Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

Mpumbavu pekee ubomoa ndoa yake kwa kupaste aonacho.
Mwanzilishi wa ndoa alitengeneza mfumo, sheria na kanuni Ili ndoa idumu kuanzia uchaguzi wa mtu sahihi, jinsi ya kuishi pamoja, malezi ya watoto, nk. Sema tu binadamu tuna ubinafsi ndio upelekea talaka.
Kanuni namba moja ni kiwa hamjagegeda au kugegedwa kaabla ya ndoa. Ma milioni ya ndoa tayari zinakuwa zilishafeli hiki kipengele alafu bado wanataka ndoa idumu. Kujidanganya tuu.

Tunasema ndoa ni kuvumiliana lakini hao wanandoa watarajiwa wameshindwa kuvumilia kula mbususu na de libolo. Je kweli hawa watakuwa na uvumilivu ndani ya ndoa? Tusiwe na matarajio ya ajabu wakati sifa za kuishi kwenye ndoa wengi wetu hatuna.
 
Nimeeleza sababu za kukosoa ambazo ziko katika mfumo wa swali, kama unaweza kujibu swali itakuwa vizuri, kama huwezi pia ni sawa tu.

Umemsifu na kumuweka kama role model wako, nikataka kukuonyesha kuwa huyo unayetamani kuwa kama yeye, hoja yake haina mashiko.
Haya mambo huyawezi wewe hahahaha
 
Kanuni namba moja ni kiwa hamjagegeda au kugegedwa kaabla ya ndoa. Ma milioni ya ndoa tayari zinakuwa zilishafeli hiki kipengele alafu bado wanataka ndoa idumu. Kujidanganya tuu.

Tunasema ndoa ni kuvumiliana lakini hao wanandoa watarajiwa wameshindwa kuvumilia kula mbususu na de libolo. Je kweli hawa watakuwa na uvumilivu ndani ya ndoa? Tusiwe na matarajio ya ajabu wakati sifa za kuishi kwenye ndoa wengi wetu hatuna.
Mkishatafunana mnaunganisha nafsi na tabia mbaya na madhaifu ya mwenzio ujificha,ngono ni sumaku utamu wa ngono uzuia kuona mapungufu ya mwenzio. Thus mila na dini vinapinga watu wanaotegemea kuishi pamoja kufanya ngono Ili iwe rahisi kumjua mwenzio. Ngono ndio sumaku iwavutayo watu kuingia kwenye ndoa bila kujua mapungufu ya mwenza.
Mkishaunganisha nafsi hamuwezi chunguzana.
 
Mkishatafunana mnaunganisha nafsi na tabia mbaya na madhaifu ya mwenzio ujificha,ngono ni sumaku utamu wa ngono uzuia kuona mapungufu ya mwenzio. Thus mila na dini vinapinga watu wanaotegemea kuishi pamoja kufanya ngono Ili iwe rahisi kumjua mwenzio. Ngono ndio sumaku iwavutayo watu kuingia kwenye ndoa bila kujua mapungufu ya mwenza.
Tuache uasherati jameni. Hakuna jema litokanalo na uasherati ata siku moja.
 
Mashauri ya ndoa na talaka 1,358 yamefunguliwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke (IJC), Dar es Salaam katika kipindi cha kuanzia Novemba 2021 hadi Julai, 2022.

Idadi hiyo ni sawa na mashauri 220 yanayofunguliwa kila mwezi kituoni hapo, hali inayoonyesha kuyumba kwa taasisi nyeti ya ndoa, hasa mkoani Dar es Salaam.

Mashauri hayo ni miongoni mwa mashauri 4,267 yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, kati ya hayo 2,911 yakihusu mirathi.

Hata hivyo, kituo hicho kimefanikiwa kunusuru ndoa 29 kati ya 80, ambazo wanandoa walifikishana hapo kwa ajili ya kuzivunja.

Naibu Msajili wa IJC, Mary Moyo amesema mashauri yanayoongoza kufunguliwa katika kituo hicho ni ya mirathi ambayo ni 2,911, sawa na asilimia 62 ya mashauri yote, ikifuatiwa na mashauri 1,358 ya ndoa na talaka sawa na asilimia 38.

Kwa upande wa mashauri ya ndoa yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, Moyo alisema mashauri yanayoongoza ni ya talaka, wanandoa kuomba kutengana, mgawanyo wa mali baada ya ndoa kuvunjika, matunzo ya watoto na sehemu wanakotakiwa kuishi watoto baada ya wazazi wao kutengana.

Alisema kati ya mashauri 1,358 ya ndoa, mashauri 1,127 ndiyo yaliyosikilizwa na kutolewa maamuzi, huku mashauri 231 yakiwa bado hayajatolewa uamuzi.

