Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Itakuwa vipi kamati ya EPA itakapoleta taarifa ambayo kila jambo anatakiwa athibitishe Ballali kama vile nani alimwndikia vimemo vya akasaini.
Au walete taarifa kuwa yale ni makampuni ya Ballali na Ditto na kwa sababu wameshakufa no Mo MONEY

Hoja yako nzuri kweli. Lakini sidhani kama Balali ndio alikuwa kila kitu ndani ya BOT. I mean, haiwezekani kwamba yeye ndio alikuwa mhasibu, karani etc. Kwahiyo katika kuidhinisha malipo haya ya EPA, kuna watu wengi wenye information. Mimi nimekiri kwamba Balali huenda ndio alikuwa shahidi mkuu, lakini naamini kabisa wako mashahidi wengine kwenye hili.
 
Kijiwe kitafungwa kwa kuandika kwamba aliyemuua Ballali ni Rostam Aziz?

Gazeti linaweza kufungiwa lakini sio JF. Ukifungia JF leo, zitakuja zingine 20.

Mimi siamini hii habari ya sumu kwamba ni kweli. Wewe utalishwa sumu, ukimbilie USA, ukae miezi tisa, hakuna hata daktari mmoja ambaye anaweza kusimama na kusema wazi kwamba umelishwa sumu?

Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?

Hili suala la sumu mimi nililipinga toka mwanzoni na sasa ndio natapata sababu kubwa za kulipinga. Sumu ilikuwa ni sababu ya Ballali kutoroka TZ na kupotelea kimoja USA wakati wanaandaa mipango mingine.

Kuna kampeni kubwa ya kuwadanganya Watanzania juu ya hili jambo la Ballali.
 

Kikubwa zaidi ni pale wanaJF wanaposhadadia kuhusu kunyweshwa sumu huku. Ukicheki huku ndani kuna threads kibao kuhusu kunyweshwa sumu kwa Balali. Tukiomba ushahidi tunaitwa critics!
 
Inaeleweka Mburushi kafanya kweli lakini alitumia aina gani ya sumu??????
 


Mkuu Mtanzania
Mtu kulishwa sumu kwa kiwango cha Balali ama mimi na wewe ni daktari anaweza kujua na ndugu zake ama zako wa karibu na wakiamua kusema watasema na wakiamua kuendelea kuuguza ni uamuzi wao .Hili liwe wazi maana mwisho kila kitu kitakuja nje .


NO JF haiwezi kufungwa na yeyote acheni hisia za kuwapa kichwa kwamba wanaweza maana hii nis sauti ya Umma na kufunga hiki ni kufungua kingine na kingine .Kwanza wanafungia wapi ? Hii haiko Brela .
 
****Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?**
SUMU ILIOMUUA """KOLIMBA""DODOMA NA ""MTOTO WA MALECELA"" NDIO ILIOMUUA BALALI ...ILA YA KOLIMBA ILIONGEZWA NGUVU ZAIDI
MTANZANIA NATUMAINI UKIFWATILIA UKO UNAWEZA KUTULETEA CONTENTS ZA HIYO SUMU....NA KUWEZA KUJADILIWA....LABDA OMBI LANGU KWA WALE WANACHAMA WA CCM MTAKAOITWA DODOMA HALI MKIJUA ZALI LAWEZA KUWATOKEA NAOMBENI MSIKARIBIE MAUTI MNAYOIONA ""CCM SASA NI WAUAJI HALISI"""" NA WALA SI CHAMA TENA ...LAITI NYERERE ANGAJUA AMEACHA MAFISADI PEKEE ANGEWEZA KUSIKITIKA LAKINI KUMBE AMEACHA CCM YA WAUAJI WATUPU TENA KWA SUMU JAMANI NINGEPENDA KUJUA VYAMA VYENYE MREGO W MAUAJI KAMA CCM ..DUNIAN KOTE TUWENAVYO MAKINI
 
MKUU MTANZANIA

NATUMAINI WEYE ULIE KARIBU NAO UKO WAWEZA KUTUELIMISHA NINI CHA KUFANYA AMA WAZAZI WETU WENGINE CCM ..JE WAKIITWA WAJIBUJE KWA UONGOZI..AU WAKIMBILIE CCBRT KULAZWA NA KUTAFUTA VYETI KISA KUHIOJIWA ..KAZI IPO NYIE WATU HAWA WAUAJI HAMWUWAONI AU MPAKA WAJE KUGINGA NYUMBA KWA NYUMBA NA MAPANGA NDIPO MTAKAPOIOGOPA CCM..HAYA KAZI KWAO
 
Total crap. Story za vijiwe vya kahawa. Mkiombwa ushahidi mnakuwa wakali. I'm not buying that.
 



Hata wewe bado hujamtaja
 
Mimi nasema hivi watu wengine wanastahili hayo wanayoyapata. Balali hakuona umuhimu wa maisha yake ukilinganisha na siri ya kuwaficha hawa majambazi. Kama angelijua thamani ya maisha yake angetutajia majina na mtiriko mzima wa wizi pale BOT. Lakini kwa kuwa aliona ni bora a-sacrifice maisha yake ili kuendelea kuwatunzia siri majambazi wengine.Ndo haya yamemtokea. Sorry!! Ila ndo ukweli

Hivi kama Balali mwenyewe alishindwa kuweka hii ishu wazi tunategemea nini jipya kwa hao mnaosema wameachiwa siri yote. Kama ni ndugu ,Mke au Wakili watakachofanya ni kufaidika tu na hizo nyaraka kwa kuzifanyia blackmail.
 
