Hujambo? Sasa tunapopambana na ukatili Sababu ya watu wanaoshindwa kudhibiti hasira sijawahi hata kukusikia. Leo mtu mmoja amezishinda hasira, hajafanya ukatili, katuachia amani, tunataka tumpongeze, napo unapinga.
Kwa kuwa hata kwenye mapambano ya kudhibiti na kutokomeza ukatili sijawahi kukusikia, nadhani maoni yako nayo nimeyasoma halafu siyatekelezi, tuzo tutampa tu Ili wengine waone kuwa, inawezekana kudhibiti hasira na kutofanya ukatili wa kijinsia.
Kumbe wewe wasema ni mlevi na alilewa? Halafu akaishinda hasira? Na walevi wengi hushindwa na hasira na kufanya ukatili? Basi kumbe huyu ni Shujaa zaidi, anastahili PONGEZI zaidi.
Haya asubuhi njema na heri kwako.