“Takwimu hizi ni tangu kituo hiki kilipoanza kutoa huduma Novemba, 2021 hadi Julai 19, 2022 na wanaokuja kupata huduma katika kituo hiki wengi ni wanawake ambao wamekuwa wakifungua kesi za ndoa, talaka, malezi ya watoto na upande wa wajane wamekuwa wakifungua kesi za mirathi,” alisema Moyo.

Kuhusu mirathi, Moyo alisema tayari wasimamizi wa mirathi 2,376, sawa na asilimia 82 wameshateuliwa na mahakama hiyo kukusanya mali na madeni katika kipindi hicho.

Alieleza sababu kubwa ya kituo hicho kupokea kesi nyingi kwa kipindi kifupi ni kutokana na kituo hicho kuhudumia mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Tofauti na mahakama nyingine, kituo hicho kina ngazi tano za mahakama kwa pamoja, yaani Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, jambo ambalo limerahisisha watu kupata huduma kwa urahisi.

Chanzo: Mwananchi
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Wanaona uzushi nahisi
Usalitiwe left and right, matunzo hawapewi wanakomalia nini sasa

na ambao bado hawajaleta mashauri baadhi wanaishi basi tu wasogeze siku
usizungumzie matunzo,mbona bill gate kaachana na mkewe,kwani mkewe alikosa nini?
 
Mmh! Mimi nadhani hiyo ni nia njema, watu wengi wanaingia kwenye ndoa uninformed, ukijua unaingia kwenye changamoto unajiandaa kushughulika nazo.
Kwa upande mmoja ukitazama ni hivyo ila kwa upande mwingine inakatisha tamaa, mtu anaona ni kama ndoa haina thamani tena maana watu wanaingia na kutoka ovyo, lakini pia mtu anaweza kuingiwa na uwoga kuwa huko kwenye ndoa kuna nini hadi watu wanatoka spidi wakati waliingia kwa hiari
 
Wanaona uzushi nahisi
Usalitiwe left and right, matunzo hawapewi wanakomalia nini sasa

na ambao bado hawajaleta mashauri baadhi wanaishi basi tu wasogeze siku
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
hauta nipa misukosuko kama hao wengine wanayopeana? Maana bwana alinipa maono kuwa nitanenepea ndan ya ndoa ila hakuniambia ni nan ataifanya hio kaz
🤣niambie Unataka mwanamke wako utakae mwoa Unataka akufanyie nn....Ili ndo unenepe ivo
 
hauta nipa misukosuko kama hao wengine wanayopeana? Maana bwana alinipa maono kuwa nitanenepea ndan ya ndoa ila hakuniambia ni nan ataifanya hio kaz
Ila ndoa sikuhizi ni moto,ubahatike tu
 
Mpumbavu pekee ubomoa ndoa yake kwa kupaste aonacho.
Mwanzilishi wa ndoa alitengeneza mfumo, sheria na kanuni Ili ndoa idumu kuanzia uchaguzi wa mtu sahihi, jinsi ya kuishi pamoja, malezi ya watoto, nk. Sema tu binadamu tuna ubinafsi ndio upelekea talaka.
Huo ubinafsi ndiyo hizo wanazoita haki hao wabeba mimba
 
Washamalizana huko ila sijui kanda ya ziwa Kuna shetani gani

Screenshot_20220803-144652.png
 
🤣niambie Unataka mwanamke wako utakae mwoa Unataka akufanyie nn....Ili ndo unenepe ivo
ahakikishe Nina aman yote inayotakiwa mtu awenayo (aman ya moyo, ya akili, ya wakati wa sex nk)
2. mapocho pocho yakutosha ( ni pamuhim sana tena ahakikishe Kila mda Nina kula)
3. Heshima

Mengne tutavumiliana au atayakuta huko huko kwenye ndoa
 
Ila ndoa sikuhizi ni moto,ubahatike tu
shida watu wamesahau na wengine wameacha kabsa misingi ya ndoa iliyowekwa na muasisi wake na kujiendea tu wengine wanaingia kwenye ndoa Kwa kutafta attention za watu siku ya harus anasahau kuwa kuna maisha baada ya kuvua shera
 
ahakikishe Nina aman yote inayotakiwa mtu awenayo (aman ya moyo, ya akili, ya wakati wa sex nk)
2. mapocho pocho yakutosha ( ni pamuhim sana tena ahakikishe Kila mda Nina kula)
3. Heshima

Mengne tutavumiliana au atayakuta huko huko kwenye ndoa
Yote hayatonishinda,ila 2 sasa....utakuwa unaacha hela ya kutosha pia🤦?
 
shida watu wamesahau na wengine wameacha kabsa misingi ya ndoa iliyowekwa na muasisi wake na kujiendea tu wengine wanaingia kwenye ndoa Kwa kutafta attention za watu siku ya harus anasahau kuwa kuna maisha baada ya kuvua shera
Hakika ndicho chatuponza
 
Back
Top Bottom