Labda walimtishia familia yake so he has to sacrifice his life kwa ajili ya wale anaowapenda. Na alijua yeye lazima wamuue tu anyway
 


Mwanahalisi,

Watu hamfanyi mazoezi, mkikumbwa na ugonjwa wa moyo, mnasema mmepewa sumu?

Kolimba alikuwa kwenye pressure kubwa, ingelikuwa huku ULaya, kabla ya kwenda kwenye hicho kikao, angepimwa pressure kwanza na kuhakikisha yu salama kabisa. Lakini kwa TZ ndio kwanza mtu anaweka nyama choma kwanza.

Ye mtoto wa Malecela mimi siyajui vizuri kwahiyo wacha nisitoe comments zangu.

Sijui kwa US, lakini naamini hapa UK, kumlisha sumu mtu ni kosa, hata bila ya yeye kusema, hospitali wanaita polisi. Kama ni kweli alilishwa sumu, hospitali walikaa kimya basi mafisadi
wetu wametoa rushwa mpaka kwa madaktari wa USA, mpaka kwa polisi kwi kwi kwi!!! Haiwezekani.

Mimi swali langu ni lile lile, je alilazwa kwenye hospitali ipi? Huku nje kuna Freedom of Information na inatosha kuliandika vizuri swali, jibu utapewa tu.

Najua ndio maana familia yake hawataki kabisa kutaja hospitali, hawataki wafanye ujinga wa Kitinye.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema wazi kwamba serikali haihusiki na kifo cha Gavana wa zamani wa BoT, Daudi Ballali.... more to come
 

hapo ndio ninapo boreka na magazeti ya bongo, kichwa cha habari kinasema huyu, ukishanunua gazeti unabakia na vitendawili! hutamtaja kwa faida ya nani? hamna vyombo vya dola kumshitaki? tuseme hata madaktari wake hawakujua BALLALI amekuwa poisoned? acheni utani! na pesa za wananchi wanaonunua habari kumbe hamna kitu, sana sana speculations!

iwapo na sisi hatutalishwa sumu, kama hatajitaja, tutamtaja siku moja, katika kuweka vema historia ya mapambano dhidi ya ufisadi.

woga huo, woga nao!!!...inakufanya uwe a coward!



hearsays, speculations & more hearsays!!!... jamani kuna facts na fictions,... kama BALLALI alilishwa sumu, au kuuliwa kwa namna yeyote ile kwa nchi kama Marekani hiyo ingekuwa detected, na vyombo vyao vya dola wangeingilia kati, ndio maana wenzetu hao wana issue death certificate baada ya Autopsy/post mortem, huzikwi tu holela holela.

nitaendelea kuamini Daudi Ballali amefariki kutokana na maradhi hayo ya Cancer ya kichwa, lakini kifo chake kitaendelea kubakia simulizi kwa watanzania kwani amefariki na "siri nzito" ya zile pesa.

aaaah, maudhi matupu, sijui leo nimeamka vibaya (?)
 
Hata viongozi wetu wa Nchi wanatujua sisi wananchi wao wa Tanzania kuwa tuna sifa zipi ndiyo maana wanaweza kufanya wayafanyayo wakati wote watakapo;[tangu enzi za kifo cha Sokoine hadi Leo kifo cha Ballali]; sifa katika hizo tulizobalikiwa ni:
===== Kuongea sana na kusahau [ blah blah blah]
==== kubwa zaidi, ingawa tunawajua akina nani ni vinara wa mambo hayo basi sisi huishia kwenye wale weak points;
from the begining, Ballali was just a messenger on implementing his bosses orders; we know his bosses, why attacking ballali who was a mere messenger?
Kikwete and Mkapa are the ones to answer these questions we are throwing to Ballali!
 

Kwani bado wana uwezo wa kukifunga ,Fundi mitambo embu tuwekee maoni kuhusu hili la uwezo wa kukifunga jiwe hili ,ili kuondoa tisha tisha ambazo WaPemba wameishaziacha mbaali na sasa wanapita na kuimba "....Kura Maoni kikwete kampe mkeo...." Nimeona kideo ya mkutano wao huko Pemba wanasema nakuimba kama hawana akili uzuri.Ila nilipouliza nikaambiwa ndio makali ya siasa hayo lazima ukubali kukumbwa na kila jambo yakiwamo mauti.
Kwako fundi mitambo vipi hili jiwe la Jamii bado jamaa wanauwezo nalo ??

Nikiunganisha hiyo habari ya kitendawili basi Rostamu hatoki ncha zote zilizotajwa anaingia kichwa kichwa ,kama nimekosa basi inabidi sasa patolewe mji ili jamaa amtaje .
 
Mimi swali langu ni lile lile, je alilazwa kwenye hospitali ipi? Huku nje kuna Freedom of Information na inatosha kuliandika vizuri swali, jibu utapewa tu.

Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele, hapa umesema neno moja zito sana kuhusiana na this whole thing kuhusu Balali na kifo chake, sina tatizo na msimamo wako on the ishu ya kufa kwake, lakini at the same token ninajaribu ku-reason out,

Kwamba Balali, hajafa, familia yake imeamua ku-play a stint na kuwaaarifu dunia nzima kuwa amekufa, watu wa karibu na familia hiyo, ndugu wa karibu wote wa Balali na Muganda, wamekwenda huko DC, mmiliki wa Tanzania Daima ambaye naye ni ndugu wa karibu amefahamishwa kuhusu hicho kifo, serikali imefahamishwa kuhusu hicho kifo, dada yangu amefahamishwa na kualikwa kwenye msiba, juzi yamefanyika mazishi,

Sasa kama ninakuelewa vizuri, ni kwamba huu wote ni uongo uliotungwa na familia hiyo ya Balali, lakini Balali yupo na ataendelea kuishi baada ya all this?

kweli unaamini kuwa this makes a sense?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…