Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

Eti leo Heche ndio mwenye nguvu Chadema kuliko Mh Lema
Kuliko Mnyika
Heche katokea wapi kabla ya kuja Shemeji Chamani 😂😂

Kuwa Mbunge mbona wengi tu walikuwa Wabunge wa
Chadema❗️
lkn hawana nafasi kubwa ndani ya Chadema
kwanini wewe ❗️

na kwanini
wapuuzwe wenye mizizi pale Chadema❗️❗️

Heche kwanzia leo mpaka Jumatatu & Jumanne sisi nawewe Heche
utasema
kila kitu kwafaida ya
Watanzania ✍️
 
Mwamba unaupiga mwingi mpaka unamwagika
 
Chama kuwa na wenye mizizi, akili mgando hizi. Chama ni cha watu wote yeyote ruksa kuwa kiongozi as long as ana sifa. Chama si mali ya ukoo ndo maana huwa nakudharau toka nikujue kwa kuamini upeo wako ni finyu sana
 
Huu ni Udhalilishaji, kumbuka hata sisi ndiko tunapoelekea. Hawa ni wazazi wetu wanahitaji kuheshimiwa
 
Amefumua mengi sana, ingekuwa ni hatari kwake angeshaambiwa na Lissu
Ngoja tutajionea hapa ndipo sehemu sahihi pakumpima John Heche mpaka Sasa John Mnyika ndio kafanya vizuri sana kama Heche akaweza mtihani wa kina katuga basi Lissu atakuwa na mtaji mzuri wa kuwa na mashahidi watatu wenye maelezo yalionyooka kutumika na mahakama kufanya maamuzi na hao ni John Mnyika, Lupia na John Heche kama akifanya vizuri yule mwingine alichemka
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 9.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako na kwa kumbukumbu zako, uwapo wa maneno:

“Jeshi la Ulinzi/Wananchi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Mgambo, Jeshi la Akiba,”

na maneno ya namna hii katika hotuba yangu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zangu, hakuna maneno:

“Jeshi la Ulinzi/Wananchi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Mgambo, Jeshi la Akiba,”

katika hotuba yake.

Lissu: Sasa, shahidi, hao wote niliowataja ndiyo Serikali. Waeleze Waheshimiwa Majaji, haya maneno walitonishtaki nayo yamemtishia nani?

Heche: Haya maneno hayajamtishia mtu yeyote aliyetajwa hapo juu. Ni maneno ya kawaida.

Lissu: Sasa, shahidi, kwa ufahamu wako, waeleze Waheshimiwa Majaji, haya maneno niliyokusomea yana kosa gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, haya maneno sioni kosa lolote, kwa sababu ni maneno ya kawaida ya kisiasa.

Lissu: Sasa, shahidi, kwenye ushahidi wako ulisema ulikuwepo katika huo mkutano, na umeona hizo video za Chanzo, Mwanzo na Jambo.

Sasa, katika hizo video, waeleze Waheshimiwa Majaji uwapo wa maneno: “Tunaenda kuchoma vituo vya kupigia kura.”

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hiyo hotuba hakuna mahali Mwenyekiti amesema katika hotuba yake, “Tunaenda kuchoma moto vituo vya kupigia kura.”

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kwenye video na ukumbini nilisema, “Tunaenda kuchoma vituo vya mwendo kasi, magari na vitu.”

Heche: Hakuna mahali popote kumetajwa, “Tunaenda kuchoma vituo vya mwendo kasi, magari na vitu.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.

KUNA MAKOSA YA KIUNDISHI UNAONA?
 
Ila kuna comment za watu humu zina furahisha na kusikitisha sana sana si aheri izo ela za bando wangenunulia juice za miwa kuboresha afya kuliko kujitoa akili kama wafanyavyo kweli inasikitisha

Nyinyi mlitaka Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupelekwa ICC

MUNGU ACHEZEWI UYO kunja uso Heche kikaangoni🫎🫎

mbele ya Mahakama
majibu ya Mungu mkuu
tunayaona ndani ya Tanzania mchana kweupe ✍️

Wenye hatia wanadhalilika mbele ya Macho yetu vile vifo vitawasakama Daima milele ✍️
 
sisi wangapi mkuu na wapi uliona comment kama iyo kuwa makini usikurupuke stick to the lecture.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwapo wa maneno, “Mkakate vidole watakaoenda kupiga kura au wapigwe.”

