka nyumbani kwako kwahiyo nikapelekwa Tegeta nyumbani kwangu na kuanza kugongea watu nyumbani kwangu na sikufunguliwa mashitaka yoyote.

Hiyo ni mara ya kwanza ya Samia kunikamata


Lissu anaendelea kutoa utetezi wake.

Mwezi uliofuata yani Septemba 07, 2024 Mkurugenzi Hamasa wa Chadema Makao Makuu, Mohamed Ally Kibao akiwa ndani ya Bus alitekwa maeneo ya Tegeta akashushwa kwenye Bus na watu hao ambao walikuwa na silaha za moto na magari ya Polisi yenye vioo vyeusi. Na mabanduki wanayotumia Polisi, kama sio Polisi basi ni Usalama wa Taifa.

Kesho yake Mzee Mohamed Ally Kibao aliokotwa ufukweni Ununio akiwa amemwagiwa Tindikali na akiwa amefariki.

Waheshimiwa Majaji Marehemu Mzee Kibao akiwa anatekwa na kuuwawa kulikuwa na matukio mengi ya Viongozi wa Chadema kutekwa na kupotezwa. Huo ni mwaka 2024 kama Chama tukasema tusipochukua hatua itakuwa hatari sana.

Tukaanzisha Maandamano ya kupinga mambo ya utekaji maana ni Haki kuandamana katika nchi hii katika Azimio hilo tuliazimia kuwa tutaanza Tarehe 23/09 kufanya maandamano hayo.

Nilivamiwa na Polisi asubuhi na mapema hiyo Tarehe 23/09 na kukamatwa na nikadhani napelekwa central lakini nilizungushwa huku mjini na kupelekwa Mbweni Kituo cha Polisi kwa mara ya kwanza sikupelekwa Central.

Nikakaa Mbweni Police Station hadi usiku na baadae wakanirudisha nyumbani kwangu.

😂😂😂 hawa Mapolisi kuna muda wakimkumbuka nafikiri huwa wanaenda kumchukua wanapiga nae story halafu wanamuachia, vilaza kweli😂😂😂

Anaendelea.

Around March 2023, nilikamatwa na Samia kule Karatu ili nisiende kuonana na Wananchi wa Ngorongoro nilienda kufungwa kituo cha Polisi Monduli Juu kule.

Niliwekwa Monduli na jioni wakampigia Mzee Alute wakasema njoo umchukue mdogo wako huku ili mradi tu wanivurugie ratiba zangu.

Tarehe 09/04/2025 ni mara ya nne nakamatwa na SAMIA na Mapolisi wake. This time wamenifungulia kesi ya UHAINI siku iliyofuata ya Tarehe 10/04/2025 na tayari hapa nilipo nimeshakaa gerezani miezi 16 naelekea mwezi wa 17 yani mwaka mmoja na miezi 5.

Waheshimiwa Majaji, it is the longest I have stayed in prison in my entire life na ni kipindi kirefu ambacho kiongozi wa CHADEMA amekaaa muda mrefu kuliko mwingine na naamini hakuna kiongozi wa mageuzi nchini aliyekaa kipindi kirefu zaidi ya hiki.

Na kesi hii ndio kubwa kuliko zot, hakuna kiongozi amefunguliwa kesi ya aina hii na kuwekwa Mahabusu muda mrefu kama mimi.

Sasa Waheshimiwa Majaji hayo ndio yamenitokea mimi peke yangu, naamini hakuna kiongozi yeyote wa juu wa Chadema ambae hajapitishwa kwenye bonde la uvuli wa mauti na wapo wengi ambao nimefanya nao kazi leo ni marehemu toka mwaka 2015. Wengine wamepotezwa hawajulikani walipo.

Hata Chama tumepelekwa kuzimu na kurudishwa. We have been taken to hell na tukarudishwa.

Tumefunguliwa kesi na Mapolisi na Mawakili hawa wa serikali za kila aina na za uongo.

Mhe. Lissu anainama chini na kuokota kitabu fulani kikubwa kina rangi ya blue.

Anasema, Waheshimiwa Majaji Tume ya Rais ya Kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za Haki Jinai, maarufu kama kama Tume ya Jaji Chande hii hapa, Inapopendekeza kuwa Jeshi la Polisi na taasisi zingine zifumuliwe kwasbababu zinaonea watu sana.

Sio Polisi wanaofungulia watu kesi za Bure, Sio Polisi peke yao, ni ya Polisi na hawa hapa. Anamuoneshea Kidole Katuga.

Likatuga limetuna kwenye kiti linatoa tu macho

Mhe. Lissu anaende hii miaka mitatu nimeumizwa sana na nimeumizwa sana na nimeumizwa sana.

