Kifo cha Sokoine: Watoto wake wataka mwili uchunguzwe kubaini kama alikufa kwa ajali au la!

Kifo cha Sokoine: Watoto wake wataka mwili uchunguzwe kubaini kama alikufa kwa ajali au la!

Nyerere Aaamini misukule😄😄😄😄😄mcommunist na mambo ya mitaani wapi na wapi ......uzi una kamba huuu
Acha kupayuka. Nyerere hakuwa mkomunisti. Hujui hata maana ya mkomunist unakuja kupiga kelele hapa. Na kwa taarifa yako, kuna wakati wazee wa Dar es Salaam walimwambia Nyerere wampeleke Bagamoyo Mlingotini akafanyiwe "huduma" na wazee wa Bagamoyo, alikubali. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na akili kuliko uwezo wako wa kufikiri
 
Duh

Wakamsingizia Rashid kama vile wanavyomsingizia Naniliu ajali ya Lisu 🐼
Kuna sababu zilizofanya watu wamshuku Rashidi. Ni kweli Sokoine alimwona Rashidi kuwa nae ni fisadi tu, pamoja na Cleopa Msuya. Inasemekana wakati kina Rashidi wanalalamika sana kwa Nyerere dhidi ya Sokoine kwamba anapita kiasi, Nyerere aliwaambia sasa nyie pia si viongozi, kama mnaona anapita kiasi mdhibitini. Watu wanasema Rashidi alikuja sema "uliposema tumdhibiti sie tulijua unamaanisha...." Sasa sijui kama ni kweli.

Lakini kuna watu kama Msuya pia, ambae wakati fulani Sokoine alitaka achunguzwe kwa tuhuma za ufisadi. Msuya alikuja juu sana na kukasirika.

1713441581376.png


Ninachokumbuka ni kwamba, baada ya kifo cha Sokoine, Nyerere hakutaka kabisa kumwona Rashidi. Rashidi aliomba sana lakini ilichukua muda mrefu kabla ya Nyerere kukubali kukutana nae. Je ni kwa sababu Nyerere alijua wamehusika na kifo cha Sokoine?
 
Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.

Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.

Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.

Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.

Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.

Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.

Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.

Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.

Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?
Source of information.....Niamini mimi bro.
 
CCM ni ile ile na haijabadilika. Ni kawaida yao kuKolimbana. Ndiyo maana eti hawaachi chupa ya kinywaji ikiwa wazi mezani ili kwenda msalani. Na hii siyo katika CCM pekee bali ni katika siasa kwa ujumla; na huko kwingine. Ukikaribishwa katika ngoma duarani cheza kwa uangalifu na hakikisha hukanyagi watu na maslahi yao. Vinginevyo unaweza kuwa Wangwelized ukageuzwa jina na kuitwa Mwendazake!

Sokoinne alifanya kosa moja kubwa la kimedani. Inasisitizwa sana kwamba katika siasa; na kwingineko, "Never outshine your master". Yeye sasa ilifika mahali ikasemekana hata Nyerere mwenyewe alianza kumuogopa; na kuna mambo alikuwa anafanya hata bila kuomba ruhusa. He became too powerful to be controlled; and he had to be eliminated.

Ingetokea akawa rais basi wananchi wangeteseka sana. Ni katika maamuzi yake watu walikuwa wanapanga mstari siku nzima ili waweze kununua nusu kilo ya sukari; na kuna watu walifungwa kwa kukutwa tu na dawa ya meno ya Colgate. Wakati ule wa uhujumu uchumi watu walikuwa wanabeba hela zao na kwenda kuzitupa milimani. Uchumi gani ungeweza kustawi katika mazingira yale? Hali ikawa mbaya watu wakaanza kuvaa mpaka magunia.

Baada ya kwenda zake nchi ilipumua; hasa mwanadiplomasia mwenye exposure Salim Ahmed Salim alipokuja kuchukua madaraka ya uwaziri mkuu na kuifungua nchi kidogo. Bila hivyo sijui nchi hii ingeelekea wapi.

Sokoinne had to be eliminated; and rightly so!
 
Kuna sababu zilizofanya watu wamshuku Rashidi. Ni kweli Sokoine alimwona Rashidi kuwa nae ni fisadi tu. Inasemekana wakati kina Rashidi wanalalamika sana kwa Nyerere dhidi ya Sokoine kwamba anapita kiasi, Nyerere aliwaambia sasa nyie pia si viongozi, kama mnaona anapita kiasi mdhibitini. Watu wanasema Rashidi alikuja sema "uliposema tumdhibiti sie tulijua unamaanisha...." Sasa sijui kama ni kweli.
Nyerere alisema Rashid na Jamal walikuwa viongozi Waadilifu sana
 
Nyerere alisema Rashid na Jamal walikuwa viongozi Waadilifu sana
Sokoine hakukubali Rashidi alikuwa mwadilifu kiasi hicho.

Na hata viongozi wengine maarufu wakati huo, kama Cleopa Msuya, Sokoine alimwambia Nyerere ni mafisadi wanatakiwa wawekwe ndani! Inasemekana Nyerere alichomkubalia ni kumwondoa Msuya kwenye UP, lakini sio kumweka ndani

Kwa mfano, kuliwahi kutokea skendo ya meli za serikali (Tacoshili nadhani) kuuzwa kwa bei chee kwa sababu watu walipewa mgao wao, na ikasemwa Rashidi alikuwa main actor hapo.

Kwa hiyo Sokoine alikuwa na maadui ambao walikuwa ni viongozi very powerful, kina Msuya, kina Kawawa nk.

Ni kweli Rashidi alikuwa very loyal kwa Nyerere. Mwadilifu? I doubt that. Ni sawa na Rasi Samia aseme Mwigulu ni waziri wangu mwadilifu sana ndio maana yupo hapo wizara nyeti. Utamwamini?
 
Sokoine hakukubali Rashidi alikuwa mwadilifu kiasi hicho.

Kwa mfano, kuliwahi kutokea skendo ya meli za serikali (Tacoshili nadhani) kuuzwa kwa bei chee kwa sababu watu walipewa mgao wao, na ikasemwa Rashidi alikuwa main actor hapo.
Inasemekana Nyerere alitaka awe Maarufu kwa muda mrefu
 
1713439275132.png


Angalia hii picha. Gari imegongwa pembeni, Sokoine alikuwa kiti cha nyuma. Hakuna mtu mwingine kwenye gari hii alikufa ila Sokoine tu

Ukiwa dereva maalum wa viongozi, ukaona gari inaingia barabarani bila tahadhari, hutagongwa squarely pembeni, utabalalizwa katika kuikwepa na labda mtaishia porini. Hii ni ajali ambayo Dube alipaswa kuwa anakatiza barabara sio anaingia barabarani. Labda walioitengeneza hawakufikiria hilo.

Na pia msafara wa Waziri Mkuu unakuwa na gari mbili hivi mbele. Yaani Dube hakuziona hizo wakati anataka kuingia barabarani, akaingia kati ya gari za mbele na za nyuma? Kwa sababu gari za mbele haziiachi sana gari ya Waziri Mkuu
 
Back
Top Bottom