Sisi wa dansi hamna nyimbo kama "MTU PESA" ya mwana Masanja.
Rafiki yangu marehemu aliimba sana hapo.
Nikamkuta siku Sinza Meeda Pub aisee machozi yalinitoka.
Hali Mbaya.
Tulikua hatujaonana km miaka 15 hivi.
Hapo alikua jukwaa la extra bongo ya enzi hizo
Aliponiona akatupa mike tukumbatiane.
"Kaka ulikua wapi"?
ndio lilikua swali lake
Dah nikamtunza chochote nilichokuwa nacho nikaondoka.
Kuna Nyimbo nyingi sana mwana Masanja alizifanyia haki,
Kisa cha Mpemba etc.
T.o.t nako alimaliza sana.
Dah kuskia jamaa kafariki nilisikitika sana.
Ila yote mipango ya mwenyezi tu.