Kibongo bongo nyimbo ya Daz Nundaz “Kamanda” ni nyimbo ambayo ukiiskia inaweza kukutoa chozi

Kibongo bongo nyimbo ya Daz Nundaz “Kamanda” ni nyimbo ambayo ukiiskia inaweza kukutoa chozi

Huu ni ukweli wakuu hii ni nyimbo ambayo hata ukiiskia tu hisia za kulia inakujia hii nyimbo ni nyimbo ambayo haitowahi kutokea kwenye muziki wa bongo flava [emoji119]🥲 hakuna na haitowahi kutokea nyimbo ya kuhuzunisha kama hii

Labda Kama Uko msibani,sisi tunacheza kabisaaaa
 
1.Kamanda
2.Barua
3.Maji ya shingo
4.Rafiki-Jeby
5.Tutakukumbuka -GK

Dah zamani kulikua na ngoma bwana yaani huwezi peleka mbele ngoma yoyote ikipigwa hit tupu.
Hizi ndio Bongo fleva nazoweza kusikiliza. Hata nikibadili pC ninahama nazo
 
Sisi wa dansi hamna nyimbo kama "MTU PESA" ya mwana Masanja.
Rafiki yangu marehemu aliimba sana hapo.
Nikamkuta siku Sinza Meeda Pub aisee machozi yalinitoka.
Hali Mbaya.
Tulikua hatujaonana km miaka 15 hivi.
Hapo alikua jukwaa la extra bongo ya enzi hizo
Aliponiona akatupa mike tukumbatiane.
"Kaka ulikua wapi"?
ndio lilikua swali lake
Dah nikamtunza chochote nilichokuwa nacho nikaondoka.
Kuna Nyimbo nyingi sana mwana Masanja alizifanyia haki,
Kisa cha Mpemba etc.
T.o.t nako alimaliza sana.
Dah kuskia jamaa kafariki nilisikitika sana.
Ila yote mipango ya mwenyezi tu.
 
Mziki ulikuwa zamani

Ukisikia hata interviews za wasanii wa zamani wana stori sana,interview zao
Zinavutia kuwasikiliza
Mziki sshv matukio kik nyingi mzkki kdg

Ova
 
Achwa alafu kasikie ile nyimbo kuachwa ya mapacha wa tatu. Usipolia,, nasema usipolia
 
Huu ni ukweli wakuu hii ni nyimbo ambayo hata ukiiskia tu hisia za kulia inakujia hii nyimbo ni nyimbo ambayo haitowahi kutokea kwenye muziki wa bongo flava 🙌🥲 hakuna na haitowahi kutokea nyimbo ya kuhuzunisha kama hii
Aslay alijitahidi sana kwenye Magufuli Bye. Haikuwa sample ya nyimbo zingine ila imebeba huzuni kama ukiisikiliza kwa utulivu.

Nyingine ni Mama Neema ya 20% ile nyimbo sio poa, hasa mtu ukiwa na mama kijacho ndani lazima utafakari jambo.
 
Aslay alijitahidi sana kwenye Magufuli Bye. Haikuwa sample ya nyimbo zingine ila imebeba huzuni kama ukiisikiliza kwa utulivu.

Nyingine ni Mama Neema ya 20% ile nyimbo sio poa, hasa mtu ukiwa na mama kijacho ndani lazima utafakari jambo.
kbsa naungana na ww hapo kwa twenty peeer asilimaireee
 
Masela nawaaga tena sirudi,
Nasindikizwa na marashi ya ubani na udi
Yowe la uchungu litasikika
Pale roho yangu itapokua inatoka
Vazi langu sanda nitakua nimevikwa
Nipo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa

Mauti pindi yataponikabili
Ni nani atakaeziba pengo hili
Uhai tamati mzunguko wa damu umesimama
Kama jahazi tayari lim......

Naskia jamaa waliimba songi hili kipindi wako sekondari kidato cha kwanza kama sikosei... ona tofauti ya vijana wq zamani na sasa ...
Makini sana.
 
Back
Top Bottom