Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Hao majaji wamepangwa, hii kesi mwisho wake ni kukosekana kwa ushahidi kumtia hatiani TL. Lengo ni kumtesa tuu.
Hii ndio itakuwa hukumu ya hovyo ya mashitaka ya uhaini, kusikilizwa na majaji wa hovyo, na kuamuliwa kihivyo hovyo. Rekodi zitabaki zitakuwa za hovyo.
Sijui kwa nini, lakini binafsi naamini safari hii hawa Majaji hawatakubali kutumiwa na hawa watu waovu.

Najiweka mstari wa mbele kusutwa ikiwa matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yangu.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Job Mrema: “Nauliza kwamba hukuchukua hatua juu ya amri ya Mahakama yenyewe?”

Lissu: “Sikuchukua hatua kwa sababu nipo gerezani.”

Job Mrema: “Mashahidi ambao wamepata ulinzi unawakumbuka?”

Lissu: “Nawakumbuka majina bandia, lakini siwajui sura zao. Majaji hawawajui. Nakumbuka herufi P na sijui nini.”

Job Mrema: “Wewe kama mwanasheria...”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, mimi ni shahidi wa facts. Akihitaji kuzungumza na mwanasheria, aandae mkutano pembeni.”

Job Mrema: “Katika ushahidi wako, moja ya hoja ulieleza Mahakama hii kwamba tarehe 12 Agosti 2024 ulipata kipigo mahali.”

Lissu: “Mahali gani?”

Job Mrema: “Ulisema Mbeya.”

Lissu: “Nilisema tarehe 11.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba katika ushahidi wako hakuna kitu chochote ulichotoa kama kithibitisho kwamba ulikula kipigo?”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, kwa mdomo, ila kwa karatasi hapana.”

Job Mrema: “Kuna hoja nyingine kwamba tarehe 23 Septemba 2024 ulivamiwa na Polisi, na huutoa uthibitisho chochote?”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, nilieleza kwamba tarehe 23 Septemba 2024 nilivamiwa na Polisi, wakanitembeza kote. Baadaye wakanipeleka Mbweni, baadaye wakanirudisha kwangu.

Sikutoa chochote zaidi ya hayo maelezo.”

Job Mrema: “Ulisema umetoa watu 466 katika magereza tofauti tofauti?”

Lissu: “Ndiyo, nilieleza. Sikutia chochote.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba tarehe 09 Aprili PW1 Bagyemu alifungua kesi ya uhaini?”

Lissu: “Ndiyo, alivyosema PW1 mwenyewe.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE
 
Sijui kwa nini, lakini binafsi naamini safari hii hawa Majaji hawatakubali kutumiwa na hawa watu waovu.

Najiweka mstari wa mbele kusutwa ikiwa matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yangu.

Tunatilia mashaka majaji sababu, kulikuwa ni wazi hakuna kesi ya kujibu "No case to answer"; lakini wametaka kumsikia. Wao kusema hawaangalii uzito wa ushahidi uliowasilishwa kwa jicho zuri ni wazi kuna hila. Wangekuwa wasafi hawa majaji au hawana maelekezo wasingefika huku kwenye "Kumsikia". Kumbuka kuna mambo yanaendelea kwenye system, tume zipo na taarifa zinakusanywa.

Hapo mahakama ina kimemo mkuu! Ni ukweli lakini mchungu.
 
Job Mrema: “Wewe kama mwanasheria...”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, mimi ni shahidi wa facts. Akihitaji kuzungumza na mwanasheria, aandae mkutano pembeni.

😄😄😄😄
Hawa Mawakili wepesi sana na hizi mbinu zao ni za kitoto sana
 
Tunatilia mshaka majaji sababu, kulikuwa ni wazi hakuna kesi ya kujibu "No case to answer"; lakini wametaka kumsikia. Wao kusema hawaangalii uzito wa ushahidi uliowasilishwa kwa jicho zuri ni wazi kuna hila. Wangekuwa wasafi hawa majaji au hawana maelekezo wasingefika huku kwenye "Kumsikia". Kumbuka kuna mambo yanaendelea kwenye system, tume zipo na taarifa zinakusanywa.

Hapo mahakama ina kimemo mkuu! Ni ukweli lakini mchungu.
Watamsumbua tu ila watafeli Lissu alishawahi kukiona kifo kwa lisasi 16 hana anachokiogopa
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba ushahidi alioutoa PW1 alitoa maelekezo kwamba tarehe 04 Aprili 2025 lifunguliwe jalada la uhaini?”

Lissu: “Kwa maelekezo yake ya Polisi ni sahihi, lakini wakati anatoa ushahidi hapa hiyo reference haipo.”

Job Mrema: “Lakini ipo katika kumbukumbu za Mahakama.”

Lissu: “Kama ipo katika kumbukumbu za Mahakama, nitakubali. Ninachosema ni kwamba katika notisi zangu haipo.”

Job Mrema: “Kwa ridhaa yenu, Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa kumbukumbu ni ukurasa wa 144. Swali langu, nimeuliza, atakubaliana na mimi?”

Swali lingine: “Ni sahihi PW1 wakati wa upelelezi wa kesi hii alitoa maelekezo ya kesi hii kwa ajili ya kufunguliwa majalada mawili ya uchunguzi, ambayo majalada hayo yana kumbukumbu CDS/IR/727/2025, ambalo ni jalada la uchunguzi?”

Lissu: “Hiyo ni sahihi.”

Job Mrema: “PW1 alitoa ushahidi pia wa jalada CDR/IR/771/2025, Publication of False Information?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Utakubali kuwa hujui utofauti wa haya majalada mawili na jalada la DCMZ?”

Lissu: “Jalada la DCMZ sijawahi kulisikia kabisa, sasa nitajuaje tofauti?”

Job Mrema: “Ulieleza Mahakama kwamba PW1, baada ya kuonyeshwa video na PW2, alipowaamuru kufunguliwa kwa jalada la ufunguzi hakukosea?”

Lissu: “Kuhusu jalada lipi?”

Job Mrema: “Majalada haya mawili.”

Lissu: “Alikosea kwa sababu alitakiwa amweleze DPP.”

Job Mrema: “Kifungu gani?”

Lissu: “Kifungu cha 16 kinasema DPP ndiye coordinator wa kuelekeza kufungua majalada ya uchunguzi. Kwa hiyo, alipaswa kufuata.”

Job Mrema: “Umesema hujui jalada linalofunguliwa kwa code ya PE na IR?”

Lissu: “Sikusema hivyo. Hayo ni maneno yako.”

Job Mrema: “Wakati wa kujitetea ulisema kufunguliwa kwa jalada hilo ilikuwa kinyume na presumption?”

Lissu: “Ndiyo.”

Job Mrema: “Kwa nini kufunguliwa kwa jalada hilo kulikufanya wewe uwe na hatia?”

Lissu: “Kwani jalada linasema nimefanya nini? Tayari linasema nimefanya kosa.”

“Kosa la kwanza hivi.”

Job Mrema: “Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya kusema huyu ana hatia?”

Lissu: “Mahakama.”

“Sasa ilikuwa waseme huyu ni mkosaji wa uhaini.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom