Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho. Ikiwa dunia ina mwisho iweje CCM ikose kuwa na mwisho mkuu?Tofauti ni kwamba hapa kwetu CCM itatawala milele kwahiyo hutapata hiyo furaha. Na hata chama kingine kikishinda wana CCM tutakitoa na kuirudisha CCM
Tatizo chawa wa CCM wanajidanganya CCM haina mwisho. Wajifunze kwa Mugabe aliyekuwa analindwa na jeshi 24/7. Jeshi hilo hilo lilishindwa uvumilivu likamtimua madarakani akaenda kufia uarabuni kama mbwa na kuzikwa huko huko kama alivyozikwa Idd Amin. Hakuna jambo lenye mwanzo likakosa kuwa na mwisho. Hata hii dunia tunayoishi ina mwisho sembuse CCM.Duniani hakuna kilichona mwanzo kisiwe na mwisho hilo ujinga wako unaamini kwamba ccm imeshika mpini kwasababu ya kutumia vyombo vya dola usijidanganye. Ccm itatoka tu na usiwe na wasiwasi. Magufuli mlimpamba sana leo yuko wapi na alitumia misafara na jeshi kumlinda ila umauti hamkuweza kuudhibiti ili asife na hilo la ccm kuondoka madarakani itaondoka tu.
Kwa binadamu ni ngumu lakini God has all options akitaka.Nachelea kukubaliana na hoja yako nzuri kwenye maisha, ila kwa sheria zetu za uchaguzi na tume yetu ; kwa Tanzania usitegemee mabadiliko ya kiungozi kupitia uchaguzi.
Vv
Hili ni fundisho kubwa sana sio tu kwa CCM na chawa wake bali ni kwa madikteta wote wa Afrika wanaotumia mdaraka yao kuwanyanyasa wapinzani, kuteka na kuua wakosaji na kutapanya rasilimali za umma. Ipo siku madikteta hawa wataonja joto ya jiwe.Edgar Lungu alimweka ndani Hakainde Hichilema kwa kosa la uhaini , siku 8 za mwanzo Hakainde aliwekwa kwenye chumba ambacho hakuna choo, hakuna maji, hakuna umeme hakuna hewa.
Kumbuka Hakainde ndo tajiri namba moja Zambia ...Hakainde alienda kumpigia magoti Edgar Lungu kama amekosea amsamehe lkn Edgar Lungu kwa sababu alikua dictator alimkatalia akaendelea kumyanyasa kwenye maisha yake ya kisiasa Hakainde alikamatwa mara 17...
Leo Samia anamlaza Lissu sehemu yenye maji taka na mikojo na amemueka kwenye selo ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa wakati hajahukumiwa ..Ipo siku yatakwisha lkn akumbuke maumivu huwa ni makubwa sana so kusamehe kuna tegemea pia jinsi wewe ulivyo ni treat.
Weka recoding sawa... I'dd Amin na Mabutu walizikwa nchi za kigeniNdiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni
SASA NA WEWE SIJUI MJINGA.HAPO CHA KUSIFIA KUTOKA NCHINI ZAMBIA NI KIPI IKIWA WALICHELEWESHA RUHUSU YA MAREHEMU KWENDA KUTIBIWA? HUONI KUWA RAIS WA SASA NI KATIRI SANA KIASI CHA KUMNYIMA MGONJWA KIBALI CHA KWENDA KUTIBIWA? ANA ROHO YA KITAILI SANA HUO JAMAA YAKONaingia kwenye hoja moja kwa moja pasipo kuwachosha wala kuwapotezea muda. Naomba niwapitishe kwenye kisa kichungu lakini chenye nguvu kinachotokea Zambia leo, ambacho kila dikteta wa Kiafrika anapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa sana.
Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.
Lakini mnamo 2021, mambo yalibadilika. Wananchi wa Zambia walipiga kura, na meza ikapinduka. Hakainde Hichilema akachaguliwa kuwa Rais. Edgar Lungu sasa akawa mpinzani. Akawekwa kando na akawa hana udhibiti tena.
Ilipofika mwaka 2025 Edgar Lungu akaanza kuumwa. Hali yake ilihitaji matibabu ya haraka nje ya nchi. Familia yake iliomba ruhusa kutoka kwa Serikali ya Hakainde Hichelema ili asafirishwe hadi Afrika Kusini kwa matibabu.
Lakini serikali ya Hichelema ikachelewsha ruhusa ya Lungu kwenda kutibiwa. Ruhusa haikuja haraka. Mchakato ulikuwa wa polepole, na kila walipozidi kuchelewa kulifanya hali ya afya ya Lungu kuzidi kudorora.
