Ila zamani watu walikuwa hawana stress. Just imagine nyimbo kama kamanda, watu walicheza tena kwa kuenjoy kabisa.
Nakumbuka nikiwa tamsala mdogo wake na Ay, magdalena alikuwa ndio dancer wa huo wimbo😄
Hahaha!
Hili Huwa nikikutana na Jamaa zangu Huwa tunacheka na kufurahi kuhusu nyimbo za nyuma bongofleva!
Kisha tunaingia kwenye mjadala mkali,kuhusu Nini..??? Kuhusu Watu katika club au sherehe kucheza nyimbo za huzuni au maskitiko!!
Je,ulikuwa ni ukosefu wa nyimbo za amsha-amsha clubbenga au maisha hayakuwa na stress..???!
Afande sele akihojiwa na Baruani muhuza anasema Wasanii enzi zao walifanya kazi kubwa na yaziada kuwakimbiza/Kuwaondoa wacongo,bongo(Congo music's)..(Defao,Kofii, Extra music's,Wenge Musica,Yondo ssta na nk).
Watu kucheza Nyimbo kama kamanda,Inaniuma-Juma nature ,Ugali,Waaguzi-Wagosi wa kaya, nk...,katika sherehe au clubs...
Sababu zipo nyingi ilamojawapo pia na kubwa ni Jamii ilikuwa Bado Sana Sana katika vifungo vizito vya Mafundisho,kanuni na taratibu za Dini za kigeni(Ukristo na Uislamu) na Vifungo vizito pia vya Ujamaa/Socialism ya Jk Nyerere! ,Ubepari Bado ulikuwa haujapenya Sana!
Hivyo utunzi,utungaji wa Mashariki/Nyimbo viliaangukia katika vifungo au Mambo hayo Ujamaa na Dini,
Mfano:Sikiliza vizuri Mashairi ya wimbo wa kamanda,yamechota mawazo/Maoni na mtazamo wa kifo uliochakatwa na kuhubiriwa na Dini bila kusahau Ujamaa !
Hivyo msanii/MTU kuimba nyimbo za kushangweka na Bata,lazima ujitafakari marambili au ujilipue kama mpanzi,unapanda mbegu.
Nyimbo za Kujirusha na clubbenga zilikuwepo chache Sana Tena zilizohit Nchi nzima ndio zilikuwa chache mno. Mfano Pamba nyepesi-Insepcta haroun Babu,Mikasi-Ngwair,Jirushe-Ferouz ft jaymo,T-shirt na Jeans,Nicheki-Oten Nk...