Anasimama Katuga.....

Waheshimiwa Majaji ombi letu ni either maelekezo ya Mahakama yenu tukufu au kuikumbusha ni ushahidi in chief na hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 156(2) kinaweka wazi kuwa in chief must relate to relevant fact.

Mara ya kwanza tulikaaa kimya kwasababu shahidi anataka kuleta ushahidi wa good character sasa tunaenda astrey kwasababu watu kufa na sio vitu sahihi ambavyo vinahitajika hapa leo.

Katunga anasema Je hiyo ni good character kwake? Ni sehemu ya hii kesi? Tunaweza kukaa hata week mbili, zmeingia kesi 9 hapa, alete vitu ambavyo ni fact in issue. Mtaletewa vingi sana.

Mhe. Lissu anasimama: Waheshimiwa Majaji utetezi wangu ni kwamba hii kesi hii ni kesi ya kisiasa na imetengenezwa kwa uongo ni kesi ya kisiasa.

Kesi yangu inathibitisha kile ambacho tunakisema they abuse their power na huo ndio utetezi wangu.

Anavyosema tunaweza kutumia week mbili inanishangaza kidogo yani tumekaa mwaka mzima leo wao wanataka kusema wanapenda muda. Kama wanaona hayana relevance wana wasiwasi gani? Mimi najitetea kwenye kesi ya uhaini mniache niseme. Huu upendo wa kuokoa muda umetoka wapi?

Majaji wanateta kidogo pale juu.

Jaji Ndunguru anasema naomba tuendeleee, Tuwe guided na kilichopo.

Mhe. Lissu anasema haya namalizia lakini mvumilie tu sijaanza bado ya uchaguzi.

Bado tupo sana, tuvumiliane.

Taarifa Ndefu iliyopelekwa kwa mwendesha mashtaka mkuu

Anasimama Job Mrema, anasema kifungu cha 177 cha Evidence Act, anasema shahidi ana makaratasi anasoma na kifungu hiki. Akikaa pale kifungu hiki kina mguide nini cha kufanya.

Mhe. Lissu anajibu anasema mimi sisomi nikitaka kusoma tutakaa mwaka mzima.

Watu wanacheka 😂😂

Jaji Ndunguru : hebu tuendeleee tafadhali.

Mhe. Lissu anasema

Sasa Waheshimiwa Majaji kesi hii kiuhalisia ni mgogoro wa kisiasa unaohusu Uchaguzi nchini so hiyo ndo essence ya kesi hii.

Taarifa iliyopo Mahakamani inanituhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha watu kuitishia Serikali kwa kuvuruga uchaguzi.

Maneno ninayodaiwa kuyasema kwa kuyaangalia tu yanahusu uchaguzi, tutazuia, tukahamasisha watu kuzuia uchaguzi. Mashahidi wote 17 wa upande wa Mashitaka kila mmoja wao amesema in connection na kauli zangu kuhusiana na uchaguzi.

Ushahidi wa Nyaraka ambao ni Documentary evidence which has been tendered zote zina touch on uchaguzi.

Naomba nizungumzie Uchaguzi wa Tanzania sasa.

PW 1, PW 2, PW 3, PW na 16 na PW 17 kwa kiwango fulani walisema kauli ambayo wanadai nimeichapisha kwenye JAMBO TV Youtube ima urefu wa masaa matano.

PW 16 na PW 17 wanasema ina masaa mawili na kadhaa. Wote kwa ujumla wao wamesema picha mjongeo ni ndefu. Walicholileta Mahakamani ni maneno ukiyasoma hufiki dakika moja. Ukiyasoma hayo maelezo ninayodaiwa nilisema.

Hayo masaa matatu mengine wanayosema nilizungumza nilizungumza kitu gani?
Tujiulize.

Nitazungumza nilizungumza kitu gani kwenye hayo masaa matatu lakini ili muelewe nilisema nini lazima muelewe matatizo ya Uchaguzi wa nchi hii?

Bila kufahamu context hamtaelewa maneno yangu yana maana gani? Sasa mtaielewa Tarehe 03/04/2025 ilikuwa na maana gani?

Tunafanya General Election katika nchi hii tangu mwaka 1957. Uchaguzi wa kura tatu. Uchaguzi wa pili August, 01, 1960 ndio ulizaa Serikali ya Madaraka na baadae mwaka mmoja tukapata Serikali ya uhuru.

Kuanzia Mwaka 1960 hadi leo, tumefanya chaguzi kila baada ya miaka 5 bila kukosa. We have conducted general election every 5 years consecutivelly kabla ya mwaka 1965 kati ya 1965 na 1995 kabla hiyo.