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala popote amesema kuwa tukakate vidole wanaoenda kupiga kura au kuwapiga.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwapo wa maneno katika hotuba yangu watu wakaue polisi au waumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uwapo wa maneno katika hotuba ya Mwenyekiti juu ya watu wakaue polisi au waumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama ulisikiliza hotuba ya Jaji Chande.

Heche: Nilisikiliza hotuba yake.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama ulisikiliza hotuba yote.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nilisikiliza hotuba yote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa maneno kwamba vurugu zilisababishwa na Tundu Lissu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala popote ambapo hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande imesema kwamba vurugu zilisababishwa na Tundu Lissu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Siku ya tatu Lissu anamhoji Heche. Maswali ni yaleyale yanazunguka na yanaulizwa kwa namna tofauti
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwapo wa maneno katika hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa maneno kwamba Tundu Lissu alichochea vurugu.

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, tunaomba swali lirekebishwe.

Lissu: Tundu, nitarudia. Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwapo wa nani alichochea vurugu za tarehe 29 Oktoba.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala Jaji Othuman Chande ametaja mtu yeyote aliyechochea vurugu za tarehe 29 Oktoba.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwapo wa jina la chama cha siasa kilichochochea hizo vurugu za tarehe 29 Oktoba.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala ametaja jina la chama kilichochochea hizo vurugu za tarehe 29 Oktoba.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa majina ya watu wanaodaiwa kukatwa vidole.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala watu waliokatwa vidole wametajwa.

Lissu: Au walio wakata watu vidole?

Heche: Kwenye hotuba hiyo, Waheshimiwa Majaji, hakuna mahala wametajwa majina ya watu waliokata watu vidole.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa majina ya askari walio uawa na watu walio wauwa hao askari.

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hotuba ya Jaji Chande hakuna mahala pametajwa majina ya askari waliouawa au watu waliowaua.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa majina ya watu waliouawa au watu waliowaua.

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hotuba ya Jaji Chande hakuna majina ya watu waliouawa na walioua.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama katika hiyo hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Mohammed Chande, uwapo wa majina ya maeneo ambayo vituo vilichomwa.

Heche: Sina kumbukumbu na hilo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye hotuba ya Jaji Mkuu Othuman Chande, uwapo wa orodha ya magari ya watu binafsi au ya Serikali yanayodaiwa kuchomwa moto.

Heche: Orodha au idadi?

Lissu: Orodha, kila gari ina aina na namba.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna orodha na majina ya magari yanayodaiwa kuchomwa.

Lissu: Sasa, shahidi, mimi nilikuwa gerezani wakati haya yanatokea. Nilishashitakiwa, gerezani tayari.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, wewe ambaye hukuwa gerezani au viongozi wenzako wa chama kuitwa kwenda kueleza chochote mbele ya Tume ya Jaji Othuman Chande.

Heche: Hebu rudia swali.

Lissu: Uliitwa wewe na viongozi wenzako?

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi binafsi sikuwahi kuitwa na sina ufahamu wa viongozi wengine kuitwa kwenda kutoa maelezo kwenye Tume ya Jaji Chande.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Katiba ni sauti ya umma
na kuna uhuru wa kuongea
Na nyie si ndio mmenituma,
mpo tayari kunitetea?

Wilaya mnafanya mkoa
ili wapangwe washkaji
mkuu wa wilaya changudoa
hii ni miradi ya upigaji

watasafirisha nyani,
sisi tunashangaa Twiga?
utamfunga nani ?
yeye na mwanasheria mkuu ni maswahiba….
 
Mpaka hapa amefanya vizuri, wasiwasi wetu asije akapaniki kwa maswali ya kijinga, watampeleka huko ili aingie kwenye mfumo wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…