Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

kisheria huwa ina ruhusiwa ili ku mdivert mtu na kupima msimamo wa anachosema ila kwenye ilo lililo mkuta sijui ngoja tuone kitakacho zaliwa mbeleni man jamaa huwa anajua kuyajengea hoja mambo serious sana

..hairuhusiwi.

..mahakama si mahali pa kufanya michezo michafu michafu ili kupata ukweli wa ushahidi.

..mawakili hawapaswi kum-provoke, wala kumtisha, mshitakiwa au shahidi.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Lissu: “Nakielewa kwamba taarifa za kufanyika kwa kosa la jinai inaweza kutolewa kwa mdomo au kwa maandishi kwa afisa wa eneo husika wa mamlaka.”

Job Mrema: “Katika eneo husika unalolalamikia, ulipeleka malalamiko?”

Lissu: “Sikupeleka kwa sababu nilikuwa nusu mfu, kwa sababu nilipelekwa Nairobi nikiwa sijitambui. Kwa hiyo, sikuwepo; nilikuwa Nairobi napigania uhai wangu.”

“Niliporudi, nikaenda kwa RPC Moroto kwamba nimerudi, nichukueni maelezo, wakakataa. Nikawaambia nipeni gari langu, nikachukua gari, lakini hawakuchukua maelezo.”

Job Mrema: “Kwenye maelezo yako umeieleza Mahakama kwamba kwa sababu umekuwa mwanaharakati kwa muda fulani, ukataja baadhi ya Polisi kwamba ukasema kuna sehemu wakasema, ‘maliza huyu.’”

Lissu: “Utakuwa umesikia vibaya.”

Job Mrema: “Wewe ni mwanasheria, unajua kwamba ukiwa na malalamiko unatakiwa kutoa taarifa Polisi?”

Lissu: “Unatoa taarifa Polisi kama Polisi siyo wahusika wenyewe. Nimesema nimekuwa nikikamatwa, kufanyiwa vitisho na Polisi wenyewe.”

Job Mrema: “Moja ya statement ulitoa ya Majaji ni CCM na Mahakamani hakuendeki, yalikuwa yanakiuka kifungu cha 51(1).”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, sikubaliani na yeye.”

Job Mrema: “Utakubaliana na mimi kwamba Mahakama ikishatoa maamuzi yake, inatakiwa kufuatwa?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba Mahakama Kuu ilishawahi kutoa amri ya ulinzi wa mashahidi?”

Lissu: “Ndiyo.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba shauri lililoamriwa na kutoa ulinzi wa mashahidi ni tofauti na shauri hili lililopo mbele sasa hivi?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba kupitia uamuzi huo wa ulinzi wa mashahidi, haijawahi kufanyiwa uamuzi wa kuondolewa?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Kama hukufurahishwa na uamuzi huo, si ungeweza kuchukua hatua?”

Lissu: “Nikichukua hatua ndiyo maana nikaja kuwaambia Majaji hapa kwamba kinachofanyika hapa ni tofauti na amri ya Jaji Mtemwa.”

Job Mrema: “Sijauliza utekelezaji wa amri.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Hapa Lissu kamtoa Knock out. Kwamba alipeka Malalamiko kwa RPC akagoma kichukuwa maelezo. Pia amejibu kuhusu mashahidi wa kificho kwamba kilichofanyika ni tofauti na mahakama.
 
Ndugai alimuondoa lissu bungeni eti kwa sababu ya utolo kipindi wote wanajua kuwa anaumwa wakti hule and at the same time walijadili bungeni kuhusu kupigwa risasi kwa lissu, nchi imepitiq ujinga mwingi hii.
Leo yuko wapi mr Ndugai spika mbabe kana kwamba alikuwa na hati milki ya uzima, tujifunze kutokana na makosa ya waliotangulia
 
TAL anautulivu sana kichwani na wamegundua kwenye mambo ya sheria hawamuwezi kwa hiyo wanachotumia ni kumpanikisha alopoke jambo lolote lile ambalo baadae watalitumia kwa wale mashahidi wengine tena Mimi Nina hofu na Heche watamuuliza maswali ya kumpa hasira nae aropoke waunganishe dot watumie kwenye uhaini sasa.....awe sana makini mwenyekiti wenu
Asee kwa mimi hapo ningeshawatukania wazazi!🤔
 
TAL anautulivu sana kichwani na wamegundua kwenye mambo ya sheria hawamuwezi kwa hiyo wanachotumia ni kumpanikisha alopoke jambo lolote lile ambalo baadae watalitumia kwa wale mashahidi wengine tena Mimi Nina hofu na Heche watamuuliza maswali ya kumpa hasira nae aropoke waunganishe dot watumie kwenye uhaini sasa.....awe sana makini mwenyekiti wenu
Nimeona pamoja na jamaa kumprovoke ila amemjibu vizuri. Ingawa maswali ni nje na kesi iliopo.
 
Nadhani anaweza kufanya hivyo. Sema ameamua kwenda nao hivyo hivyo

Hofu yangu ni kwamba unapouliza maswali; akili inaweza kujikita katika maswali na akajikuta amelijibu. Kuna swali moja Kaulizwa alilikubali na akataka kuweka "ila", muuliza swali huyo wa kwanza (Wakili) akamwambia "umeshajibu". Ni wazi TL, alijua swali lile au linahitaji ufafanuzi, au amelijibu ndivho sivyo.
Naona atakuja lisawazisha, alikusudia nini. Likibaki vile vile ni maksi kwa mashitaka.
 
Huyu Lissu utafikiri yeye ndiyo anamfanyia dodoso huyo Katuga! Mpaka anafikia hatua ya kumuita mjinga, na Katuga mwenyewe anaridhika.

Maswali mengi ni ya kipuuzi tu! Eti shuleni ulifundishwa multiple choice!! Jamaa anasema yeye alifundishwa critical thinking 😆

Mnajipa Moyo japo ukweli mnamashaka na jinsi Lissu kabanwa vibaya 👈
 
Hofu yangu ni kwamba unapouliza maswali; akili inaweza kujikita katika maswali na akajikuta amelijibu. Kuna swali moja Kaulizwa alilikubali na akataka kuweka "ila", muuliza swali huyo wa kwanza (Wakili) akamwambia "umeshajibu". Ni wazi TL, alijua swali lile au linahitaji ufafanuzi, au amelijibu ndivho sivyo.
Naona atakuja lisawazisha, alikusudia nini. Lilibaki vile vile ni maksi kwa mashitaka.
Kweli ni janja za mawakili tu.
 
Back
Top Bottom