Kuna picha ya Nyerere peke yake na box lingine giza,!unaambiwa chagua mtu unayempenda.

Mwaka 1992 Uchaguzi Mkuu uliofuata ulikuwa uchaguzi wa vyama vingi hakukuwa na giza na picha ya mtu. Vyama vingi vikaanza. Wakati tunaingia mfumo wa vyama vingi Rais Mwinyi aliunda Tume ya Nyalali.

Je ilipendekeza nini juu ya mfumo wa Uchaguzi?

Tume hii iliweka ratiba na kupendekeza inapofika mwezi Sept. 1993 wakati huo ilikuwa 17/02/1992 kwamba tuwe na Katiba Mpya na kwenye Katiba Mpya tuwe na tume huru ya Uchaguzi, yalisemwa hayo kwenye ripoti ya nyalali na ikasema katiba yetu ya sasa ni Katiba ya Chama kimoja haifai kwenye vyama vingi.

Tume ya Uchaguzi ni tume ya CCM na haifai kwenye mfumo wa Demokrasia wa Vyama Vingi.

Lissu anaendelea kutoa Utetezi wake

Anasema Tume ya Nyalali ilisema pia kuwe na Wagombea Binafsi, Independent Candidate.

Serikali ya Mwinyi na Chama Chao walikataaa mapendekezo ya Jaji Nyalali, walikataaa Katiba Mpya na Tume Huru na Wagombea Binafsi, vyote walikataaaa.

Marehemu Mzee Mwinyi aliandika kitabu kabla hajafariki, alisema tulikataaa mapendekezo ya Jaji Nyalali ili kuokoa CHAMA na Watu wa CCM wangekimbia CHAMA.

Na akasema hiyo habari ilileta ugomvi mkubwa na Mwalimu Nyerere kwahiyo hatukupata Katiba Mpya na Tume Huru na Mgombea Binafsi.

Kwenye kilichotokea kwenye sheria ya mabadiliko ya Katiba 1992 yakaifanya Tume ya Uchaguzi kuwa ya CCM zaidi na kuwafanya wajumbe wote wa Tume kuwa wateule wa Rais moja kwa moja kabla ya hapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alikuwa ni Spika wa Bunge.

Wao wakamfanya Mwenyekiti awe ni Jaji ambae ni mteule wa Rais yale mabadiliko yakamfanya Mkurugenzi wa uchaguzi pia kuwa mteule wa Rais.

Na Marais wote miaka yote huwa ni Mwenyekiti wa CCM na mara zote anateua tume ya Uchaguzi iliyokaaaa ki CCM CCM.

Sheria ya Uchaguzi 1985 iliyofutwa na hii ya juzi ya 2024 iliwafanya Wakurugenzi wa Halmashauri, kuwa ni wasimamizi majimboni hawa wote ni waajiriwa wa Rais. Na hao Wakurugenzi wanateua watu wa chini kusimamia uchaguzi huko chini hivyo mfumo wote wa Uchaguzi ni wa CCM.

Haya ninayosema mfumo mzima wa Uchaguzi ukawa ni mfumo wa ki CCM ni maneno yaliyopo kwenye tume ya Jaji Warioba, ilifanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya Kikatiba.

From Top - bottom ni Tume ya Rais ndo maana aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzu Wilson Mahera kwasasa ni Mbunge wa CCM jimbo la Butiama.

Tume ya Uchaguzi ilikuwa na Makao Makuu yake hapa Dar es salaam kwenye uchaguzi mkuu 1995 vifaa vya uchaguzi havikupelekwa vituoni. Walimuogopa Mrema ili kuvuruga uchaguzi wa Dar es salaaam na Zanzibar.

Mauaji yalianzia Zanzibar na sasa yamevaaa kila eneo na mimi nimefanya utafiti miaka kadhaaa. Na watazamaji au waangalizi wa Uchaguzi wamesema sana kuanzia 1995 kuwa yafanyike mabadiliko ya Kikatiba ili kuifanya Tume ya Uchaguzi iwe huru.
Haya mambo ya kuipendelea CCM yana potential ya kuleta uvunjifu wa Amani lakini Serikali ya Mkapa na CCM ilikataaa.

Mwaka 1998 Tume ya Jaji Kisanga ikapendekeza tuwe na mfumo bora zaidi wa Uchaguzi nchini na Mkapa na Serikali yake wakakataaaa. Mwisho wake maafa yakatokea Pemba watu waliuwawa, Tukapata wakimbizi Tanzania wengine wakakimbilia Mombasa sababu Mkapa alikata Tume huru ya Uchaguzi Nakumbuka Katiba Mpya.

