Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Ajuaye: “Shahidi, una PGO?”

Lissu: “Ninayo.”

Ajuaye: “Soma 403.”

Lissu: “Paragraph ipi?”

Ajuaye anainama kwa wenzake, wanapekua.

Ajuaye: “Wakati tunatafuta PGO, soma Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Lissu: “Nipatie, sina hapa. Au nisomee inasemaje.”

Lissu: “Au nikusaidie PGO 403 ya kuhusu ‘Other Meetings’?”

Ila serikali haina watu aisee, imagine huyu ni wakili wa kesi ya uhaini
Huyu atakuwa alipitia Merton College. Yeye ndio Katoa kifungu halafu anajifanya hakioni mpaka Asaidiwe na mtuhumiwa.
 
lisu alipokua akiwahoji wale mashahidi wa serikali alikua kanyooka na maswali hayaendi nje ya walicho kisema sasa kwanini hawa mawakili wa serikali wanzunguka na kujigeuza kama kambare?, anauliza swali hili anaruka anaenda huku what for?
 
H
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Job Mrema: “PW1 alieleza hapa Mahakamani kwamba majalada yamefunguliwa kwa kufanya uchunguzi wa yaliyofanywa na wewe.”

Lissu: “Nilikuwa tayari ni mkosaji kwao, ndiyo maana nalalamika nimebambikiziwa kesi.”

Job Mrema: “Unafanya nini hapa sasa hivi?”

Lissu: “Najitetea kwa kesi ya kubambikiwa.”

Job Mrema: “Mahakama hii imeshatoa uamuzi wa hii kesi?”

Lissu: “Haijatoa.”

Job Mrema anaenda kuteta na Jopo la Mawakili wa Serikali.

Job Mrema: “Waheshimiwa Majaji, mimi naomba kuishia hapa. Naomba kumkaribisha Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye.”

Ajuaye: “Shahidi, ni kweli wakati unafanya mkutano wako kuhusu uchaguzi haukuwa na kibali chochote kutoka mamlaka yoyote?”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, mikutano ya ndani haihitaji vibali, na hata mikutano ya hadhara haihitaji vibali, ni taarifa.”

Ajuaye: “Shahidi, una PGO?”

Lissu: “Ninayo.”

Ajuaye: “Soma 403.”

Lissu: “Paragraph ipi?”

Ajuaye anainama kwa wenzake, wanapekua.

Ajuaye: “Wakati tunatafuta PGO, soma Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Lissu: “Nipatie, sina hapa. Au nisomee inasemaje.”

Lissu: “Au nikusaidie PGO 403 ya kuhusu ‘Other Meetings’?”

Ajuaye: “Soma 402.”

Lissu: “Inasema kuhusu Political Party Campaigns.”

Ajuaye: “Soma.”

Lissu: “Wakati wa uchaguzi au kampeni, vyama vitatoa taarifa kwa Polisi.”

Ajuaye: “Sasa wewe ulitoa taarifa kwa Polisi?”

Lissu: “Sikutoa kwa sababu haukuwa wakati wa kampeni na haukuwa mkutano wa kampeni.”

Ajuaye: “Na ilikuwa bado kampeni hazijaanza.”

Lissu: “In fact, ni miezi sita mbele kabla ya kampeni ndipo mkutano ulifanyika.”

MAHAKAMA: Kicheko.

Ajuaye: “Soma Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Lissu: “Nisomee.”

Ajuaye anasoma...

MAHAKAMA: Kicheko.

Lissu: “Asante. Uliza swali.”

Ajuaye: “Ni kweli ulitakiwa upeleke notification Polisi?”

Lissu: “Si kweli. Huo ulikuwa mkutano wa ndani. Sheria inasema mkutano wa ndani.”

Ajuaye: “Ni kweli sheria ina option mbili, mkutano wa ndani na nje?”

Lissu: “Si kweli. Mikutano ya hadhara tu ndiyo inahitaji notification.”

Ajuaye: “Next?”

MAHAKAMA: Kicheko.

Ajuaye: “Kuna sehemu inasema ‘any place of any area’?”

Lissu: “Si kweli kwamba ‘any place’ ni of any public area.”

Ajuaye: “Next?”

Lissu: “Tulia basi, mbona unaharaka?”

Lissu: “Swali lingine.”

Ajuaye: “Kuna sheria inasema unaweza kufanya mkutano wowote bila kibali?”

Lissu: “Kifungu hicho hicho.”

Ajuaye: “Ni kweli mliwaita waandishi wa habari na hivyo hauwezi kuwa mkutano wa ndani?”

Lissu: “It doesn't make it a public meeting. Ni mkutano wa ndani uliorushwa live.”

Ajuaye: “Ni kweli kwamba umekuwa ukisema maneno ya hati ya mashitaka ni ya kwako?”

Lissu: “Nimeongea maneno yaliyopo katika hati ya mashitaka yasiyo ya uhaini mbele ya waandishi wa habari.”

Ajuaye: “Uliyaongea au hujayaongea?”

Lissu: “Hayo maneno ambayo nimeongea kwa zaidi ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE
uyu ajuaye ndio kabisaaaa dah masikini
 
Job Mrema: “Mashahidi ambao wamepata ulinzi unawakumbuka?”

Lissu: “Nawakumbuka majina bandia, lakini siwajui sura zao. Majaji hawawajui. Nakumbuka herufi P na sijui nini.”
Hahahah, kwanini serikali ina mawakili vilaza hivi jamani, yani toka asubuhi wanazunguuka kwenye kutaka lissu awatambue hawa mashaidi wa vificho.
 
Mbona sisi hatuhoji nchi kuongozwa na mama mtoto na mkwe wake

RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN

Makamu wake ni Ndejembi

CCM mwenyekiti DK SAMIA SULUHU HASSAN
Makamu mwenyekiti ni Mzee Wasira

CHADEMA ya 2025 MUME na SHEMEJI yake wanakusanya tone tone kutoka kwa Wananchi mikoa
mbali mbali ‼️

Mwenyekiti changieni chama pesa mpeni SHEMEJI Heche 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 

Attachments

  • 6383535-d2a99db8c1716a1080d26b345b5eadf6.jpg
    6383535-d2a99db8c1716a1080d26b345b5eadf6.jpg
    20.3 KB · Views: 12
Back
Top Bottom