Kifo cha Magufuli: Dunia imeshuhudia Watanzania walivyokuwa wanampenda Magufuli

Kifo cha Magufuli: Dunia imeshuhudia Watanzania walivyokuwa wanampenda Magufuli

Katika vitu ambavyo wanasiasa wanatakiwa kuwa makini nikutomuongelea Rais Magufuli kwa mabaya wakidhani watapata credit kwa wananchi.
Wanaweza wakajikuta wamepigwa mawe na wananchi..

Let JPM rest in peace.
Watanzania tulimpenda mno.
Na tutaendelea kumpenda daima.
Kwani kama wewe ulimpenda unadhani ambao hawakumpenda wanakosa gani?

Mbona mnafikiri kijima namna hiyo? Kama ambavyo wewe ulikuwa na haki ya kumpenda na wale ambao hawakumpenda wanna haki hiyo! Kwa nini unataka kulazimisha kila mtu awe na mtazamo wako?
 
Lakini ndugu yangu vitu vingine tukae kimya tu maana tunaonekana wajinga kama siyo vituko.
Hivi hiyo simu au laptop uliyotumia kuandika na kutuma huu "uzi" wako si vifaa vilivyotoka kwa "mabeberu"?

Au mwenzetu simu yako au computer yako zimetengenezwa Buza au Tandale kwa Mtogole???
 
Daaaa Juan unajisahaulisha aisee. Huyu Mzee tupende tusipende, alikuwa anapendwa. Na Kazi kubwa kafanya nchi hii. Najua kinachofanya utoe maneno haya ni siasa, lakini ukweli baba alikuwa anapendwa na yupo mioyoni mwa watu. Mimi kama mtu wa takwimu hili naliona wazi wazi. R.I.P Jembe letu Dr. John Pombe Joseph Magufuli
 
Hivi na watu waliokufa uwanja wa UHURU kwa kukanyagana walikuwa ni wapinzani tu! Au CHADEMA mmeishiwa vitu vya kutafutia kiki? Mbona vifo mnavifurahia sana?
 
Matanga yenyewe ya kulazimishana!! Haya wacha akutane na kina Saanane na Azory!!
Unawatanguliza wenzako kwa kuwaminya kwa mateso makali unasahau na wewe kumbe una ka moyo kanatumia battery ya saa ya mchina!!
 
Salim kikeke FALA tu, ETI KAACHA TAIFA LILILO GAWANYIKA...? kivipi???

Mwache si kasha zeeka, ana fukuzwa huko eti kastaafu, ATARUDI KUISHI WAPI KAMA SIO TZ??

Sijui yule Samy Awami aliendaga wapi!!!!? Maana alikuwa akitangaza kwa haki kabisa.
 
Na itachukua muda sana kuondoka ...its a psychological thing, yan unafurahia kua maskini na unajiona uko sawa na tajiri mwenye comfortable life , na ndio hao wameenda kukanyagana huko uwanjani na kusababisha vifo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana hamumjui Magufuli ninyi jinsi kacreate fursa....

Eg...mtu kumiliki kiwanja tz sio issue Tena.....kila mtu hata watoto wamemilikishwa kwa niaba....tatizo labda Ni eneo gani unataka...Kama ulikutwa viwandani au barabarani umetoboa...na hakuna tajiri au mpima ardhi kukuondia bila hiari yako...m

Wengi wao pale unawaona wameandika kanga Wana milioni za kutosha bank...

Viwanja hata dar milioni unapata..masurveyor wamejiajiri wengi Sana......

Expansion ya nchi thro dodoma....dar is still a business town..... Singida tabora shy iringa njombe no zinakula tricke..

Ndio tafsiri ya raisi wa wanyonge...sio hio mnaodhani ninyi

Tuacheni tulie
 
Salim kikeke FALA tu, ETI KAACHA TAIFA LILILO GAWANYIKA...? kivipi???

Mwache si kasha zeeka, ana fukuzwa huko eti kastaafu, ATARUDI KUISHI WAPI KAMA SIO TZ??

Sijui yule Samy Awami aliendaga wapi!!!!? Maana alikuwa akitangaza kwa haki kabisa.
 
Acheni Kumsingizia JK kwa uzembe wa Genge ; ambao toka wakati wa kampeni walijua afya ya Rais haikua nzuri kwakua pacemaker yake ilihitaji kuwa replaced ; lakini walikaaa wakiona anazorota eti kwa kigezo ; “hataki kwenda ujerumani “ , kwani alivyonguka bungeni si alipelekwa hajitambui?

