TANZIA Kijana aliyempiga makofi Rais Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

TANZIA Kijana aliyempiga makofi Rais Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Huyu Mwinyi nae alipenda kupigwa, uzee wote huo bado anahimiza kondom za mini sasa?
Soma hapa uelewe zaidi
Screenshot_20190602-223102.jpeg
 
Huu uzi umenifanya nijue watu wengi ni wajuzi juzi huku JF. Yaani hili tukio kumbe kuna watu hawakulijua. Ila halikuwa kofi wala kibao ni jamaa alimdokoa kidogo tu mzee mwinyi, kama vile tumbili [emoji626]

RIP Bro
Ndio hivyo mkuu
 
Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na alipe kwa kheri zake. Ameen.
 
Mungu amuhifadhi sehemu salama
Pole kwa wafiwa

Mabibo Loyola nimaeneo yangu ya kujidai
 
[emoji2960][emoji2960]
Kupiga kofi ni kule kupiga kiganja kimoja cha mkono na kingine kama katika kushangilia au kumtanabahisha mtu, hicho ndiyo kiswahili fasaha na si kupiga makofi, na kupiga kibao ni kumpiga mtu kwa kutumia kiganja cha mkono (kwenye tumbo la kiganja) shavuni, na ukimpiga mtu shavuni kwa kutumia nyuma ya kiganja hicho kinaitwa kibao cha kelb.
 
Kule alikopelekwa baada ya kupiga sirikale...ndio slimoanzia huo ugonjwa!
Mengine tujifunze kumezea tu!
maana ndio vile...kaisari naye yupo...
Uchonganishi kama huu unakusaidia nini mkuu? Waliosoma naye wanasema dishi lilikuwa linahama wakati mwingine, kuna member hapa kasema alisoma naye IFM alikuwa akiingia class anazima AC mara anzima taa kisha huyooo anatokomea mtaani.....
 
Mara ya mwisho nilimuona miezi miwili iliyopita, nilipaki gari pale IFM posta, akaja akaanza kukunja side mirror kwa nguvu. Nilikosa cha kumfanya kwa muda huo, maana alikuwa amerukwa na akili. Niliwauliza wenyeji huyu chizi katoka wapi, ndiyo wakanipa historia yake.
Daaah, kumbe mshikaji ameshafariki!!!
R.I.P
Mkuu, naomba nikupongeze kwa kumiliki mkoko Darisalama....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom