Kifo cha Edgar Lungu na uhaini wa Tundu Lissu ni funzo kwa Rais Samia

Labda na wewe utakuwa umekufa kitambo tayari
Hata mm na wewe pia tuna mwisho mkuu. Hatutaishi milele. Ipo siku tutaingia kaburini na kuoza. Hiki sio kitu kipya.
 
Naingia kwenye hoja moja kwa moja pasipo kuwachosha wala kuwapotezea muda. Naomba niwapitishe kwenye kisa kichungu lakini chenye nguvu kinachotokea Zambia leo, ambacho kila dikteta wa Kiafrika anapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa sana.

Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini mnamo 2021, mambo yalibadilika. Wananchi wa Zambia walipiga kura, na meza ikapinduka. Hakainde Hichilema akachaguliwa kuwa Rais. Edgar Lungu sasa akawa mpinzani. Akawekwa kando na akawa hana udhibiti tena.

Ilipofika mwaka 2025 Edgar Lungu akaanza kuumwa. Hali yake ilihitaji matibabu ya haraka nje ya nchi. Familia yake iliomba ruhusa kutoka kwa Serikali ya Hakainde Hichelema ili asafirishwe hadi Afrika Kusini kwa matibabu.

Lakini serikali ya Hichelema ikachelewsha ruhusa ya Lungu kwenda kutibiwa. Ruhusa haikuja haraka. Mchakato ulikuwa wa polepole, na kila walipozidi kuchelewa kulifanya hali ya afya ya Lungu kuzidi kudorora.

Mpaka walipomruhusu Lungu kusafiri, walikuwa wamechelewa. Alitua Afrika Kusini, lakini afya yake ilikuwa tayari imezorota kupita kiasi. Ndani ya siku chache, Edgar Lungu alifariki.

Sasa taifa linaomboleza, lakini uchungu katika moyo wa familia yake ni mkubwa zaidi. Wanaamini kwamba ikiwa serikali ingemruhusu kuondoka mapema, huenda angali hai hadi leo.

Katika uamuzi wa ujasiri na wa kimhemko, familia imekataa mazishi ya serikali. Hawataki serikali ambayo wanalaumu kwa mateso yake kumlaza. Badala yake wameamua kumzika Lungu huko Afrika Kusini.

Ndiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni. Hii sio tu kuhusu Zambia. Huu ni ujumbe kwa viongozi wote wa Afrika wanaotumia madaraka kunyamazisha upinzani.

Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.

Pumzika kwa Amani Edgar Lungu.
​

Tatizo ni MaCCM wote kujifanya VYURA VIZIWI.
 
Ngoja wajifanye vyura lakini evolutionary changes zitawabadilisha kuwa samaki. Haya majitu ni ya ovyo sana ktk nchi hii. Sijawahi kuona mijitu yenye akili za kiqumer kama miCCM.
 
Umeandika mambo usiyoyajua. Rais Hichilema alikuwa mpinzani kitambo sana na aligombea urais mara 4 kabla ya kushinda mara ya 5. Chanzo kikuu cha yeye kushughulikiwa na serikali ya Lungu na kupewa kesi ya uhaini ni kutopisha msafara wa Rais alipokuwa akienda kwenye sherehe za kimila huko Mongu. HH na msafara wake walifanya jambo la kihuni mno ambalo lingeleta madhara makubwa. Hakuna Rais yeyote angeweza kuvumilia uhuni alioufanya Hichilema hiyo siku. Nimekuwekea video.

Pia anachokifanya HH ni sawa na mtangulizi wake. Lungu aliondoka Zambia kwenda SA kwa matibabu kijanja hali iliyofanya mkuu wa viwanja vya ndege na baadhi ya wafanyakazi wa uwanja wa ndege kutumbuliwa kwa kosa la kumruhusu Lungu kupita.

Pia familia ina sababu za msingi kukataa Lungu asizikwe Zambia. Sababu kuu ni kuwa marehemu aliacha wosia kuwa HH asihudhurie msiba wake ila HH kakomaa na kutaka lazima ahudhurie. Kwa sheria za Zambia familia ndo yenye uamuzi kuhusu mazishi ya baba yao Rais mstaafu.

