Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

Tanzania one anaionesha mahakama na umma kwamba kichwa hiko na kitu sio zero brain...
 
Yaani ushahidi wa Mnyika unawavua nguo hawa waliandaa hii kesi, mawakili wa serikali naona na hapa wamepigwa KO, Maana Lissu yeye haandai Mkutano lakini wao kwenye mashitaka yao wamemshitaki Lissu 🤣🤣🤣
 
Yaani kwa kifupi unataka kusema hivi...

Jamuhuri ilisubiri kitendo... Kwa kufanya yafuatayo....

Walikamata watuhumiwa wa Uhaini... Kisha wakawahoji na kuwafutia kesi zao ili wawe mashahidi kesi ya Lissu..

Kisha watuhumiwa wanaachiwa wanarudi mitaani ..baadae miezi 7 mbele wanafanya tukio (Lissu yupo ndani) .. Kisha Serikali inasema kweli tukio limetokea..... Tuendelee na kesi...

Tanzania itakuwa ni channel ya vituko Duniani
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Lissu: Upo Mahakamani kwa sababu ya shitaka la kesi inayonikabili mimi.

Ambapo shitaka linasema tarehe 03 Aprili mwaka jana, 2025, niliitisha Mkutano wa watia nia ya kugombea Ubunge kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Katika Mkutano huo nilitengeneza nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Waeleze Majaji kama una ufahamu wowote kuhusu Mkutano huo.

Jaji Ndunguru: Ingawa umeanza kumlisha maneno.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, sijamlisha maneno yoyote. Haya niliyoeleza ni maneno yaliyopo katika Preliminary Hearing na katika Mashitaka yangu.

Mnyika: Nina ufahamu kuwa Mkutano huo uliandaliwa kwa maelekezo yangu na uliandaliwa na Sekretarieti ya Makao Makuu, ambayo nilisimamia vikao vyake kwa kupanga maandalizi ya Mkutano.

Na niligawa majukumu ya maandalizi ya Mkutano huo.

Lissu: Twende taratibu, usikimbie kuliko mimi.

Mnyika: Na nilikubali fedha za maandalizi ya Mkutano huo kama Afisa Masuhuli (Accounting Officer).

Na nilishiriki Mkutano wenyewe.

Lissu: Sasa, Shahidi, kwenye ushahidi wako wa mwanzo ulisema kuna aina mbili za mikutano ya chama.

Mikutano ya hadhara au mikutano ya ndani ya chama.

Eleza Majaji, huo ulikuwa ni Mkutano wa hadhara au Mkutano wa ndani ya chama.

Mnyika: Ulikuwa ni Mkutano wa ndani wa Chama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huo Mkutano unahusu nini na ulikuwa wapi?

Mnyika: Mkutano ulikuwa kama sehemu ya utekelezaji wa azimio la Mkutano Mkuu wa Chama wa kutaka kufanyika kwa mabadiliko na mageuzi ya Kikatiba na ya kisheria, ya kuwezesha kuwepo kwa uchaguzi wa huru na haki chini ya kaulimbiu ya “No Reforms, No Election.”

Na kwa tafsiri yetu ya Kiswahili, ni “Bila mabadiliko, hakuna uchaguzi.”

Lissu: Nimekuuliza sehemu ya pili, huo Mkutano uliwahusu kina nani?

Mnyika: Mkutano uliwahusu waliokuwa na nia ya kugombea uchaguzi wa 2025, maarufu kama watia nia wa uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Kulingana na Katibu Mkuu Mnyika; Mwenyekiti wa Chama sio Mjumbe wa Secretariat ya chama hicho. Kwa tafsiri ni kwamba, Mkutano ule uliandaliwa na Katibu Mkuu na Mwenyekiti alialikwa tuu. 😊
Njama ya Uhaini upande wa mashitaka, inaanza kuishiwa "pawa".
 

Hoi sio karunguyeye. Hii ni nungunungu
 
Twende
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Hapa bila copy za WhatsApp, ikiwa katika mfumo wa maelezo ya kawaida:

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama mkutano nje ya Sekretarieti na watia nia walialikwa, ni kina nani wengine?

Mnyika: Tulialika viongozi wakuu wa Chama na waandishi wa habari.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ukisema ulialika viongozi wakuu wa Chama, unamaanisha kina nani?

Mnyika: Namaanisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Antipas Lissu; Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche; Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Saidi, na viongozi wakuu wengine ambao ni sehemu ya Sekretarieti, ambao ni Katibu Mkuu na manaibu wake.

Lissu: Waeleze Majaji, huo mkutano unaouita wa ndani ulifanyikia wapi?

Mnyika: Ulifanyika Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, Mtaa wa Daima, Nyumba Namba 31.

Lissu: Waandishi wa habari wa vyombo vipi ambao mliwaalika, kwa kumbukumbu zako?

Mnyika: Tuliwaalika wote kwa ujumla, na walialikwa na Brenda Jonas Rupia.

Nilielekeza vilevile itolewe taarifa ya habari kwa umma ya wazi.

Ambayo ilitolewa tarehe 27 mwezi Machi, na ilitolewa na Brenda Rupia.

Ambayo ilialika waandishi wa habari, lakini pia iliutaarifu umma kuhusu kikao hicho.

Lissu: Wakati wewe na Sekretarieti yako mnafanya yote haya, Mwenyekiti wako alikuwa wapi?

Mnyika: Alikuwa katika ziara Kanda ya Nyasa, akiendelea na Operesheni ya Katiba Mpya.

Lissu: Kanda ya Nyasa ni wapi?

Mnyika: Inajumuisha Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo ziara ya Mwenyekiti ilitumia muda gani?

Mnyika: Nakumbuka ilianza tarehe 23 mwezi Machi hadi kabla ya tarehe 03 Aprili.

Lissu: Waeleze Majaji kama Mwenyekiti wa Chama alishiriki maandalizi yoyote?

Anasimama Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, tunaona shahidi anavyoongozwa kwa taratibu za in-chief zinakiukwa.

Tunaomba Bwana Tundu Antipas Lissu akumbushwe namna ya kuongoza mashahidi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Ajuaye kauliza swali moja tuu😀. Sasa si angelimalizia jana tu mambo yakaisha😀
Nilisema toka juzi, huyo Katuga ndio wanayemtegemea, kama yeye ameflop, hao wengine wao ni kijitutumua tu ili wasionekane hawajafanga chochote. Nilisema hao wengine watakuwa na maswali machache yasiyo na maana kabisa.
 
jamaa anawatengenezea ugumu kwenye cross examination mpaka inaogopesha maana namna ya maswali na majibu yote yanajisheleza bila kuachia mianya dah🤣🤣
 
job mrema tulia baba shahidi atoe maelekezo mbona ninyi hamkupewa limit wakati mnawahoji mashahidi wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…