Kigamboni haina maji inakuwaje yaliyopatikana yapelekwe mjini kabla ya wanakigamboni kupewa maji?

Kigamboni haina maji inakuwaje yaliyopatikana yapelekwe mjini kabla ya wanakigamboni kupewa maji?

Ifike sehemu viongozi muwe na aibu jamani na wakazi wa kigamboni hata kama niwapole!

1. Wananchi wa kigamboni wanaishi kama digidigi kwenye pantoni na hakuna kiongozi hata mmoja anaeguswa na hilo
2. Mabanda ya abiria kwenye pantoni hayana viti lakini hakuna anaejigusa Si Temesa, Si LATRA, Si mbuge wala mkurugenzi

3. Vyoo kwenye mabanda ya pantoni kipindi cha MAGUFULI walifuta tozo, lakini sasa ni malupo ili abiria atumie choo lazima alipie tena akiwa ndani ya banda!
4. Abiria wa pantoni wanalipa na wapo wa kutosha lakini vivuko ni vibovu balaa na pachafu utafikili wanavusha mifugo (No standard)!
5. Hakuna mkakati rasmi wa kulinda utu na ustaarabu wa abiria.
6. Msaada wa AZAM TAX wananchi wanashukuru, lakini Hakuna taarifa rasmi kwa wananchi kwamba AZAM ametoa huduma hiyo kwa makubaliano yepi, je ana mkataba upi wa zawadi au tenda yake ni ya mda gani! Kajitolea au kaombwa kwa makubaliano gani (Tunashukuru lakini wananchi wapeni taarifa-Updates)
7. LATRA Wekeni ruti ndefu ya usafili kuunganisha kigamboni na kinondoni ili kupunguza msongamano kwenye pantoni
8. Ingawa tiba ya kudumu kabisa pale ni kuweka daraja la chini pale kivukoni katika muundo wa spiral - sea under pass!

Yote tisa kumi Sasa mnataka kuibua mgogoro mwingine wa ishu ya maji kwa makusudi kabisa

Tone la maji la kwanza kigamboni linapelekwa mjini wakati wakazi wa kigamboni hawana maji tangu Uhuru hii ni dharau iliyopitiliza!

Siyo kwamba napinga maji kuvushwa mjini hapana, lakini je Wakazi wa kigamboni wamepatiwa hayo maji yenyewe?

Mwaka 2019 kwenye kampeni ya vyoo bora, kigamboni ilikuwa ya mwisho kutokana na ukosefu wa mtandao wa maji majumbani.

Visima vya maji kigamboni ndo kwanza vimekamilika sasa, Wananchi asilimia 95% hawana maji inakuwaje unazindua mradi kwa kuelekeza maji mjini kabla ya neema hii kuwafikia wanakigamboni kwanza?

Kama hoja ni upungufu wa maji mjini, kwa uzito huohuo ifahamike wanakigamboni wao hawana maji kabisa!
View attachment 2400944
Mnakaa mnaandika malalamiko ya kipuuz kila siku hapa ,wakati solution mnaijua , solution ni kuing'oa ccm madarakani , mmeshindwa ni bora mkae kimya tu , haya malalamiko hayana maana
 
Mnakaa mnaandika malalamiko ya kipuuz kila siku hapa ,wakati solution mnaijua , solution ni kuing'oa ccm madarakani , mmeshindwa ni bora mkae kimya tu , haya malalamiko hayana maana
Utaiong'oa CCM kama kisiki bila kuongea?
 
Utaiong'oa CCM kama kisiki bila kuongea?
Action ndio inayotakiwa , kama kuongea tushaongea sana ,unafikiri wewe ni wa kwanza kuleta hoja ya matatizo yanayomkabili mwananchi wa kawaida nchi hii ?
 
Action ndio inayotakiwa , kama kuongea tushaongea sana ,unafikiri wewe ni wa kwanza kuleta hoja ya matatizo yanayomkabili mwananchi wa kawaida nchi hii ?
Sawa toa maelekezo ya kiufundi
 
Back
Top Bottom