Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Lissu: “Kuzuia shughuli zote za uchaguzi; kampeni zisifanyike, matokeo yasitangazwe — shughuli zote za uchaguzi.”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, utaratibu wa saa 1 tunahairisha umekuwa suspended?”

Jaji Ndunguru: “Unasema, Mshtakiwa?”

Lissu: “Umekuwa ni utaratibu, ikifika saa 11 tunahairisha. Sasa ni saa 11 inaenda na nusu.”

Jaji Ndunguru: “Nilikuwa nahisi anamaliza swali la mwisho hili, lakini tunaona anaendelea.”

Ajuaye: “Ni dhahiri Mshtakiwa atakuwa amechoka. Tunaomba ahirisho.”

Lissu: “Ni kweli, nimekuwa nikihojiwa maswali tangu saa 3 asubuhi.”

Majaji wanateta.

Magereza wanasogea kizimbani kwa Lissu.

Jaji Ndunguru: “Kwa hiyo shauri linahairishwa mpaka kesho saa 3 asubuhi.”

WEKA EMOJI

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
 
Kwa akili zangu na upeo wangu huwa nikiona mtu kanizidi kete dawa huwa ni kukubali tu yaishe
Sasa nikiangalia hawa mawakili wa serikali wanavyopelekeshwa na mtu mmoja natamani nipate nafasi ya kuonana nao niwaambie mbele ya lissu mmeshapelea
Wanahangaika sana. Ila Katuga alisema wapo kazini inabidi wafanye kazi.
 
Huyu ajuaye walimuokotea wapi?
 
nafkiri kuna haja ya kuja kuitafuta na kuisoma kesi yote ya kina Ghandi ili kuelewa kesi halisi ya uhaini na viashiria vyake ili kujifunza ila huku sipati kuelewa kabisa uhaini ni nini na huwa una viashiria gani ukweli. ni kujifunza tu na kuelewa
Maana naona wanahangaika na mkutano na maneno. Uhaini au kiashiria cha Nia ya uhaini haionekani.
 
Tunakutegemea kwa updates
 
Ajuaye: “Shahidi, una PGO?”

Lissu: “Ninayo.”

Ajuaye: “Soma 403.”

Lissu: “Paragraph ipi?”

Ajuaye anainama kwa wenzake, wanapekua.

Ajuaye: “Wakati tunatafuta PGO, soma Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Lissu: “Nipatie, sina hapa. Au nisomee inasemaje.”

Lissu: “Au nikusaidie PGO 403 ya kuhusu ‘Other Meetings’?”

Ila serikali haina watu aisee, imagine huyu ni wakili wa kesi ya uhaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…