Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Mkuu una exposure kubwa sana, kongole.

Asante kwa kutufundisha hili, wengine hatujui lolote juu ya haya mambo.
 
KOSA LA UHAINI

KUNA KILIHOFANYWA NA LISU? HAKUNA

Kisheria, kosa la uhaini linatendeka pale ambapo mtu anafanya vitendo au njama za hatari zinazolenga kuhatarisha usalama wa nchi au kuipindua serikali halali.
Kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu (Penal Code, Cap 16) ya Tanzania, mambo yafuatayo yakitendeka yanafanya kosa la uhaini kuwa limetendeka: [

Matendo Yanayofanya Uhaini
    • Kumdhuru Rais: Kumuua au kujaribu kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    • Kuanzisha Vita: Kuanzisha vita au kuchochea uvamizi wa kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Muungano ndani au nje ya nchi.
    • Kusaidia Maadui: Kushirikiana na maadui wa nchi kwa kuwapa misaada, siri, au taarifa za kuhatarisha usalama.
    • Kutumia Silaha: Kuchukua silaha kwa lengo la kulazimisha serikali ibadilishe maamuzi yake au kuiondoa kwa nguvu.
    • Njama za Kupindua: Kupanga, kushauri, au kuwashawishi wengine kuiondoa serikali madarakani kwa njia zisizo za kikatiba.

Vipengele Muhimu Vya Kisheria (Elements)
Ili mtu akutwe na hatia ya uhaini, mahakama inapaswa kujidhirishisha kwa mambo haya:
    • Nia Mbaya (Hostile Intent): Kuwepo kwa dhamira au nia ya wazi ya kusaliti au kuvuruga mamlaka ya nchi.
    • Kitendo Halisi (Overt Act): Mtuhumiwa awe amechukua hatua au kufanya kitendo kinachothibitisha mpango huo (si tu kuwaza).
    • Utiifu (Allegiance): Mtuhumiwa kuwa ni raia wa Tanzania au mtu aliye chini ya utii wa sheria za nchi.
 
TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO NA WAKILI WA SERIKALI

Muendelezo wa Dodoso la Mshtakiwa

MAHAKAMA NIMEREJEA

Majaji wameingia tayari.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, tupo tayari kwa dodoso kwa mshitakiwa.

Jaji Ndunguru: Shahidi, kiapo chako kinaendelea na upo tayari kwa maswali ya dodoso?

Lissu: Nipo tayari.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji, tutauliza maswali wote na ataanza Nassoro kama tulivyojipanga.

Nassoro Katuga: Shahidi, pole na ushahidi mrefu kwanza.

Lissu: Asante sana.

Nassoro Katuga: Leo, kama nilikusikia vizuri, ulisema utatuacha tuulize maswali sisi ndugu zako?

Lissu: Nafikiri nilisema hivyo.

Nassoro Katuga: Utakubali kwamba hiki ni kitu cha kisheria tunachoenda kufanya, mimi na wewe hatuna masuala binafsi zaidi ya kusaidia Mahakama?

Lissu: Mimi na wewe hatuna masuala binafsi.

Nassoro Katuga: Nimesikia unasema wewe ni mtaalamu wa sheria.

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Sitokosea nikisema wewe ni mwanasheria mbobevu?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Tanzania ilipata lini uhuru?

Lissu: 9 Desemba 1961.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema Tanzania ni nchi huru?

Lissu: Sahihi.

Nassoro Katuga: Ni chombo gani cha mwisho kutoa maamuzi?

Lissu: Mahakama ya Rufaa.

Nassoro Katuga: Tuseme Mahakama.

Lissu: Hapana, umesema chombo cha mwisho.

Nassoro Katuga: Sawa.

Nassoro Katuga: Mahakama ipo huru kutoa uamuzi wake na hailazimishwi.

Lissu: Hailazimishwi.

Nassoro Katuga: Je, nimesikia wewe ni Mwenyekiti wa CHADEMA?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Je, umeiambia Mahakama una kinga ya kutoshitakiwa kwa sababu wewe ni Mwenyekiti wa CHADEMA?

Lissu: Sina kinga na sijaiambia.

Nassoro Katuga: Nilisikia Mahakamani unasema una tuzo mbalimbali. Hebu tuambie zilikuwa katika fomu gani.

Lissu: Unapokuwa umepewa tuzo unapewa maandishi.

Nassoro Katuga: Hapana, nauliza tuzo hizo zina cheti?

Lissu: Niache sasa nikujibu.

Unapokuwa unapewa tuzo, siyo mfanano wa aina moja.

Unapewa citation au katuzo, kama mfanano wa Kombe la Dunia.

MAHAKAMA KICHEKO

Nassoro Katuga: Je, hizo tuzo zote ulizileta Mahakamani?

Lissu: Sijaleta na sina wajibu wake.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Tuendeleee jamani, bado hawajatoka?