Siku nyingine jifunze kwanza siasa za nchi jirani kabla ya kuandika kihisia kama mwanamke mwenye tamaa ya hela. Pumbav

View: https://youtu.be/13igYRDa1-M?si=YHw7MXbK3VdvpaHH
 
Mkuu ina maana huoni uhusiano uliopo kati ya ushenzi ambao Samia anamfanyia Tundu Lissu na ushenzi ambao Lungu alimfanyia Hichelema? Hebu soma hapa chini kwanza ufunguke ubongo wako uliovurugwa na uchawa uliomo kichwani mwako. Na, je, ushenzy ambao Magufuli alimfanyia Tundu Lissu unasameheka?

Soma hapa chini uujue kwa undani ushenzi wa Lungu kwa Hichelema. Je, amemkamata na kumtia kizuizini mara ngapi?

Ubaya ubwela. No reforms, no election. Dawa ya moto ni moto. Malipo ni hapa hapa duniani.
Nakubaliana na wewe 100%: "NO REFORMS, NO ELECTION".

Hili la "Dawa ya moto ni moto", hili linajadilika. Kwani haiwezi kuwa "Dawa ikawa MAJI";
Kama ni moto usiozimwa kwa maji, zipo njia nyingine tele za kuzima mioto ya aina hiyo. Kwani lengo ni nini, kuuzima moto au siyo?
"Malipo ni hapa hapa duniani"? Imani zetu za asili, za hapa hapa kwetu Africa zinasemaje juu ya hili?
 
Ila tutaiacha CCM ikitamba
Wewe unaamini hivyo? Nenda kaitafute UNIP ya Zambia, au KANU ya Kenya kama utazikuta huko.

Hii CCM anaimaliza Samia na Genge lake. Bahati pekee ya yenyewe kupona ngwe hii ni huko ndani patokee watu wenye akili timamu wa kuijengea uhai mpya, vinginevyo hii iliyotekwa na BAKWATA haitadumu.
 
CCM huwezi kuifananisha na KANU, Lazima ujue CCM siyo chama ni mfumo yaani kuitoa ni kama kutoa chumvi baharini
 
Rubbish,
Edgar Lungu amekalia kiti cha urais miaka kibao bila kubotesha hispitali za Zambia.
Hospitali za Zambia zingekua na vifaa tiba na mabingwa si angetibiwa on time tena kwa gharama nafuu.
Watu wanakaa Ikuluwsnajisahau sana hawajui kwamba kuna kesho.
Napenda nimpongeze Kikwete kwa kuboresha muhimbili hasa pale JKCI na Mliganzila kiasi kwamba safari za india zimepungua sana na hata watu wakubwa including ex presidents wametibiwa Muhimbili.
Big up home boy.
 
Kwa kuwa watu wanafanya Mabaya na maovu na wanajua hakuna Consequences.

Ni wakati sasa mifumo ibadilike. Ulaya na Marekani wanajua chochote unachofanya ukiwa kiongozi you will eventually suffer the outcomes.

Ndio Maama Israeli inapopigana vita wanadeal na Viongozi wa maadui. Hawana muda na raia wa kawaida.

Ndio kusema kwamba viongozi wa hayo makundi Hasimu chochote watakachoamua wajue kuna outcomes nzuri au mbaya na wao yatawahusu.
Mkuu 'Bush Dokta', ni sahihi uliyosema kuhusu hao viongozi wa uUlaya na 'consequences' kama ulivyo zieleza; isipokuwa hukuwa 'specific' kuhusu 'consequences' hizo! Sheria zipo zinazowabana, na kulipia maovu yao. Sasa linganisha na hili la Hichilema Haikande na Edgar Lungu; au wengineo hapa kwetu Afrika.