Zanzibar ilikuja Tume ya Kimataifa na baadae Tume ya Jaji Mac Bomani nayo ilipendekeza Katiba Mpya na mabadiliko ya mfumo wa Katiba Mpya. Hiyo ni mwaka 2003 walimkatalia.

Jaji Mac Bomani aliwekwa kwenye Tume ya Uchaguzi na mwaka 2005 akataka kugombea Urais kupitia CCM.

Hivyo matatizo yakaendelea kuwa makubwa siku hadi siku. Waangalizi wa kimataifa wakapendekeza tena mwaka 2000 na 2005 kuwa nchi hii inapaswa kuwa na mabadiliko ya mfumo wa Uchaguzi.

Ameondoka Mkapa amekuja Kikwete.

Tukaenda Uchaguzi wa 2010 na Tume hii hii na uchaguzi huu huu, yakatokea maafa tena Zanzibar na alipoingia tena akasema lazima tuwe na KatibaMpya tumalize hii habari ya katiba.

Tukapambane kuwezesha tume ya mabadiliko ya Katiba, wale wajumbe wote tulipendekeza na tukalazimisha tupate Tume yenye balance.

Katika historia yetu yote hatujawahi kuwa na tume aina ya Warioba ndo maana hawampendi yule Mzee.

Tukaenda na mjadala 2014 tunaelekea mwishoni CCM wakavuruga swali la kura ya maoni lilishatengenezwa tukaenda uchaguzi mkuu 2015 na Tume hii hii na Katiba hii hii tukampata Magufuli na Samia.

Lissu anaendelea kutoa utetezi

Anasema baada ya Magufuli na Samia kuingia 2015 Kazi waliyoifanya ndo imetuleta leo hapa mpaka nimepewa kesi ya Uhaini.

Sikusema Ijumaa kuwa 2020 nilirudi kutoka uhamishoni kutoka Ubelgiji kuja kumkabili Magufuli ni wazi sikuchaguliwa lakini ningechaguliwa, nisingekuwa hapa.

Baada ya matokeo ya Uchaguzi Tume itapaswa kuchapisha matokeo ya jimbo kwa jimbo.

Ukiangalia chaguzi za kabla ya mwaka 2020 Tume huwa zina gazette matokeo yote jimbo kwa jimbo na Kata kwa kata nchi nzima.

Ya Ubunge Jimbo kwa Jimbo nchi nzima lakini ya Urais huwezi kuona kokote kule.

The results were never gazetted na sheria inasema baada ya miezi 6 yatachomwa moto. Hatutakuja kujua Magufuli alipata kura ngapi? Kwanini? kwasababu Tume ni ya KiCCM.

Toka mwaka 1995 wagombea wa upinzani wameenguliwa kila mwaka.

Toka mwaka 1995 na uchaguzi wa 2020 ndo ulitia fora, Wabunge wa majimbo 28 walipita bila kupingwa, aliyeengua ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambae kwa sasa ni mbunge wa CCM.

2020 kwenye General Election ilikuwa ni mass disqualification walioenguliwa ubunge walikuwa 63 kati ya 244 tukapambana nao sana.

Madiwani 832 walienguliwa na kwa mara nyingine kukawa na mauaji sana.

Sasa Waheshimiwa Majaji ukisoma taarifa za watazamaji wa kimataifa walisema uchaguzi sio wa huru na haki na CCM inapendelewa. Uchaguzi ulikuwa na fujo na sisi huwa tunapigwa na Mapolisi na sio wanaCCM, watu wetu wanatekwa na Mapolisi sio wanaCCM.

Kwenye hotuba yangu ninaposema polisi wanatembea na vibegi mgomboni vimejaa kura. That is the truth of our heart, hakuna uongo.

Samia anasema tuliwapiga fix tukawaengua. Samia anasema hivyo kwenye ripoti.

Watazamaji wakasema bila mabadiliko ya Uchaguzi kutakuwa na maafa mwaka 2025. Ripoti ya watazamaji wa Umoja wa Afrika kuwa kuna haja ya kuwa na mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi.

CCM walisema Katiba haitaleta Chakula nyumbani sisi tukasema hapana tutapigania Katiba Mpya, wakamkamata Mbowe na kukaa jela miezi 8 kwa kesi ya uwongo ya Ugaidi na waendesha mashitaka ni hawa hawa.

Waliposema ajiteteee waka enter nolle hakujitetea tukashtukia yuko Ikulu. Nasikia jana AMEIBUKIA BWAWA LA MWALIMU NYERERE, MWENYEKITI WAKE YUKO JELA YEYE ANAIBUKIA HUKO YUKO NA MAMA.

Watu wanacheka kwa maumivu huku ndani.

Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye anasema Muda umeisha twende Mapumnziko tafadhali. Twende lisaa limoja.

Jaji sasa tukirudi utamaliza.

Mhe. Lissu hapana nafikiri tutaenda enda vizuri niachieni tu niende.

Kesi inaahirishwa baada ya lisaa tutarudi.

Kesi inaendelea

Majaji wameingia na Mwenyekiti Lissu pia ameingia.

Kelele za Rais, Rais, Rais ni nyingi sana.

Inapigwa Courttttttt

Majaji wanaingia na watu wananyamaza.

Waandishi wanashusha chini Camera zao.

Mwenyekiti Lissu anahamia upande wa pili wa kizimba.

Hapa Mahakamani vipo vizimba vya wazi viwili, kile ambacho hukaa watuhumiwa na kile cha mashahidi.

Kulia kwa Majaji ni kizimba cha watuhumiwa na kushoto kwao ni Mashahidi.

Mwenyekiti Lissu yuko Kushoto kwa Majaji.

Anasimama Ajuaye Zengeli na kusema wako tayari kuendelea upande wa Serikali. Mh. Lissu nae amesimama kwa sasa.

Masuala ya Uchaguzi na masuala ya uendeshaji wa Uchaguzi yasipowekwa sawasawa huwa yanaleta maafa kwa taifa.

Leo mtu yeyote anayesema hivyo hawezi kuonekana kicha kabla ya October 2025 ulikuwa ukisema hivyo unaonekana kichaaa.

Sisi ni Jamhuri ya Muungano wengi wetu kwasababu hatufundishwi historia sawasawa hatuelewi imekujaje.

Tunafikiria Nyerere na Karume walikaaa wakasema tuunganishe nchi, tumekuwa Jamhuri ya Muungano kwasababu Zanzibar walifanya mapinduzi ya umwagaji wa damu kwasababu ya uchaguzi.

Ripoti ya tume ya Nyalali ndio ushahidi wangu, 17 Feb. 1992 Tume ya Nyalali ilisema baada ya wazanzibar kuchoka wakachukua silaha na kupindua serikali.

Tume ya Nyalali iliyotupendekezea Vyama vingi vya siasa ndo ilisema hivyo.

Tangu mwaka 1992 tulikataaa kuona huo ukweli, tokea mwaka jana kama haijatufungua macho then tuna tatizo.

Tume ya Othman Chande imesema ya mwaka jana yanatokana na matatizo ya muda mrefu ikiwemo Matatizo ya Demokrasia, Uonevu wa Vyama Vya siasa, matatizo ya Uchaguzi.

Tulifanya kila jitihada kuepusha Oktoba 2025 ili kuepeusha maafa, tukaonekana vichaaaa.

Sasa Uchaguzi ni masuala nyeti sio ya kuchezea, ukichezea matokeo yake ni haya. Mfumo wetu wa uchaguzi matatizo yake ni ya miaka mingi sana na yameandikwa kila mahali kwenye Ripoti za Uchaguzi na waangalizi mbalimbali.

Walisema tusipoangalia tutaenda kubaya. Sisi wa CHADEMA sasa baada ya Magufuli kufariki na SAMIA kuingia madarakani nilikuwa uhamishoni.

Nilikoswa koswa koswa mwaka 2020, nikakimbilia Ubalozi wa Germa badae nikakimbia nchini.

17/02/2022 Rais Samia alifanya ziara Ulaya na kulikuwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kiafrika na Zile za ULAYA. AU EU SUMMIT akaja Ubelgiji.

Akanitumia ujumbe kupitia watu wake.

Watu wanasema niliomba hapana sikuomba, aliniomba yeye wakati huo Mwenyekiti Mbowe yuko Gerezani.

Nilivyopata ujumbe nikashauriana na Viongozi wenzangu.


Nikaenda, tukaonana alisema kimsingi anataka amalize haya matatizo yaliyotokana na utawala wa mtangulizi wake. Nikamwambia anza kwanza kumuachia Mbowe. Pili, Tuzungumze Katiba Mpya na Mfumo huru wa Uchaguzi.

Akasema niko tayari na pia nikamwambia tumekimbia nchi kwa kuogopa kifo sasa utangaze tutakuwa salama.

Akatangaza Hamad Masauni sio yeye, akiwa Bungeni.

Na baadae akamuachia Mh. Mbowe na tukapata faraja ya kurudi nyumbani.

Tulirudi tukamwambia tunataka wafungwa wetu wote waachiwe na kuachiwa.

Tukaanza mazungumzo yanaitwa Maridhiano. Tukaanza na Kinana anawakilisha CCM na Mbowe anawakilisha CHADEMA.

Tulipendekeza marekebisho ya Katiba na kubadilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mapendekezo ya maandishi na ratiba ya mabadiliko.

