Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Waanzilishi wa siasa za uadui hao hao wanaliliaji wa siasa za amani. Aiseee wanasiasa wanafiki
Hao wanaccm wa siasa za ugoko kwa ugoko wameamua kubadilika. Na sisi ndio kilio na shauku yetu ya toka zamani
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Tunajua chanzo cha wasi wasi wako ni kutonana na maumivu makubwa awamu ya tano ilisababisha.
 
Mbowe alitoa machozi pale kanisani, Jela sio mchezo. Ni bora wakatulia waachane na suala la katiba na maandamano, then 2025 watapewa viti 10 vya ubunge na mamilioni ya ruzuku kama ilivyokua 2010 hadi 2020.

Wanaozea jela alafu sisi makamanda uchwara hata kuandamana tunaogopa.
 
CHAWA wapo kila chama kilichopewa usajili pale ofisi ya msajili. Waliokuwa wanaimba nyimbo za hamasa kila siku Mbowe alipokuwa akipelekwa mahakamani, akija kupata cheo kikubwa hawatakuwa CHAWA kweli!?.
 
CHAWA wapo kila chama kilichopewa usajili pale ofisi ya msajili. Waliokuwa wanaimba nyimbo za hamasa kila siku Mbowe alipokuwa akipelekwa mahakamani, akija kupata cheo kikubwa hawatakuwa CHAWA kweli!?.
Ule sio uchwawa. Ule ni upambanaji kwa ajili ya haki.

Chawa ni mlamba viatu kwa ajili ya kujipatia chochote.
 
Mkuu kama ulizoea siasa za kutukana wapinzani tafuta kazi nyingine.

Iam Sorry to say that lakini ndio mwelekeo wa Mama Samia
 
Katiba mpya ni pigo kwa ccm hawako tayari kwa hilo kwa gharama yoyote

Suala msumari kwa chadema kwa sasa ni katiba mpya sasa ukiangalia hapo usalama na amani vitatoka wapi
 
Hakina mbowe ndio matapeli wa siasa za nchi hii,nakumbuka kipindi cha dkt Slaa wananchi tulikuwa tunajitokeza kufanya chochote tulichokuwa tukielezwa na viongozi wa Chadema,kila siku tulikuwa tukitoka kwenda kwenye maandamano na mikutano yao, iwe mvua au jua tulikuwa tuko nao, mpaka akina Mbowe wakaota kiburi,Moto wa Chadema ulikuja kuzimwa na Mbowe na Lissu kwa tamaa zao za kipumbavu,eti wanakwenda ikuru kugawana vyeo,wakamleta mtu ambaye walipatia mtaji wa kisiasa kwa kumwita fisadi,gafra huyo aliyeitwa fisadi eti hakapewa nafasi ya kugombea urais,wakamwacha aliyekuwa njenzi wa chama,tangu hapo wenye akili zao tuliliona anguko la Chadema tukatukanwa, Sasahivi Chadema inakwenda kuwa kama tlp ya mrema,eti mnakwenda kufanya siasa za usitarabu 🤣🤣Sema Mbowe ameshindwa siasa, Sasahivi inabidi hawapigie magoti CCM waweze kumfikilia kumpatia angarau viti kama viwili vya ubunge ili maisha yaendelee,kama alivyokuwa akifanya mrema, CCM hauwezi kufanya siasa za usitarabu ukawaweza.Niko tayari kwa matusi
 
kwamba tunaweza siasa za kistaarabu lakini za Maandamano hatuwezi.
Kama hatujitokezi kwenye maandamano maana yake nini ipi kama sio hatuziwezi? na ajabu zaidi, hata hizo unazoita za kistaarabu nazo wapo wasiozitaka.

Kiongozi akifanya hata hizo anatiliwa shaka, sijui kuna aina gani nyingine ya siasa iliyobaki itakayowafaa watu wa sampuli hii.
 
Mkuu kama ulizoea siasa za kutukana wapinzani tafuta kazi nyingine.

Iam Sorry to say that lakini ndio mwelekeo wa Mama Samia
Haha kuna upinzani nchi hii? Acha mzaha mkuu. Sasa agenda ya upinzani ni nini? Katiba mpya? Uhuru wa maoni? Tume huru Au nini?
Sasa mbowe atahubiri nini? Kilichobaki watakua wamamtukana marehemu ili kumfurahisha mama, kujikomba ili kidogo wafikiriwe ruzuku.
 
Wakati wa Dr. Slaa nakumbuka maandamano pekee yaliyofanyika yalikuwa Arusha ndipo Josephine mke wa Slaa alipoumizwa na polisi.

Nipe mfano wa mikoa mingine iliyowahi kufanya maandamano ya Chadema hapa Tanzania kama unavyodai yalikuwa yakifanyika kila siku.

Mwisho unapodai Lissu na Mbowe waliiuza Chadema licha ya madhila yote waliyopitia wakati wa awamu ya tano (Lissu kupigwa risasi, Mbowe kufungwa na kuharibiwa assets zake) nipe ushahidi wa kuuzwa huko.
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli itawatafuna milele Mbowe na Lisu.

Hata mwaka haujaisha saccos yao inakiona cha moto
Na wala hakauna laaana watakayoipata yá kushangilia kifo chá magufuli.

Aliyepata laana ni yeye magufuli aliyekufuru kwa kusema aende akachaguliwe ili aongoze malaika hii ni laana tosha iliyomkumba.
 
Kwanini usichukue wewe nafasi ya Mbowe? Uwe kiongozi wa upinzani!!
 
Wakati wa Slaa Chadema walifanya oppression nyingi na zikafaniwa na kuwa na mwitikio wa nyomi la watu, mpaka Chadema ikawa tishio kwa watawala ccm,akina Slaa walikuwa wakito tamko linajadiwa nchi mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…