Hilo la Israel ulilogusia; hili ni wazi kuwa unaweza kuwa na upungufu mkubwa katika kulielewa au kulisemea. Mjadala mpana tunaoweza kuuanzisha hapa kuonyesha kwamba hayo anayofanya Israel na hawa akina Trump, Bush na wenzao wengi ya kuua viongozi yanayo matatizo mengi sana. Na elewa pia, wanafanya hivyo sasa kwa kujuwa wao hayawezi kuwapata, kwa vile wanao ulinzi na hao wengine hawana vifaa vya kuwafikia. Sasa fahamu kuwa muda si muda, teknologia ya kuyafanya hayo itakuwa kila mahali; kiasi kwamba na wao hawataweza kuwa na uwezo wa kujificha popote.
Hili ni swala la muda tu!
 
Family ya ECL imejaa uswahili sana kama familia za Magomeni bana!!! Yani Mkuu wa Nchi sio mali ya familia bali ni Mali ya umma

Kukomaa azikwe SA tena kwa Private burial ni Ujuha kabisa hio familia itamzika ECL halafu itarejea zambia kuendelea Na Maisha bure kabisa hao watu

Family imeona itumie msiba wa ECL kugain public attention, Juzi remains za ECL zilikuwa ziwe reptriated to Zambia na Everything was on Place ila later kabisa family ika deny

Good enough HH amefanya state adress na Kudai kuwa kama Taifa sasa wanazitisha muda wa Kuomboleza na Kila kitu kirudi Normal, Ametoa pia Room kwa family Kufanya engagements na Serikali kwa ajili ya State funeral ya Mkuu huyo wa Nchi Wa sita baada ya HH kutoa hio Short Hotuba kesho yake familia ya ECl imeamka na Kusema itamzika ECL South africa.
 
Sawa Bwana Kalamu, nimehusianisha tukio la Israel dhidi ya mahasimu ktk kuelezea mfano tu kwamba Mkubwa ndiye anatakiwa kubeba msalaba kwa maamuzi yake. Sijataka kujadili kwamba Israeli na his Allies wako sahihi au la.
 
Family ya ECL imejaa uswahili sana kama familia za Magomeni bana!!! Yani Mkuu wa Nchi sio mali ya familia bali ni Mali ya umma

Kukomaa azikwe SA tena kwa Private burial ni Ujuha kabisa hio familia itamzika ECL halafu itarejea zambia kuendelea Na Maisha bure kabisa hao watu

Family imeona itumie msiba wa ECL kugain public attention, Juzi remains za ECL zilikuwa ziwe reptriated to Zambia na Everything was on Place ila later kabisa family ika deny

Good enough HH amefanya state adress na Kudai kuwa kama Taifa sasa wanazitisha muda wa Kuomboleza na Kila kitu kirudi Normal, Ametoa pia Room kwa family Kufanya engagements na Serikali kwa ajili ya State funeral ya Mkuu huyo wa Nchi Wa sita baada ya HH kutoa hio Short Hotuba kesho yake familia ya ECl imeamka na Kusema itamzika ECL South africa.
Hata mimi nimeshangaa eti asizikwe nyumbani. Huu ni mwendelezo wa jeuri ile ile iliyojengeka kwa muda mrefu.
 
Mkuu siku ya kufa Nyani miti yote huteleza.

Kwa mahusiano ya chuki aliyoyaendekeza Lungu kwa Hichilema hata baada ya kuondoka madarakani, serikali ya Zambia ilitimiza wajibu wake jinsi ilivyopaswa.

Mkuu inaonekana hujafuatilia vitimbi vya Lungu ikawa Rais na baada ya kuondoka madarakani.

Hichilema alijizuia sana na alimvumilia sana. Familia inatema chuki aliyokuwa nayo Lungu dhidi ya Hichilema!!
Ninakuelewa vizuri kabisa mkuu 'MIZANIA TZ'. Nilijikaza sana kuandika hayo niliyo andika hapo. Ndiyo maana ilinilazimu nizunguke kiasi kile nilichozunguka kuwasilisha ujumbe huo.

Usifikiri ilikuwa rahisi kwangu kuandika hayo niliyo andika hapo!
 
Back
Top Bottom