Na kwa ratiba yetu tungepata Katiba Mpya mwaka 2024 mwaka mmoja kabla ya mwaka wa Uchaguzi.

Tukashangaaa hakuna hatua inayofanyika, tunapeleka maandishi lakini wao wanajibu kwa mdomo, hawataki kuandika.

Tukiwa kwenye hicho kinachoitwa Maridhiano, Tumevutana kwa takribani mwaka mzima.

Tunazungumza kuhusu kujibiwa mapendekezo yetu kwa maandishi lakin waowanataka kuona tumepiga picha.

Kwakweli Picha wanazipenda sana,

Nimerudi Tar. 27/01/2023 baada ya kukaa na vikao na Viongozi wenzangu nikasema waandike barua kwenda kwa Serikali ili tujue katika mapendekezo yetu tuliyotoa kwenye Vikao vya Maridhiano Wanakubali kipi au hawakubali kipi ili tuweze kusonga mbele?

Tarehe 31/05/2023 walitujibu kwa maandishi kwamba wamekataaa mapendekezo yetu yote.

Tukakaaa kwenye vikao tukakubaliana maridhiano ni kitu gani sasa zaidi ya kunywa chai huko???

Hiyo habari ya maridhiano ife baada ya hapo tukazungumza kama chama tukasema kampeni ya Katiba Mpya na Tume huru iwe ya watanzania turudi kwa wananchi.
Wapiganie Mabadiliko.

Tulizunguka nchi nzima kuhamasisha Watanzani, watu wetu wakaanza kutekwa nyara na kupotezwa.

Tukaenda November 2024 tulijadiliana sana katika Chama. Twende au tusiende kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa . Tukasema twende.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa unasimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Basically unasimamiwa na Rais Mwenyewe. Waziri wa TAMISEMI ni Rais mwenyewe maana ipo ndani ya Ofisi ya Rais. Hiyo ni kwa mujibu wa sheria.

Aliyetunga sheria za Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ni Mchengerwa, Mkwe wa Rais Samia, Wanaosimamia kila kitu ni Wakurugenzi na watu wao wa chini.
Kwenye uchaguzi ule wa 28 November, wagombea wa upinzani walienguliwa na leo hii asilimia zote Viongozi wa Vijiji na Mitaa ni maCCM.

Mahali ambapo watu walibisha bisha walikutana na risasi za Mapolisi sasa kama unaua Mwenyekiti wa Kitongoji asigombeee kwenye uchaguzi Mkuu utafanya nini?

Ilibidi ilipiwe kafara ya damu ya watanzania. Ilipofika Tarehe 03 December 2024 Kamati Kuu ya Chadema ilikaa na yakazaliwa maneno NO REFORMS, NO ELECTION.

Tumechoka kuzika Watanzania ili CCM iendeleee kutawala kila rafiki atusikilize na kila anayetuona adui yetu atusikilize pia. Huo msimamo tuliutangaza Hadharani.

Hiyo sio kauli mbiu ya TUNDU LISSU.

Ni kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe na tulikubaliana hivyo msimamo huo ulikuwa ni 10/12/2024 ndio ulitangazwa hadharani.

Tukajiuliza utekelezaji utakuwaje?

Tukasema tunatekelezaje tumalize uchaguzi wa Chama kwanza tupate uongozi na tupeleke huu mpango kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu upate baraka halafu tuutengenezeee mkakati.

Tarehe 20/01/2025 tulifanya kikao cha Baraza Kuu la Chama ni equivalent ya NEC ya CCM.

Na Kamati Kuu ya Chama ni equivalent ya Kamati Kuu ya CCM.

Baraza Kuu hutengeneza agenda za Mkutano Mkuu wa Chama kwahiyo kwenye kikao cha Tarehe 20/01 Kamati ikapeleka mapendekezo juu ya NO REFORMS: NO ELECTION na ikipita huko inakuwa agenda ya Chama.

Tarehe 21/01 kwenye Mkutano Mkuu yalifanyika mambo mawili ikiwemo NO REFORMS, NO ELECTION na Mwenyekiti wake alikuwa ni Mbowe.

Na jambo la pili ni kufanya uchaguzi wa Chama ambao haujawahi kufanywa kokote na mimi nikatangazwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Chama.

Tayari No reforms, No Election imeshakuwa msimamo wa Chama.

Kwa Katiba ya Chama chetu, Mwenyekiti ndio anayeteua Katibu Mkuu wa Chama, Manaibu Katibu wawili na Amani Golugwa kuwa Naibu Bara na Ali Ibrahim.

Hoja ya msingi ni kwamba baada ya hapo tukaanza kazi ya utekelezaji wa mkakati wa No reforms, No Election tukaitisha kikao cha Kamati Kuu Bagamoyo kutekeleza huo mkakati.

