'Khalid na Philemon walipendana' - Saida Karoli alimaanisha nini hapa?

Hakunaga ushoga na wala hautakujaga kutokea ushoga uhayani.
 
Alihojiwa akasema alimaamisha Philomena,,,sasa sijui philimon na Philomena vinafananaje?? Nasisi tungejuaje anamaanisha philomena
Wahaya ni watu wanaoharibu Sana majina
Kule uhayani mambo yapo hiv
Clementina- wao huita keleme
 
sisi wahaya kiswahili ni chenga sana alimanisha hawa washikaji walikuwa wana saidiana sana kwa shida na raha
 
sisi wahaya kiswahili ni chenga sana alimanisha hawa washikaji walikuwa wana saidiana sana kwa shida na raha
Ha ha sasa mbona naambiwa alipohojiwa pale Mawingu anasema alimaanisha Filomena
 
Inaonekana huko Kwao ushoga ulianza zamani sana.
 
Inaonekana huko Kwao ushoga ulianza zamani sana.
Hakujawahi na haitakuja kutokea mhaya Shoga.

Alimaanisha filomena na ndo alivyosema
ingawa uhayani kuna ule urafiki mpaka wa kuchangiana damu.na ni Kati ya marafiki WA kiume na ikitokea wakazaa watoto urafiki huo huendelezwa na watoto wengine huwa ndugu kabisa .kuna koo ziko hivyo uhayani.
 

...Chambua kama karanga mama, chambua kama karangaaaaa....
... Halidi na Filimoni walipendana, mapenzi yao yakadumu....
...wenye wivu wajinyinge mama, wenyewe wivu wajinyongeeeee...
Wenye wivu wajinyonge sana, wenye wivu wajinyongeeee....

My Take
Naupenda snaa mziki wa Saida, kwangu mimi ndio mwanamziki wa kike mwenye sauti inayonivutia zaidi. Kwangu mimi Saida ni zaidi ya Zuchu na Nandy,kile ni kipaji halisi.

Shida yangu ni kujua hasa ujumbe wake kuhusu Halidi na File. Alitaka kutuambia nini dada Saida. Walipendania nini hawa ndugu wawili tena wa kiume, kiasi cha kuwataka wenye wivu wajinyonge?
 
Zamani ilikua kawaida kusema nampenda zamoyoni mogella,kizota,pepe kale,siku hizi ukisema nampenda Aziz ki watu wanakuangalia vibaya..yaani neno 'penda' linahusishwa na ngono
 
Alimaanisha Khalid na Philomena labda....


Lakin kwenye video huoni ya kuwa vijana wawili walikuwa wanastruggle kuwapproach wasichana wawili waliokuwa wanatoka mtoni?....

Lakin huu wimbo unamuongelea Maria Salome na yaliyomkuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…