Kibanda cha Bati kwenye kaburi la Hayati Magufuli kinatia aibu

Kibanda cha Bati kwenye kaburi la Hayati Magufuli kinatia aibu

Sisi tupo njiani kwenda kuhiji kwenye kaburi la MWANA AFRIKA wa kweli,JPM.
Huyu mtu hakuwa mtu wa kawaida sana. Ukitaka kujua kuwa JPM si wa kawaida, subiri uchaguzi mkuu 2025. Gombea kwenye uchaguzi huo halafu umkashfu hayati JPM kwenye mikutano ya Kampeni. Majibu utakayoyapata kwenye sanduku la kura yatakuwa ni somo tosha kukujulisha kuwa JPM hakuwa mtu wa kawaida.
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali. Hivi mmeshindwa kujenga kibanda chenye Hadhi kulizunguka kaburi la Magufuli?

Kwakweli japo sikufurahishwa na matendo mengi ya Marehemu magufuli lakini kumtendea haya sijafurahia.

Wahusika mjitathmini.

View attachment 1784695
View attachment 1784754
Mama Jenet yuko wapi nyumba ya mzee imechakaa hivi kwa muda mfupi, hebu semeni huyu mama kama kuna mahali mliwahi kumuona
 
Mzee wa miundombinu huyo! Na kweli wasukumu ni wasukuma tu manake siku ile ya mazishi mwili haukushushwa kaburini, watu walidanganywa na uchukuaji wa picha ulikuwa strictly directed kutoonesha ukweli wa mambo. Mtu alizikwa baadaye sana kwa staili ya kisukuma na mambo mengine mengi ya kienyeji.
Kuna mila za kichawii zilikuwa zinafanyika siku ya mazishi.
 
Tatizo hizi kazi wanapeana. Halafu wanaopewa ni washamba. Mtu hana hata exposure unategemea nini.

Wangepewa professionals kufanya kazi yya kuremba kaburi hapo pahala pangeng'aa na pangeweza kuwa kivutio cha watu kupita kuhiji.
 
Bado kuna maua ya kumbukumbu kwa familia yake. Ingawa wewe ulifurahia kufa kwake elewa pia kuwa familia yake ilihuzunika.
Na wewe ni mwanafamilia... Pole sana.

Toeni hayo mabati, mjengeeni jengo la hadhi yake... kama kweli mlimpenda kihivyo.
 
Licha ya tofauti zangu na mzee marehem, kiukweli hapo walichofanya sio poa kabisa.Huyo alikuwa ni Rais wa nchi hamuwezikumuwekea banda la mbuzi hilo.
Labda kama familia yake ndio wamefanya kwakutokujua
 
Huyu mzalendo hata asingependa kaburi lake mlijengee vile kwa pesa nyingi maana yeye alikuwa anapenda kubana matumizi ya fedha za umma hata sielewi kwa nini MATAGA mnalazimisha kutumia fedha za umma.
 
Wameachia Serikali...
Hii nchi ina watu wa ajab sana

Mtu ukipata previledge vitu vyote ni serikali, hata sedan serikal ndio unanunua... huku shule za kata hata haijawah kuona spatula
Exactly, ina maana vijana wake hawawezi kufanya lolote aisee?
 
Back
Top Bottom