Tukapitisha mkakati wa Kamati Kuu Bagamoyo kuwa tunaenda kuhamasisha nchi nzima maandamano ya kususia na Uchaguzi.

Tutahamasisha wananchi watumie mamlaka yao kuleta mabadiliko, tulisema kwa njia za amani.

Hatukusema tutaenda kupiga mtu yeyote. hatukusema tutaenda kuchoma gari ya mtu yeyote.

Tulisema tutatembea nchi nzima kwenda kuwaambia habari hizi na wachukue hatua kuleta mabadiliko.

Nabii Lissu katika ubora wake!
Huyu hata wakimuua atakuwa ameshatimiza wajibu wake kwa Tanganyika!
 
Aliyekuwa mgombea wetu wa Jimbo la Mrimba, anaitwa Suzan Kiwanga wa Mrimba, anarudisha fomu, akakuta Mkurugenzi kafunga ofisi, hayupo.

Ilipofika saa 11, Mkurugenzi kajitokeza, kasema, “Umechelewa, Mama,” na mgombea wa CCM kapita bila kupingwa.
 
Lissu anaivua Ngozi ya Kondoo Tanzania. Kidogo Kidogo Ufisi wetu wa Uchu wa Madaraka unaonekana!!.

images.jpg
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 24

Waheshimiwa Majaji, nikizungumza na watia nia katika uchaguzi, kuna kitu kinaitwa maadili ya uchaguzi.

Kama vile ni kweli wanapenda maadili, wanatumia maneno matamu matamu kama kweli wanapenda maadili.

Wanaopigwa faini, wanazuiwa kampeni ni wapinzani.

Na ni wapinzani wa ukweli, maana kuna wapinzani wengine ni majina majina tu.

Ukiwa CHADEMA, “anhaaa, utakiona.”

Nikazungumza na watia nia kuwa hayo maadili, kwa sababu ya kutuchapia wakati wa kampeni, na hatukusaini.

Matokeo yake Tume hii ikatangaza kwamba kwa sababu hatujasaini maadili, eti CHADEMA imefungiwa miaka 5 kugombea. Kwa sheria gani?

Nikazungumza na watia nia kuhusu vyombo vya dola wakati wa uchaguzi, wote wanakuwa CCM.

Wakati wa uchaguzi ule, TEMCO ilishapigwa marufuku na Magufuli, waangalizi wa ndani walikuwa REDET.

REDET imekaa ki-CCM, lakini waliandika ukweli kuhusu vyombo vya habari kupendelea CHADEMA.

BBC walilipishwa milioni 10 na TCRA kwa kosa la kufanya mahojiano na mimi wakati wa kampeni.

Hawa Jambo TV ambao wanasema nimechapisha habari yao wamefungiwa mara nyingi sana kwa kufanya mahojiano.

Tun需要 sheria ya vyombo vya habari inayosema FAIR ELECTORAL COVERAGE.

Sheria inayosema pawe na usawa katika coverage ya vyombo vya habari.

Nilizungumza na watia nia namna ya kurekebisha utaratibu wa coverage ya kampeni, pawe na fairness ya kusikika.

Nikizungumza na watia nia masuala yanayohusu siku ya uchaguzi.

Hilo somo nimezungumza everywhere.

Kuhusu swala la Jumapili ya uchaguzi na matatizo yake. Wakati ule uchaguzi tulikuwa tunafanya siku ya Jumapili.

Ukiwa mshamba mshamba, unashinda na wanamtangaza mtu wa CCM.

Ukifanya vurugu, unakutana na FFU na baadaye utakutana na hawa Mawakili wa Serikali.

Mimi nilimaliza uchaguzi kwangu, nikatangazwa baada ya siku 4.

Wakati huo palikuwa na polisi anaitwa Wankyo.

Baada ya kumwambia Mkurugenzi, “Naondoa polisi,” ndipo Mkurugenzi akanitangaza mshindi.

Hayo ndiyo matatizo ya wagombea ubunge na udiwani nchini Tanzania.

Na nilizungumza nao matatizo baada ya uchaguzi.

Kwa sababu mimi ni mtaalamu wa migogoro baada ya uchaguzi.

Nikawaambia, Mahakamani hapawezekani.

Wataharibu uchaguzi nchi nzima, ila hutakaa kuona majimbo 5 uchaguzi umerudiwa.

The law is impossible. Utaratibu wa Mahakama ni mgumu sana.

Kuna ripoti ya Judiciary ambayo inasema utaratibu ni mgumu sana katika Mahakama zetu kutengua matokeo ya uchaguzi.

