Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Tunatilia mashaka majaji sababu, kulikuwa ni wazi hakuna kesi ya kujibu "No case to answer"; lakini wametaka kumsikia. Wao kusema hawaangalii uzito wa ushahidi uliowasilishwa kwa jicho zuri ni wazi kuna hila. Wangekuwa wasafi hawa majaji au hawana maelekezo wasingefika huku kwenye "Kumsikia". Kumbuka kuna mambo yanaendelea kwenye system, tume zipo na taarifa zinakusanywa.

Hapo mahakama ina kimemo mkuu! Ni ukweli lakini mchungu.
gradually, my fellow, the tide is turning for the better.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Ajuaye: “Ni kweli kwamba video ni kifaa ambacho kinachapisha tu?”

Lissu: “Eheeeeee, hayo siyajui. Wanajua wataalamu.”

Ajuaye: “Unaniuliza mimi swali tena? Subiri nikishitakiwa, na mimi nitakukodi uniwakilishe kama wakili.”

Lissu: “Mimi huwa siwakilishi wateja wa namna yako wanaosingizia watu kesi.”

Ajuaye: “Ulisema kwamba mashahidi ni wahalifu?”

Lissu: “Nyie ndiyo mliwaleta, wakasema wao ni wahalifu.”

Ajuaye: “Ili mtu awe mhalifu atathibitishwaje?”

Lissu: “Na Mahakama.”

Ajuaye: “Mbona unasema wale mashahidi ni wahalifu?”

Lissu: “Nilisikia katika ushahidi wao wenyewe kwamba kesi zao zilifutwa ili waje kuwa mashahidi dhidi yangu.”

Ajuaye: “Nilisikia una challenge committal?”

Lissu: “Ndiyo.”

Ajuaye: “Ulichukua hatua gani?”

Lissu: “Nilileta kwa Majaji hapa mbele ya Mahakama kwamba hakimu amekataa.”

Ajuaye: “Unajua hiyo ni serious allegation?”

Lissu: “Ndiyo.”

Ajuaye: “Tukiangalia proceedings tutaona. Wewe ni mwanasheria?”

Lissu: “Unataka ukute nini, kama hakimu ndiye anayeandika committal?”

Ajuaye: “Ulichukua hatua gani?”

Lissu: “Nilileta kwa Majaji hapa. Au ulitaka nichukue hatua gani?”

Ajuaye: “Unajua kuna tofauti kati ya kuzuia uchaguzi na kupinga matokeo ya uchaguzi?”

Lissu: “Nafahamu, ila sisi tulikuwa tunapinga uchaguzi mpaka mabadiliko ya uchaguzi yafanyike.”

Ajuaye: “Ni kweli ukilenga kuzuia uchaguzi, unalenga kuzuia shughuli za uchaguzi?”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Job Mrema: “Wewe kama mwanasheria...”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, mimi ni shahidi wa facts. Akihitaji kuzungumza na mwanasheria, aandae mkutano pembeni.

😄😄😄😄
Hawa Mawakili wepesi sana na hizi mbinu zao ni za kitoto sana
Mkuu kama hujui sheria mahakamani utaacha ndala, lissu ameshahudhuria mahakamani hao wakiwa bado wanafunzi, tena wakifanya mitihani ya multiple choice😄, lisu anasema amefundishwa critical thinking, sasa wew jiulize miaka ya 60s kulikuwa na multiple choice?😂 ukijumlisha na experience, hapo hawawezi fua dafu.
 
Ajuaye: “Unaniuliza mimi swali tena? Subiri nikishitakiwa, na mimi nitakukodi uniwakilishe kama wakili.”

Lissu: “Mimi huwa siwakilishi wateja wa namna yako wanaosingizia watu kesi.”

Hivi hawa mawakili wa serikali huwa wanapatikana vipi ? 🤣🤣🤣
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba ushahidi alioutoa PW1 alitoa maelekezo kwamba tarehe 04 Aprili 2025 lifunguliwe jalada la uhaini?”

Lissu: “Kwa maelekezo yake ya Polisi ni sahihi, lakini wakati anatoa ushahidi hapa hiyo reference haipo.”

Job Mrema: “Lakini ipo katika kumbukumbu za Mahakama.”

Lissu: “Kama ipo katika kumbukumbu za Mahakama, nitakubali. Ninachosema ni kwamba katika notisi zangu haipo.”

Job Mrema: “Kwa ridhaa yenu, Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa kumbukumbu ni ukurasa wa 144. Swali langu, nimeuliza, atakubaliana na mimi?”

Swali lingine: “Ni sahihi PW1 wakati wa upelelezi wa kesi hii alitoa maelekezo ya kesi hii kwa ajili ya kufunguliwa majalada mawili ya uchunguzi, ambayo majalada hayo yana kumbukumbu CDS/IR/727/2025, ambalo ni jalada la uchunguzi?”

Lissu: “Hiyo ni sahihi.”

Job Mrema: “PW1 alitoa ushahidi pia wa jalada CDR/IR/771/2025, Publication of False Information?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Utakubali kuwa hujui utofauti wa haya majalada mawili na jalada la DCMZ?”

Lissu: “Jalada la DCMZ sijawahi kulisikia kabisa, sasa nitajuaje tofauti?”

Job Mrema: “Ulieleza Mahakama kwamba PW1, baada ya kuonyeshwa video na PW2, alipowaamuru kufunguliwa kwa jalada la ufunguzi hakukosea?”

Lissu: “Kuhusu jalada lipi?”

Job Mrema: “Majalada haya mawili.”

Lissu: “Alikosea kwa sababu alitakiwa amweleze DPP.”

Job Mrema: “Kifungu gani?”

Lissu: “Kifungu cha 16 kinasema DPP ndiye coordinator wa kuelekeza kufungua majalada ya uchunguzi. Kwa hiyo, alipaswa kufuata.”

Job Mrema: “Umesema hujui jalada linalofunguliwa kwa code ya PE na IR?”

Lissu: “Sikusema hivyo. Hayo ni maneno yako.”

Job Mrema: “Wakati wa kujitetea ulisema kufunguliwa kwa jalada hilo ilikuwa kinyume na presumption?”

Lissu: “Ndiyo.”

Job Mrema: “Kwa nini kufunguliwa kwa jalada hilo kulikufanya wewe uwe na hatia?”

Lissu: “Kwani jalada linasema nimefanya nini? Tayari linasema nimefanya kosa.”

“Kosa la kwanza hivi.”

Job Mrema: “Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya kusema huyu ana hatia?”

Lissu: “Mahakama.”

“Sasa ilikuwa waseme huyu ni mkosaji wa uhaini.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Haya maswali ndio ya uhaini?
 
Back
Top Bottom