Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Mkuu asante sana nadhani umenielewa vyema zaidi kuliko, No doubt you have a good brain with you wengine wametanguliza hisia wameshindwa kufikiri kwa mapana.
 
Ukiwa na familia jenga urafiki na madoctor uwe unawaita tu bar kila week end unawanunulia bia itakusaidia sanaaa
 
Natamani Nilie kilio kisisikike uchungu uishe jamani kupoteza mtoto kunauma kunauma sana EH MUNGU nisaidie mimi mja wako kila kitu kwangu kimegeuga machozi....mwanangu ANGEL nisamehe ni umasikini wangu na ROHO MBAYA za wauguzi ndio umefanya umepoteza maisha, KILIO KISIKIE KWA JIRANI...nani anifute aya machozi nilie mpaka uchungu upungue
 
Kuficha jina la hospital ndo uzembe Mwingine unaendelea kuufanya weka wazi jina tule vichwa vyao
 
Ni ngumu sana na huwa maneno ya kumfanya mtu aliyeondokewa na mpendwa wake afarijike kiukweli kweli huwa hayapo...
Muombe sana Mungu akupatie faraja na pia akupe roho ya kuweza kuachilia uchungu wa kufanyiwa uzembe na hao watu wasio na utu.
Bila hivyo hiyo roho itakutesa sana.
Pole mpenzi japo najua hali uliyo nayo kibinadamu haielezeki
 
Pole sana kwa msiba mzito, kwa hakika hakuna jibu la maana la kutuliza hali unayopitia.
 
Ila kiukweli tunawalaumu watu wa Afya ila hatuangalii chanzo hasa cha tatizo. Kwa ujumla serikali inacheza na afya za watu. Hapa ilitakiwa uongozi wa hospitali, bima ya Afya wote watoe maelezo.
 
Pole sana , jikaze maisha mengine yaendelee mtoto unaweza kumpata mwengine japo inauma sana . Mimi nimepoteza Mzazi wiki hii na hakuna namna ya kumpata mwengine wa kupoza machungu.
 
Pole, waruka na ungo ndio waliosababisha ukose huduma ili wale nyama ya mwanao...
 
Nimejiuliza hayo maswali sijapata majibu.
Sijamhukumu ila nimeshangaa aliposema aliwauliza waseme wanachotaka hawakumjibu, kama alikua na uwezo kuwapa wanachotaka (tuseme ni hela) alishindwaje kutafuta mbadala. Bado sina majibu.
 
Daah mkuu pole sana aisee! Hii nchi kuna mambo yanatia hasira sana.
 
Pole sana ndugu yangu Mungu akawe mfariji kwako ,inaumiza sana ila hakuna namna pole sana
 
Pole sana ndugu yangu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…