johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Duh
Wakamsingizia Rashid kama vile wanavyomsingizia Naniliu ajali ya Lisu 🐼
Wakamsingizia Rashid kama vile wanavyomsingizia Naniliu ajali ya Lisu 🐼
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha kupayuka. Nyerere hakuwa mkomunisti. Hujui hata maana ya mkomunist unakuja kupiga kelele hapa. Na kwa taarifa yako, kuna wakati wazee wa Dar es Salaam walimwambia Nyerere wampeleke Bagamoyo Mlingotini akafanyiwe "huduma" na wazee wa Bagamoyo, alikubali. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na akili kuliko uwezo wako wa kufikiriNyerere Aaamini misukule😄😄😄😄😄mcommunist na mambo ya mitaani wapi na wapi ......uzi una kamba huuu
Inategemea, kama ni customized zinakuwa salama kabisa.Hata Mercedes za siku hizi?
Wengi walishakufa. Wapo wachache bado wako hai. Mmoja yuko kaskazini huko.Inasikitisha, sasa waliofanya hivyo na wao wako wapi? Hakika mafisadi ni watu hatari katika taifa. Hata JPM nina wasiwasi na kifo chake RIP.
Kuna sababu zilizofanya watu wamshuku Rashidi. Ni kweli Sokoine alimwona Rashidi kuwa nae ni fisadi tu, pamoja na Cleopa Msuya. Inasemekana wakati kina Rashidi wanalalamika sana kwa Nyerere dhidi ya Sokoine kwamba anapita kiasi, Nyerere aliwaambia sasa nyie pia si viongozi, kama mnaona anapita kiasi mdhibitini. Watu wanasema Rashidi alikuja sema "uliposema tumdhibiti sie tulijua unamaanisha...." Sasa sijui kama ni kweli.Duh
Wakamsingizia Rashid kama vile wanavyomsingizia Naniliu ajali ya Lisu 🐼
Source of information.....Niamini mimi bro.Mwaka huu kumekuwa na kumbikizi ya miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine, ambacho kiligubikwa na utata mkubwa, kukiwa na madai kwamba hakufa kwa ajali bali aliuwawa na watu ndani ya uongozi ambao walimwogopa sana.
Huenda ni kweli, kwa sababu wakati fulani Sokoine alitaka kumweka nguvuni kiongozi wa juu sana serikalini kwa kosa la ufisadi, na Nyerere ndio alimzuia akimwambia angesababisha mgogoro mkubwa wa kiuongozi. Sokoine alikubali, japo kwa shingo upande.
Hata hivyo, wakati Nyerere akiongelea kung'atuka na ikionekana wazi mrithi wa Nyerere angekuwa Sokoine, kuna viongozi walishikwa na uoga mkubwa juu ya hatima zao. Wengi waliona wazi kwamba siku Sokoine anaapishwa kuwa raisi basi milango ya jela ilikuwa wazi kwao, pamoja na wale ambao Sokoine alitaka kuwakamata na Nyerere akamzuia.
Kwa mfano, akihutubia Bunge pale Dodoma kabla ya kuanza safari ambayo ilimuua, Sokoine alikuwa ameweka ahadi kwamba akifika Dar es Salaam, alikuwa na list ya viongozi ambao walitakiwa kutupwa kikaangoni. Inaonekana Sokoine alitaka kwanza kuijadili ile list na Nyerere. Ndipo watu wanasema, akaliwa timing hata huko Dar es Saalam asifike.
Sasa katika mazingira ya ile ajali, ambayo kimsingi hayakuwa ya "head-on collision", Mercedes Benz walidai kwa maelezo yaliyotolewa juu ya ajali ilivyotokea, Sokoine hakupswa kufa. Na wakaenda mbali zaidi na kusema, wanataka walete wataalamu wao ili wachunguze, kama ni kweli Sokoine alikufa akiwa ndani ya gari yao ya Mercedes Benz, akiwa amekaa kiti cha nyuma, na kwa nini alikufa.
Sasa kumbuka gari aliyopata nayo ajali Sokoine ilikuwa customized na Mercedes Benz kwa ajili ya viongozi, yaani order za ikulu, kwa hiyo huwa zinatengenezwa maalumu kuwa na usalama zaidi kuliko gari ya kawaida. Kwa hiyo kwa Mercedes Benz hili la kusema Sokoine alikufa katika mazingira ya ajali kama ile, waliona ni kuchafua jina lao. Wakaomba waje kufanya uchunguzi, serikali ikawakatalia.
Sasa unajiuliza, kulikuwa na siri gani nyuma ya kifo cha Sokoine ambacho serikali ya Nyerere haikutaka zivuje? Kumbuka, Nyerere alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye hata angejua Sokoine ameuwawa, asingetaka ulimwengu ujue hilo. Kwake hadhi na heshima ya Tanzania vilikuwa vitu muhimu sana, na alikuwa tayari kutotoa ukweli wa jambo kama hilo ambalo aliona lingelifedhehesha taifa la Tanzania.
Kwa mfano, kuna kikundi kilimfuata Nyerere na kumwambia Mwalimu, Sokoine ameuwawa katika mazingira ya ushirikina, kachukuliwa msukule na wanajua nani walifanya hivyo katika viongozi wa taifa. Wakasema wanaweza kabisa kumrudisha hai Sokoine ikiwa watamuwahi kabla hajamalizwa kabisa! Nyerere akasema, mie naamini kabisa haya mambo ya msukule na najua yanafanyika. Na huenda ni kweli Sokoine kafanyiwa hivyo. Lakini sasa niambieni, mie baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba kijana wangu Sokoine amekufa, na nyie mkamrudisha, nitatoa tangazo gani jingine kwa ulimwengu, na huo ulimwengu utanionaje mimi na Tanzania kwa ujumla? Akasema kama mnataka kunisaidia, basi kama hajafa bado ni msukule, fanyeni afe kabisa ili hao waliomfanyia haya wasije wakamtesa.
Kwa kumkumbuka Sokoine, hebu jiulize, ikiwa leo Sokoine kwa muujiza fulani angefufuka na kuwa Raisi wa Tanzania, ni nani katika viongozi wetu waliopo madarakani milango ya jela ingefunguliwa kwa ajili yao?
Nyerere alisema Rashid na Jamal walikuwa viongozi Waadilifu sanaKuna sababu zilizofanya watu wamshuku Rashidi. Ni kweli Sokoine alimwona Rashidi kuwa nae ni fisadi tu. Inasemekana wakati kina Rashidi wanalalamika sana kwa Nyerere dhidi ya Sokoine kwamba anapita kiasi, Nyerere aliwaambia sasa nyie pia si viongozi, kama mnaona anapita kiasi mdhibitini. Watu wanasema Rashidi alikuja sema "uliposema tumdhibiti sie tulijua unamaanisha...." Sasa sijui kama ni kweli.
Sokoine hakukubali Rashidi alikuwa mwadilifu kiasi hicho.Nyerere alisema Rashid na Jamal walikuwa viongozi Waadilifu sana
Inasemekana Nyerere alitaka awe Maarufu kwa muda mrefuSokoine hakukubali Rashidi alikuwa mwadilifu kiasi hicho.
Kwa mfano, kuliwahi kutokea skendo ya meli za serikali (Tacoshili nadhani) kuuzwa kwa bei chee kwa sababu watu walipewa mgao wao, na ikasemwa Rashidi alikuwa main actor hapo.
Siye LY tumewakosea nini??...unafikiri humu kila mtu la saba...