::Habari za Tanzania Jumatatu Juni 09, 2008
Imetolewa mara ya mwisho: 08.06.2008 1519 EAT
Mchungaji aliyemzika Ballali anena
*Athibitisha aliumwa kwa muda mrefu
*Aeleza alivyoongoza ibada, maziko
Na Hassan Abbas
WAKATI Watanzania wakiwa bado katika hali ya sintofahamu kuhusu ukweli juu ya kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Daudi Ballali, Mchungaji aliyeendesha misa na hatimaye maziko yake nchini Marekani amekizungumzia kifo hicho na namna maziko yalivyokuwa.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili kwa njia ya mtandao, Mchungaji Klaus Sirianni wa Kanisa Katoliki la St. Stephen Martirs' lililoko District of Columbia, Washington DC, amelithibitishia gazeti hili kuwa Dkt. Ballali alikufa na yeye ndiye aliyeongoza misa na baadaye ibada ya maziko.
"Ni kweli Dkt. Daud T.S Ballali alifariki Mei 16, 2008 akiwa na baadhi ya wana ndugu zake hapa nchini Marekani," alisema Mchungaji Sirianni.
Kumekuwa na uvumi unaozidi kuenea nchini ambapo wengi wanahoji ukweli wa kifo cha Dkt. Ballali huku baadhi wakitaka kujua kama kweli kulifanyika ibada ya maziko mjini Washington kama ilivyokuwa imetangazwa.
Akithibitisha kufanyika kwa misa na ibada ya maziko ya Ballali, Mchungaji huyo ameliambia Majira Jumapili kuwa: "Misa iliyofanyika katika tamaduni za kikristo ya Dkt. Ballali ilifanyika kwenye Kanisa la St. Stephen Martyr, Washington, District of Columbia, kuanzia saa nne asubuhi, Mei 23, 2008."
Akaongeza kuwa yeye ndiye aliyesimamia misa na baadaye maziko hayo. "Aliyeongoza misa na ibada ya maziko ni mimi Mchungaji Klaus Sirianni," alisema mchungaji huyo ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa parokia ya kanisa hilo.
Katika maziko hayo Mchungaji Sirianni amethibitisha kuwa wahudhuriaji walikuwa ndugu, jamaa wa karibu na watu waliowahi kufanyakazi na marehemu huku akimtaka mwandishi kwa maelezo zaidi kuhusu sababu za kifo hicho awasiliane na wanafamilia.
"Maziko yalifanyika kwenye makaburi ya kikatoliki ya Gate of Heaven yaliyoko eneo la Silver Spring, Maryland na kwa mara nyingine mimi ndiye niliyesimamia ibada hiyo tena."
Kinepi
Baada ya kusoma habari hii, nilinyanyua simu nikampigia Padri Klaus Sirianni wa kanisa katoliki mtakatifu Stephen Martyr, Washington, District of Columbia,
Maswali na majibu yalikuwa kwa lugha ya kiingireza ila nitachapa kiswahili.
swali. padri habari za leo
jibu: Nzuri
maelezo: mimi ni kinepi Mtanzania,Nimepata taarifa kuwa wewe ndiye ulieendesha misa ya marehemu Dr. Daudi Balali
jibu: Ndio
swali: utajali kama nikikuuliza maswali kuhusu misa ile na huduma yote kwa ujumla
jibu: hapana
Ndio, Balali alifariki na mimi ndie niliyeendeshasha ibada ile mpaka makaburini akazikwa.
Swali: Padri je katika huduma yako hiyo ulipata kuuona mwili wa DR. balali ???
Jibu: Hapana.sikuuona.
Swali: Je ulipata wasaa wa kufunguliwa jeneza hata mara moja?"
Jibu: Hapana jeneza halikufunguliwa, niliamini maneno ya ndungu za marehemu kwamba aliyeko humo kwenye Jeneza ni Balali.
Swali: Je si lazima kujua nini kipo ndani ya jeneza kabla ya kukiombea?
jibu: ni vyema ukauliza ndugu za marehemu kwa maelezo zaidi.
kinepi: asante padri kwa muda wako, kwaheri.
Kutoka ubalozini wanarushiana mpira kuwa ni nani aliuona mwili.
Mpaka sasa Kifo cha Balali ni kitendawili.
Ninafanya jitihada kujua ni hospitali gani alilazwa. Nikipajua tu au mtu yeyote kama ana info tafadhali anipatie lazima ni jue Balali yuko wapi.
Majibu ya wizi wa fedha zetu ni muhimu sana.