Pre GE2025 Kigaila: Rais Samia hajaanzisha mradi wowote tangu awe Rais isipokuwa mradi wa mabango ya Mama anaupiga Mwingi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ila kweli ni kama hamna hata mmoja.
Hivi huyu Kigaila ndiye anayetaka kuwa KATIBU MKUU WA CHADEMA? Niliwahi kusoma tetesi kama hizo hapa JF.

Kama ni kweli, CHADEMA imekufa. Huyu ni punguani kabisa. CHADEMA msikiue chama chenu kwa kuwapa wendawazimu kuongoza chama. Du, Pengine Magu alifanya kweli, alinuia kuiua CHADEMA. Nafikiri imeshakufa.
 
Wanakopa pesa, wanazitafuna, wanazitumbua, deni linabaki kwa watanzania.
 
Unaposema ni mzee aachane na siasa. Jitazame kwanza wewe na wenzako ndani ya chama chenu. Then ndo urudi hapa kuandika.
Wakati miradi ikotekelezwa wao wanaingia barabarani.
Hivi dunia ya leo ni ya kuongea siasa tupu za mdomoni??
Kila kata nchi hii kuna mradi mpya uliopelekwa na Samia.
 
Zitaje kwa majina na eneo zilipo ili tukague kama hazikuwepo kipindi kilichopita, vinginevyo unadanganya
Usijitoe ufahamu Brother... ( Unajua kusoma na kuandika)
Tatizo mnakuja na hoja za kishabiki na sio kuwasaidia watanzania.

Mh Rais anaipambambania sana hii nchi anajitahidi sana. Naye ni binadam sio Mungu.
 
Ukichunguza ni kweli
 
Unajua nini, Nyerere alisema maadui wakubwa wa maendeleo ni ujinga, maradhi na umasikini. Lakini nadhani kuna adui mmoja tu wa maendeleo - ujinga, ambao ndio husababisha maradhi na umasikini. Watanzania wengi ni wajinga sana, na kwa sababu hiyo hatuwezi kuendelea. Mjinga anakamuliwa kodi kila mahali, anabanwa ni kodi ni kodi tu. Halafu akinunuliwa pipi kutoka sehemu ya hiyo kodi anatoa shukurani hadi kujigalagaza chini, hasahau hata kuuliza zaidi ya kuninunulia pipi fedha ulizonikamua umezipeleka wapi?
 
Kaanzisha bana asisingiziwe mama wa watu

1. mkwe waziri
2. Mwanae anawakilisha nchi bila cheo serikalini
3. Chawa chawa chawa kila kona
 
Waliisema miradi ya JPM haina tija
Walitamani Mama Samia aachane nayo
Hawaamini kama miradi hiyo mikubwa imeisha.
Heko mama Samia,hakuna kitu kikubwa utajivunia na kustaafu kwa Amani kama kumalizia miradi Ile mikubwa,ya kimkakati na yenye thamani ya matrilioni tena kwa kipindi ambacho miradi bado ilikua Michanga kabisa.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Watu wana matusi ya rejareja aisee
 
pesa zinatumika hovyo bila kujificha
 
Kigaila anaweweseka tu
Comrade jibu hoja!
Mwanaccm imara anapenda upinzani imara,mwanaccm legelege anauchukia upinzani wenye hoja!!!

Kigaila angesema na pkpk plus bajaji na miradi ya ujenzi wa madarasa na shule pia no miradi yake iliyokamilishwa!!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
 
Kigaila alienda kwao Ugogoni anapanda SGR anadhani mradi unaendelezwa na nani? πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Sina shaka ikiwa hii ndo namna wapinzani wanavyoweza kujenga hoja basi ccm njia nyeupe...sisi watanzania tunaopenda kuona mabadiriko ya kweli yasiyo ya kishabiki tutapata wapi kiongozi anayejitambua na asiye dictator sana mana udikteta Kuna mazingira ya kiuongozi ni mhimu..anayependa maendeleo ya vitu na watu yaende sambamba..yupo wapi, kajificha wapi ..mchana mwema
 
Kama Mama angeanzisha miradi mingine mipya ya kwake; lingetokea tatizo moja kubwa kwamba miradi aliyoikuta asingeweza kuimalizia

Mpaka hapa wapinzani wangempigia kelele kuwa ameihujumu miradi aliyoikuta na asingeweza kupata sababu ya maana ya kujitetea; wangemmaliza kisiasa
 
🀣🀣🀣🀣
🀣🀣🀣🀣
 
Hana maarifa ya kuendeeza miradi aliyoacha jpm. Badaka ya kuhakikisha hela inatoka ndani ya nchi kama alivyofanya Magufuki anakimbikia ushauri wa wapigaji na fisadi kukopa WB na ifm. Sijui hatambui vyombo hivyo ni vya kibiashara tu kwa nchi za kibeberu? Wanaojua watakwambia vyombo hivyo havimuachi mikono mitupu kigogo wa nchi anayesababisha nchi kukopa kwao kwa miradi ya isiyokua na tija kwa maendekeo ya nchi inayohusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…