Kigezo cha Rais bora hakipimwi na wanyonge, Wanyonge hawaelewi chochote kuhusu siasa wala uchumi

Nafikiri hujaielewa .

Point sio kuwa wanyonge wakandamizwe, lakini ubora wa Rais haupimwi kwa kuwafurahisha wanyonge

Mfano akitokea Rais akasema wananchi wanaruhusiwa kuvamia hifadhi na misitu, wanyonge watafurahi sana, je huyo atakuwa rais bora?
Mfano population imeongezeka hawana Ardhi wala lkipato chochote utawaacha wafe na njaa wakati eneo la kulima lipo hiyo mbuga Utaona wanyama muhimu kuliko uhai wao?
 
Wanyonge ukiwauliza "katiba na umeme kipi bora?" Utasikia umemeéeee!! Hahahaha
Wako sahihi.wanachohitaji ni kutimiziwa mahitaji yao sio porojo za katiba au tume huru
 
Kuwajali wanyonge ni sifa ya kipekee haswa unapokuwa unapanda kimaisha na kupata utajiri. Ni sifa ya ubinadamu.
 
Wanyonge wanahitaji kukombolewa na Sio kusifiwa unyonge
 
Kwa taarifa yako hao Wakenya wako vizuri kuliko sisi, na wana uhuru wa kutosha kwenye kujieleza kuliko sisi tuliofubazwa kwa shuruti na ccm. Mabadiliko wanayoyataka ni kuboresha zaidi hatua waliyopo, ambayo ni maili nyingi kulinganisha na sisi. Kwakuwa ww ni mzee sitegemei utake mabadiliko kwani umri na mtazamo wako tayari umeshagota.
 
Huijui Kenya.
 
Kuwajali wanyonge ni sifa ya kipekee haswa unapokuwa unapanda kimaisha na kupata utajiri. Ni sifa ya ubinadamu.

Kuna kujali wanyonge, na kuwatumia wanyonge kuficha ajenda zako. Unapowajali wanyonge unawapa ajira. Sio kunyanyasa matajiri ili maskini wa kushangilie.
 
Wadharauni sana wanyonge lakini ipo siku mtajua umhimu wao.
 
Huijui Kenya.

Nimeishi Kenya, sasa sijui kama siijui kijiografia ama kisiasa? Na nina uwezo wa kupambanua mazingira yao na yetu na kujua ukweli. Ukiitazama Kenya kwa mtazamo wa kiccm utawaona wanakosea. Lakini wako vizuri kuanzia kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya na hata kisiasa kulinganisha na sisi wenye amani ya kwenye vitabu.
 
kweli
 
Hakuna kitu kinaitwa Chatto (International Airport) ila Geita Airport na IATA Code yake ni GIT. Unajikuta mjuaji kumbe haujui chochote. 🚮

Mimi sio rubani boss utegemee nitafuata code za kirubani, najua kuna Geita na Chato. Isitoshe sioni sifa yoyote ya kujua huo uwanja kwa hizo code unazotaka nizijue.
 
Ukisema uongo hakikisha unajua pia na ukweli wake😂😂😂. Natumia sana uwanja wa Chato na nimekuja Dar jumamosi narudi jumanne. Sijaona kufutwa kwa safari za ATCL kwenda Chato

Uko sahihi, kwenda kwenye hiyo route hakumaanishi kuna faida. Wanaweza wasifunge kwa sababu za kisiasa lakini hiyo route ni baadhi ya maeneo yatakayozidi kulipa hilo shirika hasara. Rejea mashirika mengi ya umma yalivyokufa kutokana na hasara kwani yaliendeshwa kisiasa nani si kwa nguvu ya soko.
 
Bonge la ukweli
 
Kuna kujali wanyonge, na kuwatumia wanyonge kuficha ajenda zako. Unapowajali wanyonge unawapa ajira. Sio kunyanyasa matajiri ili maskini wa kushangilie.
Unapowajengea majengo na kuagiza waishi humo miaka mitano ni ishara kubwa sana ya kuwajali.

Unaposoma watoto wao bure kabisa ni ishara nyingine ya kuwajali kwa vitendo.

Binadamu anaharibikiwa kwa ubinafsi wake na sio zaidi ya hapo.
 
Naona umepanic mpaka umeokota tu link na kuitupa hapa.
Mimi nipanic kwasababu ipi?

Kenya ukitoa Genge la Wanasiasa wanaomiliki Kenya tangu UHURU na Makampuni ya kimataifa ambayo yameifanya Kenya Kama Hub ya East Africa.

Mtu wa Kawaida anaishi Kama Yuko JEHANUM ya MOTO na hajui atajiokoa lini.
 
Unapowajengea majengo na kuagiza waishi humo miaka mitano ni ishara kubwa sana ya kuwajali.

Unaposoma watoto wao bure kabisa ni ishara nyingine ya kuwajali kwa vitendo.

Binadamu anaharibikiwa kwa ubinafsi wake na sio zaidi ya hapo.

Wanyonge ni hao tu kwenye hayo magorofa? Elimu bure aliirukia maana waanzilishi walitaka iwe bure mpaka chuo kikuu.
 
Mimi nipanic kwasababu ipi?

Kenya ukitoa Genge la Wanasiasa wanaomiliki Kenya tangu UHURU na Makampuni ya kimataifa ambayo yameifanya Kenya Kama Hub ya East Africa.

Mtu wa Kawaida anaishi Kama Yuko JEHANUM ya MOTO na hajui atajiokoa lini.
Kwani kuna tofauti na hapa kwetu? watu huko vijijini wanatumia maji na mifugo tena maji yenyewe ni tope tupu.
Makampuni ya kimataifa ndio hayo serikali hii ya ccm imekuwa ikizunguka duniani kuyaleta yawezekeze hapa nchini, huenda hujui mambo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…