Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


Mkuu ES,

Uzuri wa kuishi kwingi ni kuona mengi. Tuna mifano mingi tu ya watu walio fake vifo, hivyo
ni ngumu kuamini mpaka kuwe na ushahidi wa kutosha.

Mimi swali langu ni lile lile, kafia kwenye hospitali ipi? Tukishajua hospitali, mengine tutachunguza wenyewe.
 
Hapa nilichokiaona watanzania inatakiwa tuombe radhi kwa familia ya balali.

Suala la muhimu ninaloliona ni hili , Unajua assume umekaa pale counter ya CRDB au NBC na una funguo za mahali pa kutunzia pesa. Wakaja majambazi wakaamulisha uwappe kila kilichoko benki. Ukatoa baadaye wakaondoka au wakaondoka na wewe.

Mwisho wa siku wakaamua kukumalizia. Je nani atakuwa reponsible kuhakikisha haki inatendeka. Je mwenye kosa ni yule aliyekuwa na ufunguo?

Je mambo yanahisha pale tu aliyekuwa na funguo anamalizwa. Mimi nilivyoona sakata hili ni Kwamba balali alitekwa, na majambazi wakati watanzania tukishangilia, baadaye majambazi yametoa hukumu.

Suala lililoko hapa let us see kilichoko mbele yetu. Mtunza fuunguo hayupo tena na sisi hatukuweza kuliona hili.

Tuwaombe watawala wajibu maswali mawili matatu.
Je Balali alipotekwa wao walikuwa wapi?

Je kwa nini hawakufatilia mapema kulikoni atekwe?

Je kwa nini mpaka sasa watekaji wa EPA bado ni kigugumizi.
 
ES ile DVD ulituahidi mbona hatuioni?

hivi how difficult is it kupost Video kwenye Youtube?
 
A bit of otherwise thinking.

Hivi hii habari ya balali unaweza kutengeneza movie kabisa kama 24 series.
Yaani kuanzia pale alipokuwa Shirika la fedha,akaitwa na bwana uwazi na ukweli,kisha akateuliwa kuwa gavana...

Jinsi alivyokuwa akiwasadia watu fulani fulani kuchota pesa,kisha akaingia kwenye kasha then ikasemekana kalishwa sumu..mara akapotea kwenye vyombo vya habari..then ikasemekana anaumwa....mpaka kifo chake.Inawezekana all this was a planning script. ambayo sasa imetimia.

Week endi njema.
 
Mkuu GT,

Naomba nikuombe radhi mkuu, shughuli zimenitinga sana, na ni jana usiku tu ndio nimemaliza kuziangalia vipande vyote vitano, havikuwa vinne kama nilivyosema mwanzoni, nisingeweka kitu ambacho sijakiona mwenye kwanza kwa sababu what if ndani kungekuwa na something else? Maana binamu yangu mmoja aliwahi kumpa baba yangu film akamsafishie u-China kumbe hakuangalia vizuri kuwa amempa film ya watu wako uchi ikaishia kuwa aibu kubwa sana, kwa hiyo toka siku hiyo huwa ninajaribu kuwa careful mkuu,

Muda wa kuanza kuweka huko Tube sina mkuu, isipokuwa nimejaribu kuwasiliana na wenye kuweza, nia na madhumuni yangu ni kutaka iwekwe hapa JF, kwa hiyo soon itawekwa tu mkuu, au una hoja nyingine mkuu? nifahamishe tu mkuu!
 
Aliyeiandika hii arcticle yaani Mkulu Wangu Ngurumo, ni mtu ninayemuheshimu sana kwa sababu huwa hachanganyi maneno wala hana mchezo, lakini ninakubaliana naye na pia kutofautiana naye kuwa kwa dataz nilizonazo aliyehusika na "one on one" ni mwingine,

lakini huenda huyu anayemsema ndiye the originator, lakini facilitator ni mwingine kabisa, yaani "mzee wa mbeya" Mkuu wangu Mtanzania upo hapo?
 

Mkulu naomba utuwekee angalau vijihint
 
there is nothing but speculations....
who is sure that balali was given sumu?
who is sure that balali was even sick when he was in the US?
who is sure that balali died/ did not died on may 16( or 18 ...which ever)?

if anybody knows with a certinity, then they should give us facts with proof and not 'i will not mention the name' crap
 

naona inakaribia wiki..hivi si unajyo kwenye CD hiyo Video? kwa nini usiende kwenye internet cafe waambie wakuwekee kwenye Youtube au google video


Ni free na hauchajiwi...
 
Nimetoa hint ya kutosha hapo, wakati mwingine na sisi tujaribu kufikiri na kutafuta pia, tuache uvivu, ninamtafuta Ngurumo sasa hivi ili ku-compare notes kwanza!
 
naona inakaribia wiki..hivi si unajyo kwenye CD hiyo Video? kwa nini usiende kwenye internet cafe waambie wakuwekee kwenye Youtube au google video

Ni free na hauchajiwi...

