Kifo cha Edgar Lungu na uhaini wa Tundu Lissu ni funzo kwa Rais Samia

Huwezi kuwa kiongozi wa kulipa kisasi
 
Hapa umemaliza kila kitu. Mimi siandiki tena
 
Ngoja nikufundishe Jambo, Mungu akiamua kwasisi tunao amini katika dini, haijalishi ni lini itatokea ila atahakikisha anakuacha hai na wewe upate uchungu alioupitia mwenzako
Tena kama haamini ajiulize tu rahisi kuwa nani alijua Samia Hasan Suluhu atakuwa rais wa nchi yetu? Dunia na asili ina mengi na inaweza kukushangaza muda wowote kwa namna ya ajabu usiyoitegemea. Naungana na mtoa mada,ubinadamu na kuwatendea kwa staha wapinzani wetu kwenye siasa ilipaswa iwe kipaumbele kwa waliopo madarakani. Mifano ni mingi ni watu wameshika madaraka na kulewa tu hwawezi elewa haya ila nyakati zikifika watatia huruma.
 
We bwege Tanzania na Zambia kwenye suala la siasa ni vitu viwili tofauti. LinganishaTanzania ya CCM na China ya CPC. Mtaokoteza kila takataka ila sisi tuna siasa yetu ya kipekee Afrika.
Mkuu hakuna tofauti, isipokuwa wewe ndiye unayechanganya hoja hapa.
 
Mkuu siku ya kufa Nyani miti yote huteleza.

Kwa mahusiano ya chuki aliyoyaendekeza Lungu kwa Hichilema hata baada ya kuondoka madarakani, serikali ya Zambia ilitimiza wajibu wake jinsi ilivyopaswa.

Mkuu inaonekana hujafuatilia vitimbi vya Lungu akiwa Rais na baada ya kuondoka madarakani.

Hichilema alijizuia sana na alimvumilia sana. Familia ya Lungu inatema chuki aliyokuwa nayo Lungu dhidi ya Hichilema!!
 
Mkuu siku ya kufa Nyani miti yote huteleza.

Kwa mahusiano ya chuki aliyoyaendekeza Lungu kwa Hichilema hata baada ya kuondoka madarakani, serikali ya Zambia ilitimiza wajibu wake jinsi ilivyopaswa.

Mkuu inaonekana hujafuatilia vitimbi vya Lungu ikawa Rais na baada ya kuondoka madarakani.

Hichilema alijizuia sana na alimvumilia sana. Familia inatema chuki aliyokuwa nayo Lungu dhidi ya Hichilema!!
 
Kwa Samia Suluhu Hassan, mbona hiyo itakuwa ni heshima kubwa kwake! Huko ndiko nyumbani kwao; hapa yupo kutawala tu na kutapanya mali za waTanzania na kuwafanya watwana nchini mwao!
🤔🙄👀
 
 
Huko DRC seneti ya nchi hiyo imefuta kinga ya raisi kutoshitakiwa likimlenga bilionea Joseph Kabila.

Twaweza sikia akipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za ufisadi na treason. Thats Karma unapotenda vibaya kupitia bunge ujue kesho linaweza kukutendea vibaya pia.

Yaani chawa wanapukusifu umepoa huku wakiokota kodi.zetu na matamasha feki wanayoandaa kesho wanaweza kukukana kwamba ulikuwa fisadi. A lesson to learn kwa viongozi.
 
We bwege Tanzania na Zambia kwenye suala la siasa ni vitu viwili tofauti. LinganishaTanzania ya CCM na China ya CPC. Mtaokoteza kila takataka ila sisi tuna siasa yetu ya kipekee Afrika.
Duniani hakuna kilichona mwanzo kisiwe na mwisho hilo ujinga wako unaamini kwamba ccm imeshika mpini kwasababu ya kutumia vyombo vya dola usijidanganye. Ccm itatoka tu na usiwe na wasiwasi. Magufuli mlimpamba sana leo yuko wapi na alitumia misafara na jeshi kumlinda ila umauti hamkuweza kuudhibiti ili asife na hilo la ccm kuondoka madarakani itaondoka tu.
 
Edgar Lungu alimweka ndani Hakainde Hichilema kwa kosa la uhaini , siku 8 za mwanzo Hakainde aliwekwa kwenye chumba ambacho hakuna choo, hakuna maji, hakuna umeme hakuna hewa.
Kumbuka Hakainde ndo tajiri namba moja Zambia ...Hakainde alienda kumpigia magoti Edgar Lungu kama amekosea amsamehe lkn Edgar Lungu kwa sababu alikua dictator alimkatalia akaendelea kumyanyasa kwenye maisha yake ya kisiasa Hakainde alikamatwa mara 17...
Leo Samia anamlaza Lissu sehemu yenye maji taka na mikojo na amemueka kwenye selo ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa wakati hajahukumiwa ..Ipo siku yatakwisha lkn akumbuke maumivu huwa ni makubwa sana so kusamehe kuna tegemea pia jinsi wewe ulivyo ni treat.
 
Tofauti ni kwamba hapa kwetu CCM itatawala milele kwahiyo hutapata hiyo furaha. Na hata chama kingine kikishinda wana CCM tutakitoa na kuirudisha CCM
 
Ni kweli kabisa mkuu. Hebu wewe fikiria pamoja na Tundu Lissu kupigwa risasi zote zile bado yupo hai lakini Magufuli aliyekuwa analindwa na mitutu saa 24 sasa yupo kaburini. Mungu ana siri kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…