Mpaka walipomruhusu Lungu kusafiri, walikuwa wamechelewa. Alitua Afrika Kusini, lakini afya yake ilikuwa tayari imezorota kupita kiasi. Ndani ya siku chache, Edgar Lungu alifariki.
Sasa taifa linaomboleza, lakini uchungu katika moyo wa familia yake ni mkubwa zaidi. Wanaamini kwamba ikiwa serikali ingemruhusu kuondoka mapema, huenda angali hai hadi leo.
Katika uamuzi wa ujasiri na wa kimhemko, familia imekataa mazishi ya serikali. Hawataki serikali ambayo wanalaumu kwa mateso yake kumlaza. Badala yake wameamua kumzika Lungu huko Afrika Kusini.
Ndiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni. Hii sio tu kuhusu Zambia. Huu ni ujumbe kwa viongozi wote wa Afrika wanaotumia madaraka kunyamazisha upinzani.
Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.
Pumzika kwa Amani Edgar Lungu.
Ndio. Mungu ni fundi sana. Magufuli alimchakaza Tundu Lissu kwa risasi lakini leo hii Tundu Lissu anaishi, ijapokuwa mwili wake umejaa vyuma. Kana kwamba hilo halitoshi, bado rais Samia anaendelea kumlaza TAL gerezani pamoja na wafungwa wanaosubiria kunyongwa. Mungu wetu wa mbinguni tunakuomba ufanye jambo. Ee Mungu mwenye hasira na huruma tunakuomba ushuke utuokoe waja zako tunaonyanyaswa na serikali ya kishetani ya CCM. Amina.Kwa binadamu ni ngumu lakini God has all options akitaka.
Huyo kijana amefanana sana na Rizwani KikweteUzuri ni kuwa huyu hafi ataishi milele yote View attachment 3378033
Jino kwa jino ndiyo mpango mzima.Kisasi ni khaqi kilipwe
Kwa raia hawa nchi yetu labda vitukuu vyetu 😏CCM INATOLEWA KWA MAPINDUZI YA KIRAIA AU JESHI NA C VINGENEVYO.SOMA VYAMA VYA UKOMINIST ILIVYOONDOLEWA
Dawa ya moto ni moto na mwiba ulipoingilia ndipo unapotokea. Wewe ulidhani yeye, Lungu, alipomfungia Hichelema kwenye chumba kisichokuwa na hewa wala choo ulikuwa sio ukatili? Au unadhani Magufuli asingekufa halafu Tundu Lissu akawa Rais angemuacha salama kwa risasi zote zile alizommiminia? Thubutu!SASA NA WEWE SIJUI MJINGA.HAPO CHA KUSIFIA KUTOKA NCHINI ZAMBIA NI KIPI IKIWA WALICHELEWESHA RUHUSU YA MAREHEMU KWENDA KUTIBIWA? HUONI KUWA RAIS WA SASA NI KATIRI SANA KIASI CHA KUMNYIMA MGONJWA KIBALI CHA KWENDA KUTIBIWA? ANA ROHO YA KITAILI SANA HUO JAMAA YAKO
Ukitenda mabaya lazima ulipwe ubaya hakuna jinsi nyingineMkuu karma hufanya kazi kwa njia ya kisasi, huu ni mfumo wa asili!
Huwezi kupanda mpapai ukaota mchongoma au ukaotesha mua ukavuna shubiri! hapana, unavuna ulichopanda!
Wazungu wanatukumbusha kwamba what comes around, goes around. Wema hauozi. Watendee mema wapinzani wako wa kisiasa kwani hujui kesho Mungu atawapa madaraka gani ili nao wakunyooshe jinsi ulivyokuwa ukiwanyoosha.Kwa hakika maisha ya mwanadamu ni mafupi sana .
Ishi vizuri na watu ili uishe vizuri , na siku zote hakuna ubaya usiorudi.
Mkuu umemaliza kila kitu. Kama kiongozi anataka asilipizwe kisasi, basi asiruhusu wapinzani wake kutekwa na kuuawa. Na ikiwa anahitaji kuheshimiwa, tunaomba amrudishe Mdude akiwa hai. Au kama ameishamuua, tunaomba familia irudishiwe mwili iuzike kwa heshima. Wasiwe wanaua watu na kuwatupa mtoni waliwe na mamba au mbugani waliwe na wanyama kama walivyomtupa Sativa mbuga za wanyama aliwe na fisi.Mkuu karma hufanya kazi kwa njia ya kisasi, huu ni mfumo wa asili!
Huwezi kupanda mpapai ukaota mchongoma au ukaotesha mua ukavuna shubiri! hapana, unavuna ulichopanda!