Kifo cha Magufuli: Dunia imeshuhudia Watanzania walivyokuwa wanampenda Magufuli

Kifo cha Magufuli: Dunia imeshuhudia Watanzania walivyokuwa wanampenda Magufuli

Mawakala wa mabeberu walikuwa wanajitahidi Sana kuiaminisha Dunia kuwa Watanzania wako kwenye mateso Sana chini ya utawala wa Rais Magufuli. Waliamini watanzania walio wengi watafurahi Sana na kushangilia Magufuli atakapoondoka madarakani au atakapofariki.

Kinyume chake mabeberu na mawakala wao (wakiongozwa na mkimbizi aliyeko ughaibuni huko ulaya) wamelazimika kushuhudia kwa macho yao umati mkubwa sana uliojitokeza kwa hiari kumuaga shujaa wao Magufuli!! Cha ajabu hata vyombo vyao vya habari kama BBC world service ukiingia kwenye tovuti yao hutakuta habari hii.

Laiti kama nyomi hii ya watu waliojitokeza kumsindikiza shujaa wao, ingekuwa ni maandamano ya kuipinga serikali ya Magufuli, vyombo vyote vya habari duniani vingeipa uzito wa kwanza habari hii kwa wiki nzima! Lakini kwa sasa ukifungua tovuti ya BBC news hutaona habari hii, kwa nini??

Sababu ni aibu!! Siku zote hivi vyombo vimetumika kuiaminisha Dunia kuwa Magufuli hajali watu wake, Magufuli ni mbaya, Magufuli ni dikteta. Waliaminishwa kuwa Magufuli akiondoka watu watafurahi!! Sasa kuionesha Dunia hali halisi ya watanzania walivyokuwa wanampenda kiongozi wao hawawezi!! Hawawezi kujiumbua uongo wao!! Ila wameona japo hawawezi kukiri kuwa Magufuli alipendwa Sana!! Labda anaweza kuzidiwa na baba wa Taifa tu mwl Nyerere!

Kinachowauma zaidi ni utulivu ulivyotawala!! Lingine kinachowauma zaidi ni jembe lililopokea kijiti!! Mama la nguvu Bi Samia Suluhu!! Kwanza kwa kuwaonesha jeuri hakuvaa ile "hirizi" ya wazungu wanayodai inawakinga na corona!! Hilo jopo lote la kitaifa halikuvaa hiyo "hirizi" usoni!!

Hiyo hirizi haijaweza kuwaokoa wao, itatuokoaje sisi? Hiyo Kinga ikitangulizwa mbele ya Mungu inageuka kuwa hirizi. Ukimtanguluza Mungu kwanza halafu hiyo Kinga inafuata inakuwa ni Kinga ya kawaida tu!! Sisi watanzania tumemtanguliza Mungu na Mungu ametuponya!! Mabeberu mtasubiri sana kuona vibaraka wenu wanapata nafasi nchini mwetu.

Nawahakikishia mabeberu watajuta!! Kwa hili jembe lililopokea kijiti, watasema ni afadhali ya Magufuli!! Uzalendo wa huyu mama mpaka nchi utasikia raha! Na mabeberu hawapendi kiongozi awe mzalendo wa nchi yake! Mabeberu wanapenda kiongozi awe wakala wao ilu waweze kuinyonya nchi!! Kwa Bi Samia Suluhu wameula wa chuya!!
Watz tunapendana,pia watz ni wastaarabu wanaomboleza sana misiba na mwisho kiongozi kufa ghafla inauma..... point yako sidhan kama ni kweli
 
Watu kujazana kwenye tukio la mtu kupatwa mkasa siyo kigezo cha upendo. Hata jambazi likiuawa watu hujazana na wengine hulia. Wengine wenye chuki naye huwahi siti ya mbele kushuhudia kama kweli jambazi kauwawa.
mtahamisha magoli sana na yote tutayafunga
 
Sasa kwanini aliogopa Tume huru ya uchaguzi pamoja na ushauri wa Mkapa kama alikuwa anapendwa kiasi hicho? Hukuona ushahidi wa kura fake kukamatwa na zote zikiwa zimepigwa kwa maccm?

1616616158776.jpeg

Kwa hii idadi ya watu wanaokuja mzika..... Naanza kudoubt maneno ya wapinzani kuwa wanaibiwa kura nyakati za uchaguzi

....... ..
 
Yaani watu wamefurahi sana .Kuna wanaosikitika na kunawanao furahi sasa wanaoshangilia ni wengi
 
Weka ushahidi wa tuhuma zako. Mmeaibika mawakala wa mabeberu!!
Umati wa maelfu wanaolia mabarabarani na majumbani ni ushahidi tosha kwamba 2020 #JPM alipita kwa uhalali toka kwa wananchi kiroho safi.
 
Matanga yenyewe ya kulazimishana!! Haya wacha akutane na kina Saanane na Azory!!
Unawatanguliza wenzako kwa kuwaminya kwa mateso makali unasahau na wewe kumbe una ka moyo kanatumia battery ya saa ya mchina!!
Utalipia huu uwongo unaotamka
 
Hivi yale mabunduki yote yaliyokuwa yanamlinda kila kona yalishindwa kumlinda na kifo!!!!hahahahahahahahaha
 
Kwenda kumzika , kumuaga ndio kumpenda ? Mbona mimi simpendi kabisaaa ila nilienda kuthibitisha limekufa kweli ?
 
Hapana. Labda wewe hauko Tanzania na hujui kinachoendelea.

Thro magunomics....Magufuli Ni mtu aliyetengeneza fursa nyingi Sana Sana Sana kuliko unavyodhani.

The problem is no akili chache Sana Zina uwezo na muda wa kuanalyse synthesis zake...

Outcome za kazi zake ndio zimepelekea watu kutandika kanga chini....


Huo ndio ukweli mtake msitake...

Tinaamini Tanzania Ni imara zaidi Sasa. Mafisadi na wanamtandao msijifariji. Kizazi kipya kimemuekewa ankal na hakina mpango wa kurudi nyuma.

Mtaishia kupigwa mawe.
Well said
 
Back
Top Bottom