Kijana afanya utani wa kutaka kumuua Rais Magufuli, aambuliwa kifungo cha miaka 2 jela

Kijana afanya utani wa kutaka kumuua Rais Magufuli, aambuliwa kifungo cha miaka 2 jela

Ameua kwa maneno akafungwa kwa vitendo... [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Wengine ndio SEHEMU zao za kupatia rizki
moja ya maeneo ambayo huwa sipendi kuzoeana au kusogea ni maeneo ya stend,sokoni,vijiwe vya kahawa,wapiga viatu kiwi,na wauza magazeti,kwani maeneo hayo wazee wa kazi wako wa kutosha mno
 
Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
Na kwa kasi hii hakuna mahabusu kukaa ndani zaidi ya mwezi mmoja. Ninahakika wote walioshtakiwa kabla yake sasa watapata hukumu zao kabla ya mwaka 2020, wakiwemo masheikh wa UAMSHO!!!!!!!!!!!!
 
mputa,
Kama unakiri kwamba hata wale askari walikuwa na kosa kwa mujibu wa sheria then nataka uniambie, kati ya huyo kijana na hao askari niliowataja ni nani mwenye alistahiri kupewa adhabu?, na kwa nini wale askari waliachiwa huru, kwa kutumia sheria ipi waliachwa huru ?, kwa nini huyu apelekwe jela ?, huhitaji elimu ya chuo kikuu kung'amua hili, Sijaona kosa la huyo kijana kufungwa, huyo kijana ni rasilimali alitakiwa kufanya kazi ya kuzalisha mali, kumuweka magereza ni kuongeza gharama za uendeshaji wa magereza kwenye nchi maskini kama hii, wenzetu walioendelea siku nyingi walishaacha kufunga watu magerezani kwa makosa ya ovyoovyo kama haya
 
magereza yanajaa kwa hukumu zisizo na kichwa
Na bahati mbaya sana wanalazimisha kupeleka watu magereza na wakati wanajua kabisa magereza nyingi kwa sasa hapa nchini zimejaa wafungwa na mahabusu zaidi ya uwezo wake wa kubeba lakini pia hazina uwezo hata wa kuwahudumia, mahabusu kwa mfano, anakuwa hajahukumiwa kwa hiyo kumuweka magereza ni gharama ya bure, kwani mwishowe huja kuachiwa halafu kama serikali mnakuwa mmeshaingi gharama za kumtunza, umaskini kwenye nchi hizi hautaisha, hizo fedha za kugharamia wafungwa zingeweza kuboresha pakubwa sana kwenye maeneo muhimu kama Afya na Elimu, Poor Africa
 
Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
Si amekiri kosa huyo zumbukuku?hakuna haja kumchelewesha
 
Ni kutia tu viboko anarudi kwenda onesha mpira
Wakuu wa mahakama zamani walikuwa na akili nyingi sana, kuna aina ya makosa mtu alikuwa anpewa adhabu (kifungo cha nje) anakwenda kwenye ofisi ya serikali iliyo karibu nae anapangiwa kazi ya kufanya kwa muda wote wa hukumu yake, hawa wa sasa wanatoa hukumu huku wanaangalia picha ya rais iliyoko ukutana wanaogopa kwamba huenda rais anawaona
 
miss zomboko,

Huyo Kijana ametoa som/fundisho kwa wengine ambao wanapenda sana kuropoka au kusemasema ovyo! SI vizuri kusema mbele ya watu maneno mazito kama haya!
 
Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
Huyo alikiri kosa,hapo ulitaka Mahakama icheleweshe kesi kwa vipi?
 
Hii ni nzuri sana. Acha akanyee debe huko ajifunze kuwa na nidhamu ya mdomo!

Hawa vijana wa siku hizi wanakaa vijiweni kuropoka ropoka tu na kushadadia ngono nzembe!

Leo kaingia kingi. Akitoka huko ataziba hilo domo na supagluu.

Bravos!
 
Sio mmoja. Imeripotiwa kuonekana kama ni kundi zima la raia 'wema'! Bila shaka hilo nalo lina mantiki yake.
Sio kundi, ni lofa mmoja mlamba miguu ndie alienda kutoa taarifa kwa polisi, Vijana wa ccm waliua aliyekuwa mwenyekiti wa chadema geita, polisi mpaka leo hawajakamata hata mtu mmoja
 
Ni kosa kisheria jamani, hata wewe ukitishwa kuuawa nenda kashtaki.Mimi nimewahi kumshtaki mtu kwa kunitamkia kwamba ataniua ila badae nikamuonea huruma sikwenda mahakamani mpaka kesi ikafutwa. Pamoja na hayo Rais ni nembo ya Taifa unatishia vipi kumuua hata kama unatania.

Tuache ushabiki wa kijinga.
John mwenyewe si anatishia kuwapoteza watu hadharani!
 
Back
Top Bottom