Mkuu GT,

Nia ni kuiweka hapa JF, kuna wanaoweza kufanya hivyo na watafanya hivi karibuni, kwa wale walioniomba copy naomba kusema hivi, siwezi kuirusha hewani ikakufikia sasa jaribu kufikiri kabla ya kunitumia ujumbe!
 
Huu mtandao ni mnene sana na nilitabiri wana JF kutegwa!
Kila ninalotabiri ndugu zangu sijui kwanini hutokea!
Sasa hapa ni mwendo wa rumours after rumours hadi watu wachoke...Inawezekana nia ni kuwachosha watu kwa mi information isiyokuwa na kichwa wala miguu na kuwa throw out of the real point..Ikishindikana then tujaribu kusije kukatokea watu watakaoipelekea JF kufungwa kwasababu hilo halitazima moto..Bali kuuchochea!
 
Anayeamini kuwa aliyefanya hivi ni ni RA ameuzwa na hajakaa chini kufikiri. Ngojeni wengine tutakapoandika ndipo dots zitakapounganishwa. Katika kutafuta majibu naomba niwape clue mbili:

a. Ni nani sources za habari za Ballali, ugonjwa wake, sumu, kifo, n.k
b. What if the misinformation of Tanzania haikuanza wiki iliyopita au baada ya Ballali kuondoka?


sasa hivi lengo ni kuhamisha kidole toka kwa mhusika mwenyewe na kukielekeza kwa mtu mwenye jina baya. Nilipokuwa mdogo tuliishi jirani na jamaa mmoja ambaye alijulikana kuwa ni mwizi. Lakini huyo jamaa pia alikuwa ni mjenzi. Sasa alikuwa anaiba na kujenga au anapopewa nafasi ya kujenga anaiba pia cement nk na kujenga kwake.

Sasa sisi tukafikiria kwanini tusimpe huyu jamaa ujenzi wa nyumba yetu? Tulipompa ujenzi na kumsimamia kutwa nzima wizi mtaani ulipungua. Lakini siku moja tukiwa kwenye kumwaga zege kutwa nzima na makarai yale... tunarudi mtaani (tulikokuwa tunajenga ni kama maili 3 hivi toka kibanda cha zamani) basi mtaani walipomuona jamaa watu wakaanza kumpigia kelele kuwa amewaibia mchana huo. Hilo lisingewezekana kwani karibu watu 20 walikuwa naye kwenye ujenzi wetu.

Lakini wakajitokeza hadi mashahidi kuwa walimuona huko. Ni baada ya hekima ya wazee ndipo ilipogundulika kuwa mwizi alikuwa ni mtu mwingine mtaani hapo ambaye alikuwa anatumia "sifa mbaya" ya fundi wetu kujitajirisha na yeye akijua kuwa akiiba atakayelaumiwa ni "mwizi anayejulikana".

so, in this case kuna jaribio la kumfanya RA ndiye mwizi wao!! na mwizi mwenyewe anaendelea na mikutano, yuko Bubu, na hakuna mtu atakayethubutu kuandika kichwa hicho cha habari bila kutiwa kashkash.
 
Wale waliokuwa wakifurahishana kuwa tusahau kuhusu kifo cha Ballali kwasababu alikuwa huru na haikuwepo haja ya kuwa shaidi wa kwanza ama mtuhumiwa ama "A key suspect" kama walivyosema wanasheria wetu then wajiulize upya?
Wakina MKJJ kujaribu kufunika ukweli na kudhalilisha wengine kwa maneno ya kejeli kuwa tunaota!
Sasa hawa wanasheria ambao we think the same nao wanaota?


Kati ya hayo niliyo highlight hapo juu ambayo wanasheria hao wameyasema kuna ambalo sijawahi kulizungumzia hapa jf?

Sikusema kuwa itakuwa vipi serikali imlipie Ballali gharama za matibabu halafu isijue kilichomsibu?
Bilii zote za matibabu serikali ni lazima inazo na inajua everything!
Wanajidahi kuwa hawajui...Fool me once..Shame on you..Fool me twice shame on me.
 

[FONT="Comic Sans M[B][B]gaijin,

In his resignation letter to the president, Balali mentioned sickness as a major factor that has forced him to resign.[/B][/B]S"][/FONT]
 

We unaongea lugha ya kigeni hapa. Nakuelewa kwa mbali ni kama lugha ya Mantiki. Kama nimepatia, basi hatuongei hiyo lugha hapa. Ni sawa na kumwongelesha Mhabeshi Kidachi. Hatokuelewa!

Wazungu waliobobea kwenye elimu za Sayansi wanaamini Elvis Presley kajificha na Tupac. Itakuwa sisi wenye asili ya imani za Kichawi Chawi na kuamini yasiyo thibitika?

Ili tuelewane na hiyo lugha yako ya kigeni, kwanza tupe Kamusi ya Mantiki-Kiswahili au Logic-English Dictionary!
 
Ndio maana wa Kenya huwa wakituita wa Tanzania kuwa waswahili maneno mengi.....sasa ndio ime click in my mind
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…