Niliwapitisha kote huko kuwa tunahitaji mabadiliko katika Election Petition.

Election Petition ni kesi za madai, lakini proof ni beyond reasonable doubt.

Nchi za kidemokrasia zilishaondoa hiyo beyond reasonable doubt kwa sababu uchaguzi unavurugwa kitaifa kwa majimbo 265.

Mahakama zipo wapi za kusikiliza kesi 265 za uchaguzi na Majaji wapo wapi?

Kwa majimbo yote hayo 265?

Nilawaambia hii ndiyo reform tunayodai na kuhamasisha Watanzania wadai kwa ku-boycott if needs be.

Na nilisema kingine very controversial kwamba sisi tunadai mabadiliko, kwa miezi hii michache hatuwezi kupata vyote hivi.

Nilisema kwamba tupo tayari kusubiri kwa kuahirisha uchaguzi usifanyike mwaka huu, tufanye mwakani ili tupate mabadiliko ya maana.

Ndani ya chama wakaniuliza, “Tuwaache waendelee kuwa madarakani?”

Nikawajibu, “Ndiyo, kama tunataka kupata mabadiliko ya maana.”

Badala yake wakanijibu kina Wasira, “Haiwezekani, uchaguzi upo Kikatiba.”
(Huku Lissu akimuigizia sauti yake Wasira.)

MAHAKAMA KICHEKO.

Tungeweza kuepusha vifo vya watu wetu wengi sana. Jaji Chande anasema watu 500, lakini nani ajuaye kwamba kuna maelfu wengine wamekufa?

Tungeweza kuahirisha uchaguzi na watu wetu wasingekufa.

Wanasema ulisema tutakinukisha, ulisema utahamasisha uasi.

Inabidi usikie maneno yote haya, siyo maneno ya kunyofolewa.

“Oooh, unatishia Serikali.” Hakuna katika maneno neno “Serikali” na hawajaleta pia katika hati yao ya mashitaka.

Wanasema lengo lilikuwa ni kutishia Serikali. Neno wamelitoa wapi na walizungumza na nani akawaambia ni Serikali?

Hiyo inayoitwa nia ya kutishia Serikali haikuwa ya kutishia Serikali, bali ilikuwa ni kuwaelezea watia nia wa chama changu matatizo ya uchaguzi ili waweze kuelewa na kuunga mkono msimamo wa chama wa No Reforms, No Election.

Sikuzungumza kuhusu Serikali, bali kuvuruga uchaguzi.

Na mimi ni mwanasheria, nimezungumza kuvuruga uchaguzi kwa sababu hakuna kosa la kuvuruga uchaguzi.

Nimezungumza kukinukisha kwa sababu siyo kosa kisheria.

Wangetaka, wangeniuliza ulikuwa na maana gani. Mimi ni mtaalamu wa masuala ya uchaguzi.

Dhumuni lilikuwa ni kuwaelewesha Watanzania nchi nzima.

Na tulipeleka kila sehemu, hadi Kenya kwa Raila, Shura ya Maimamu, kwa Jaji Warioba.

Haikuwa siri.

Waheshimiwa Majaji, mimi siongozi chama cha conspirators, naongoza chama cha wapigania haki.

Waheshimiwa Majaji, sidhani kama nina muda.

Tutakapokutana kesho kutwa, nataka kuwapitisha kwenye ushahidi ulioletwa.

Nataka niwaonyeshe kama huo ushahidi ukiletwa, kama unatosha kunyonga mtu.

Waheshimiwa Majaji, naomba niishie hapa. Napendekeza tuahirishe hadi Jumatano.

Nashukuru, Waheshimiwa Majaji, kwa kunisikiliza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA MWISHO


Jaji Ndunguru: Hatujasikiliza upande wa Serikali kama wanataka tuendelee.

Lissu: Ni sawa, ila mimi kwa leo nimekata pumzi. Tuahirishe hadi kesho kutwa.

Wakili wa Serikali: Kwa sababu anasema mwenyewe amekata pumzi, basi tuahirishe tu.

Majaji wanateta.

Jaji Ndunguru: Kesho tumia kuongea na shahidi wako wa kwanza ili kesho kutwa umalize.

Tuendelee na DW2.

Jaji Ndunguru: Natumaini utamaliza ndani ya saa 1 ushahidi wako.

Lissu: Siwezi kuahidi saa 1.

Jaji Ndunguru: Masaa 2 je?

Lissu: Labda masaa 3.

Jaji Ndunguru: Basi naahirisha kesi hadi kesho kutwa.

Afande: HIGH COURT!

Magereza wanamfuata Lissu kizimbani.

Majaji wanatoka.

Asanteni Tukutane jumatano
 
Back
Top Bottom