heading;
...wallaaaaaahi billaaaaah,....nimeisoma hiyo article mara tatu sijaona wapi padri kasema hakuuona mwili wa balali!
Wait !!! Inamaana kila uliposoma wewe ni kuwa Padire ameuona mwili wa Balali ?
samahani maelezo ya mahojiano na Padri yamechelewa kidogo.
Bali Padri kwa kinywa chake amekiri hakuona mwili wa Balali.
Simu ya kanisa ni : 202 785 0982.
Mkuu,
Inaelekea hujui kusoma between the lines. Mimi niliisoma hii habari na moja kwa moja nilijua padre hakuona maiti..
KAda unaamini balali kafa??
Naomba kuuliza, hivi mapadre wote wanavyosalisha misa za mazishi wanapaswa kuona mwili, je wanalazimika kisheria za kanisa? Au tu kwa sababu imekuwa Balali?
Kama ni kweli alizikwa kikatoliki kama inavyodaiwa, kuna hatua ambapo padri huwa anamfunua uso maiti na kumnyunyizia "maji ya baraka". Sijui kama padri huyo alikwepa hatua hiyo? Inapaswa aulizwe, wenye nafasi huko tusaidieni hiyo kazi. Hii kitu kama inaisha vile lakini inaibuka upya mara kwa mara!
Mkuu FMES,
Basi tueleze huyo balozi Sefue aliona maiti wapi?
Mimi nilikuwa najua kwa asilimia 100 kwamba kwenye misa hakukuwa na kuona maiti. Sijui ndugu yangu FMES alipata wapi hiyo ya kusema balozi aliona maiti?
Pia FMES data zako zinasema Ballali alikufa jumapili tarehe 18, padre anasema 16.
Data za Jasusi zinasema alikufa ghafla, padre anasema aliumwa kwa muda mrefu.
Hapo tukubali tu tumefungwa goli la kisigino na kwasababu serikali nayo haimtafuti basi huko aliko ataendelea kufaidi pesa za wizi.
Ila wengine tutaendelea kuirudisha hii habari mpaka kieleweke.
Mkuu Mtanzania,
Na wenine heshima mbele, mimi kama Mkristo safi hii ishu nimeinawa mikono, ninaomba tena kusema ninchojua na kilichonifanya ninamini na bado ninaamini kwa 100% kuwa Balali amefariki, lakini pia ninaheshimu sana mawazo ya wale wanaoamini kuwa yupo:-
Nina uhakika kuwa alifariki Jumapili nyumbani kwake, alishughulikiwa in one way or another katika hospitali ya George Washington University Hospital lakini sio kwa jina la Balali, na hili jina la Siriani mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kulitoa, na mpaka jina la kanisa la huyu padri mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kuyatoa, sasa ninashukuru kuwa kuna waliofuatilia kama nilivyoomba kule nyuma,
Ninaamini kuwa Balozi Sefue aliuona mwili, ndio akamuarifu rais na Membe, wakuu mimi as a Christian huu ni ushaidi tosha mbele ya Mungu wangu kuhusu kwa nini ninaamini kuwa amefariki, na ninaomba ninawe mikono hapa, lakini kwa yoyote anayetaka msaada zaidi nitampa kama nilivyowapa magazeti, katika kufanya uchunguzi zaidi, ila mimi dini yangu na Mungu wangu inanikataza kuendelea zaidi ya hapa nilipofikia na uchunguzi,
Lakini ninazisoma lines in the betweeen kwa makini sana, na ninawatakia heri wanaoendelea lakini akama kawa sina tatizo kutoa msaada kwa walio serious, pia nitoe respect kwa Majira na wengineo kwa msimamo imara wa kutoyumbishwa, that is waht we need kwa taifa letu.
Ahsante Wakuu!
Mkuu serikalini kuna protocol sio kwamba unaongea tu, hii ni very sensitive ishu ambayo mwenye haki ya kuongea na public kwa sasa ni waziri wa nje Membe au rais tu, kwa hiyo ndio maana Sefue hajasema na hawezi sema kitu kwa public!
Mkuu mimi ninaomba kunawa mikono, labda wanaojua vizuri zaidi waseme.
Ahsante Mkuu!