Leo na jana kwakwel ni kwa mtoto, CCM inapitishwa kwenye moto kuanzia chamani mpaka Mahakamani, wanaona aibu sasa hata wakiwaza kumfunga hawajui huyu aliyejiuzulu ataanza kurusha mawe kuanzia wapi, waswahili wanasema usianzishe ugomvi kama unaishi kwenye nyumba ya vioo
 
Nassoro Katuga: Ni chombo gani cha mwisho kutoa maamuzi?

Lissu: Mahakama ya Rufaa.

Nassoro Katuga: Tuseme Mahakama.

Lissu: Hapana, umesema chombo cha mwisho.

Nassoro Katuga: Sawa.


Ila lissu dahh 😀😀😀😀
 
Mbona huyo Katuga hana maswali, hebu aje mwenye maswali anatuchelewesha
 
Nassoro Katuga: Ni chombo gani cha mwisho kutoa maamuzi?

Lissu: Mahakama ya Rufaa.

Nassoro Katuga: Tuseme Mahakama.

Lissu: Hapana, umesema chombo cha mwisho.

Nassoro Katuga: Sawa.


Ila lissu dahh 😀😀😀😀
Ni shidaaa
 
TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO NA WAKILI WA SERIKALI

Nassoro Katuga: Uliposema hatujaleta video, wewe umeleta maneno na nini?

Lissu: Sina kazi ya kuthibitisha kama wewe.

Nassoro Katuga: Ni sheria ipi inasema natakiwa kuleta video?

Lissu: Sheria ya Ushahidi.

Nassoro Katuga: Umesema kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi, anayetakiwa kuthibitisha anatakiwa kuja na ushahidi?

Lissu: Siyo kifungu cha ngapi, bali sheria inasema unapoleta ushahidi wa nyaraka lazima ulete nyaraka.

Nassoro Katuga: Sheria ipi?

Lissu: Principles of sheria ya ushahidi.

Nassoro Katuga: Twende taratibu, tutavunja undugu. Usilete ujuaji.

Lissu: Siyo lazima uwe ndugu yangu na mimi ni mjuaji haswa.

Nassoro Katuga: Principle ya wapi?

Lissu: Principle ya sheria.

Nassoro Katuga: Ile sheria ya mtu anayeleta shutuma must prove, wewe umeprove?

Lissu: Mimi nimeprove mtu safi.

Nassoro Katuga: Ulisema hii ni nchi huru.

Lissu: Ndiyo, ni nchi huru.

Nassoro Katuga: Ukiwa shahidi, kuna sehemu yoyote umekanusha maneno ya “Tutakinukisha, tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi”?

Kama nimekusikia, umesema haya maneno kwamba wameyatoa katika video ya masaa matatu.

Katika ushahidi wako wote, kuna neno lolote katika Mahakama hii umesema maneno haya siyo ya kwangu na ukitaka kuyaelewa lazima usikilize video yote?

Lissu: Maneno ya mashahidi wenu.

Nassoro Katuga: Mimi siwezi kutumia yale maneno yako. Ulikuwa unauliza mashahidi kwamba “una akili timamu.” Wewe ni kaka yangu.

Nassoro Katuga: Ulisema siyo ya kwako, hukusema?

Lissu: Sikusema.

Nassoro Katuga: Sasa wewe ni kaka yangu, unajizungusha-zungusha muda wote nini?

Lissu: Sijakataa, nimesema haya. Shida nakataaje na hayana shida.

Nassoro Katuga: Umesoma historia?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Ni kweli wakoloni waliwatumia viongozi wenye tamaa ya uongozi?

Lissu: Viongozi gani?

Nassoro Katuga: Je, wazungu waliingia Afrika kwa kutumia viongozi wenye tamaa?

Lissu: Waliwatumia viongozi kupitia mikataba.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo Waarabu waliingia kama wakoloni kwa kutumia viongozi wenye tamaa?

Lissu: Waarabu hawakuwa wakoloni, walikuja kama wafanyabiashara.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo unakubali kwamba waliingia mikataba?

Lissu: Ndiyo, kama wanavyoingia mikataba kina Samia leo. Hawakuingia na watu wa chini huku.

Nassoro Katuga: Ulisema kuhusu utetezi wa madini?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Na ukawa unatetea makinikia yatoke?

Lissu: Huko sikusema, lakini ukitaka nitakwambia kuhusu taarifa ya Magufuli kwamba ilikuwa “professorial rubbish.”

Nassoro Katuga: Unasema mtetezi wa madini na unapigania yatoke?

Lissu: Ukitaka huko twende tu.

Nassoro Katuga: Nitarudi baadaye.

Nassoro Katuga: Ulisema ulikuwa Rais wa TLS?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Umeiambia Mahakama kwamba ulishaitakiwa wakati ukiwa Rais wa TLS katika kesi hii?

Lissu: Hapana.

Nassoro Katuga: Nilisikia unasema wewe ni mtaalamu wa kesi za uchaguzi.

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Je, ni namna gani sheria inasema Tanzania namna ya kupiga uchaguzi, au sheria inayokinzana na Katiba?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Mambo ni mengi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…