Kibongo bongo nyimbo ya Daz Nundaz “Kamanda” ni nyimbo ambayo ukiiskia inaweza kukutoa chozi

Kibongo bongo nyimbo ya Daz Nundaz “Kamanda” ni nyimbo ambayo ukiiskia inaweza kukutoa chozi

Madee- kazi yake mola [emoji22]

Hii ngoma wakati inatoka ilipishana kidogona msiba wa auntie yangu alie nilea, sijawah kuizoea hii nyimbo, zaman nilikuwa nikiisikia lazima nilie ila siku izi nikiisikia naweza kuwa off mood siku nzima
 
kazi yake mola, haina makosa
kazi yake mola, haina makosa
anafanya atakalo, anafanya awezalo
kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo
kazi yake mola, haina makosa
kazi yake mola, haina makosa
anafanya atakalo, anafanya awezalo
kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo
umekuta dunia imeandaliwa
na we bila hiyana si ukazaliwa
umekuta wasafiri
waliotutoka kwaheri
kimwili hauko nasi
kiroho tupo nawe
upo kwenye kina kati mbao juu mawe
mchana na usiku tunaomba tuwe nawe
haiwezi kuwa sawa
ugonjwa unatibika, mauti hayana dawa
kwa heri mwanahawa, kizima huaribika
kufa na kupotea
mchana na usiku dua tunakuombea
ulale mahali pema huku unatungojea
njia yetu ni moja ipo siku utatupokea
salamu wasalimie wote utao wakuta
wambie babu tale machozi keshafuta
na keshalala matanga
tangu enzi zile alipoondoka kichanga
 
Angekuwepo rafiki nisingewaza rafiki kipenzi ninaye mpenda

Angekuwepo rafiki nisingewaza rafiki kipenzi ninaye mpenda


Ayupo Tena Dunia swaiba niliye mpenda kwa kumoyo Swaiba

Ayupo Tena Dunia swaiba niliye mpenda kwa kumoyo Swaiba

Na nukuu amaneno yake busara zake alikuwa mtu wa watu uyu mtu

Nuru aina mwanga mbele giza rafiki niliye mpenda amenitoka

Nilikuwa na marafiki sikatai lkn rafiki wa kwel bye bye

Akufa kwa ngoma donsalale siku yake ilisha fika pema alale

Uzuni isiyo kiwisha moyoni nashika tama sioni

Ananijia ndotoni swahiba ananiambia nisikonde

Rest in peace Mama
Mkuu huu wimbo unaitwaje? Na umeimbwa na nani? Naukumbuka kwa mbali sana,kitambo aisee,maneno yako yamefanya niukumbuke ila sikumbuki uliimbwa na nani.
 
Masela nawaaga tena sirudi,
Nasindikizwa na marashi ya ubani na udi
Yowe la uchungu litasikika
Pale roho yangu itapokua inatoka
Vazi langu sanda nitakua nimevikwa
Nipo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa

Mauti pindi yataponikabili
Ni nani atakaeziba pengo hili
Uhai tamati mzunguko wa damu umesimama
Kama jahazi tayari lim......

Naskia jamaa waliimba songi hili kipindi wako sekondari kidato cha kwanza kama sikosei... ona tofauti ya vijana wq zamani na sasa ...
 
Huu uzi unanikumbusha mbali sana,kweli miaka inaenda.

Mandonjo na Domokaya,hawa jamaa licha ya kuburudisha tu bali nyimbo zao zilikua ni elimu tosha.
 
Dah! Hit za miaka hiyo!
Kwa sasa hakuna wasanii, kuna wahuni na wapiga kelele.
Tumezeeka, na wasanii wetu hawatungi nyimbo za rika letu.
 
Ila zamani watu walikuwa hawana stress. Just imagine nyimbo kama kamanda, watu walicheza tena kwa kuenjoy kabisa.
Nakumbuka nikiwa tamsala mdogo wake na Ay, magdalena alikuwa ndio dancer wa huo wimbo😄
 
Back
Top Bottom