Kibanda cha Bati kwenye kaburi la Hayati Magufuli kinatia aibu

Kibanda cha Bati kwenye kaburi la Hayati Magufuli kinatia aibu

Mjengo unaloendelea nyuma ya hilo bati ukiisha mtasaga meno.ni swala la muda tu. Tumeweka kwa wajili ya waombolezaji wanaokuja kila siku, huku ujenzi ukiendelea.

Mtulie sindano itawaangia vizuri njengo ukiisha
 
Yes mkuu thanks kwa kuona hilo.

Hakika unaweza kugundua akili ya mtu kwa kuhoji au anachoandika, maana kwa akili ya haraka haraka hawa vijana wetu wa (new age) wangejiuliza sehemu mbalimbali kukiwa wamezungusha mabati buwa ni nini kinaendelea humo?.

Jibu lingetosha kujua ahaa kuna ujenzi unafanyika, sasa kwa hapa imekuwa nongwa kwa familia na marehemu pombe.
hapo hicho kibanda ujenzi unaendelea ndani ya kaburi au??? siku 40 sio za kushindwa kuchagua dizain ya kajumba kazuri cha kujengea kaburi la rais ishu ni kwamba no body cares at all
 
Kuna taratibu za kujengea makaburi.... na muda wa kujengewa hapo bado

Muda ukifika watajenga na usiache kuongeza picha
hapo sio kujengea kaburi ni kijumba cha kuzunguka kaburi...
 
Je

Fikiria vema utaelewa maana ya swali langu... (aidha ikiwa tu mtu anashindwa kuzuru kaburi la mpendwa wake ambae anataka aaminishe dunia alikuwa akimpenda sana... je anawezaje kuitetea "legacy" aiimbayo kila uchao?"
Kama ulitaka hiko kibanda kisionekane kwenye mitandao basi mngekataza VP alipotembelea asipige picha .
 
LOoooh, kuna majibu ambayo hayategemewi kabisa!

Siyo swala la kibanda pekee. kwa kiongozi aliyeliliwa vile, pamoja na mabaya yanayomhusu; lakini mwonekano katika eneo hilo ulivyo kwa sasa ni wa kusikitisha.

Hata hayo maua yaliyokaukiana humo hayastahili kabisa kuwemo humo.

Hata ndugu tu, wangeweza kujitolea kadri wawezavyo kulipa mwonekano wa hadhi kaburi hilo.

Hii inatoa tafsiri pana sana kuhusu maisha ya Magufuli.
Yaelekea familia pia imefurahia bwana yule kwendazake...
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali. Hivi mmeshindwa kujenga kibanda chenye Hadhi kulizunguka kaburi la Magufuli?

Kwakweli japo sikufurahishwa na matendo mengi ya Marehemu magufuli lakini kumtendea haya sijafurahia.

Wahusika mjitathmini.

View attachment 1784695
View attachment 1784754
Ninavyoelewa ni kuwa eneo line sasa hivi lina mvua nyingi sana kwa hiyo sishangai kama walijenga hilo banda kuwa temporarly shelter hadi mmvua zitakapokiwsha
 
Back
Top Bottom