Hata mtaalamu Jakaya yeye ndie aliwaaambia baada ya kuona amekata roho mfanye kifo chake siri ili muangalie mmoja wenu apate madaraka huku mkitaka kumdhulumu Samia ? Hata mke wake hakujua nini kinaendelea?
Wanaotakiwa kujibu kwa kuzembea hadi Magufuli akafa ni madaktari wake na wasaidizi wa karibu ; ukweli tajulikana tu
 
Siyo watanzania wengi waliotumiwa, bali ni watanzania wachache waliokuwa mafisadi. Magufuli alidhibiti mafisadi! Mafisadi na watoto wao ndio wenye chuki na Magufuli.

Ona mwenyewe nyomi iliyokuwa inamuaga kwa heshima zote shujaa wa Taifa! Walitandika na nguo barabarani ili gari lililobeba mwili wa shujaa wa Taifa ili likanyage juu ya nguo!!
Maigizo fc hata aibu , mnakodi mpaka waliaji , waropokaji afande Sele mna akili , sio wote walioenda wanampenda , wengine tumeenda kumuona dikteka ibilisi kafa kweli , uwe unaelewa .
 
Ni kawaida kwa Watanzania kuzika tofauti zao kwenye misiba ili kumsitiri marehemu na kufariji wafiwa. Hii haimaanishi wote wanaoshiriki msiba walikuwa wanampenda au kuwa kwenye good terms na marehemu.

Pia lazima ufahamu kuwa mkusanyiko wa msiba siyo sawa na mkutano wa kampeni wa kisiasa. Mila zetu zinataka marehemu akipitishwa mahali unasimama unatoa heshima, Sasa Mwili wa JPM unapita mabarabarani unataka watu wasiupe heshima waendelee na shughuli zao?

Tatu lazima ujue kuwa Marehemu alikuwa ni rais aliyefia madarakani, kwa heshima ya Taasisi ya Urais, mtu aliyekalia kiti hicho ana heshima yake kama mtu na ana heshima ya kipekee sana kama kiongozi wa Taasisi, maana rais ni nembo ya Taifa, kwa hilo peke yake wananchi watampa heshima tu, na hii haimaanishi eti anapendwa saana ktk mambo ya uongozi wake

Nne, kuna ishu ya media kuutangaza huu msiba, na matangazo yanavyoendeshwa kwa kumanipulate emotions za watu, na pia maombi ya viongozi walioko madarakani sasa kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kumuaga marehemu.

Tano, wapo kweli ambao walikuwa wanampenda na kumkubali, nao watakuwa wamekwenda kwa muktadha huo.

Lazima mjue, akifa raisi yeyote madarakani na mwili wake ukapitishwa mabarabarani na ukatangazwa kwa hisia kali na media, mtawaona wananchi kibao wakitoa heshima yao. Hii ni kwa sababu ya Heshima ambayo wananchi wanayo kwa Taasisi ya uraisi
 
Kwani kama wewe ulimpenda unadhani ambao hawakumpenda wanakosa gani?

Mbona mnafikiri kijima namna hiyo? Kama ambavyo wewe ulikuwa na haki ya kumpenda na wale ambao hawakumpenda wanna haki hiyo! Kwa nini unataka kulazimisha kila mtu awe na mtazamo wako?
Bwashe Kuna mahali nimekulazimisha?

Endelea na chuki zako binafsi tu Wala haina shida.
 
Gadafi walishangilia wale walio lishwa sumu za CNN na propaganda za kipumbavu za magharibi. Ila nadhani waliona madhara yake wale wananchi. Naomba niseme tuwe Watanzania kwanza kabla hatujawa CCM au CHADEMA, tuwe huru kutoa ya moyoni lakini jambo gumu linapolipata taifa letu, tuwe Wamoja kama taifa. R.I.P Dr. John Joseph Pombe Magufuli. Ahsante kwa muda ulioitumikia Tanzania na mwendo umeumaliza.
 
Weka ushahidi wa tuhuma zako. Mmeaibika mawakala wa mabeberu!!
Ushahidi ni kwamba watoto na vijana walipewa karatasi za kura kabla ya uchaguzi na kumpigia kura za ndiyo na waliahidiwa 5000 na hawakupewa (nanda ofisi ya ccm wilaya pale kinondoni). Kwenye Vituo wasimamizi wakuu wote walifungua vituo saa 9 usiku na kuanza kupiga kura za ndiyo kwake. Na kuna engine walipita kutumbukiza Kira zilizopigwa wakati zoezi linaendelea. Mango huu ovi uliratibiwa na TISS.
ULISHAWAHI SIKIA KIONGOZI ANAYEKUBALIKA ANAFANYA HAYO?
 
Watanzania hukusanyika kwa tukio lolote hata kama halina maana.
CCM imefanikiwa sana kuonesha Magu anapendwa wakati amekufa.Sijui ni wanyonge wangapi maisha yao yamekuwa bora kuliko zamani.
 
Back
Top Bottom