Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kwani kabla ya sendoff hamkujua ni mlevi au ni unafki tu, kwa kauli za ajabu ati ametuaibisha.

Huyo mke alotaka kumuoa hajui mumewe anakula vyombo, mbona kamkubali, mbona mahari ya mlevi wameila!! ??

Acha chapombe apewe tuzo, na bila shaka tuzo inakua na kipozeo kidogo, hicho akitumie kugida lager nyingine akili ikae sawa
Bora muulize nyie ndugu zangu kuhusu je awali haya madhaifu hayakujulikana ?. Mimi nauliza huenda labda kuna sentensi fulani naisahau ndiyo maana wengine wanakuwa hawanielewi. 🙏🏽🇹🇿
Mseme nyie ndugu zangu mjadala wa kijamii ni nguzo ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zetu.

Ukatili wa Kijinsia unatuumiza sisi sote kwa namna moja au nyingine. Mtu mmoja anapouepuka ina tija Sana.
 
Kweli kabisa ndugu yangu. Kitu alichofanyiwa ingekuwa wengine wale wanaotawaliwa na hasira, hekima haipo, mtakubaliana nami kuwa Leo tungekuwa tuna stori ingine.

Tunapoisihi jamii kuepuka ukatili wa kijinsia na walau mmoja akaishinda hasira kwa hekima, inapendeza Sana kumtia moyo na kutambua hekima yake. Huenda ikawa chachu ya mabadiliko kwa wengine 🙏🏽
Nilipoona like za kutosha ghafa nimerudi kuangali mchangiaji nilikuwa sahihi
 
Yule mwamba aliyenyimwa mke siku ya harusi kwa kisingizio cha kwenda kwenye send off akiwa chakari,amepewa tuzo.

Amepewa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na waziri Doroth Gwajima

Kwa kweli jamaa anastahiki tuzo kweli maana mimi mwanamke anikatae siku ya harusi nyumba yao ningeichoma moto

Hongera sana kwako mheshimiwa waziri

View: https://youtu.be/45RcMjUciIw?si=6d_1XalRNMnEpd5j

Hongera Mh. Waziri wetu Mama Gwajima, tunakupenda sana
 
Kwani kabla ya sendoff hamkujua ni mlevi au ni unafki tu, kwa kauli za ajabu ati ametuaibisha.

Huyo mke alotaka kumuoa hajui mumewe anakula vyombo, mbona kamkubali, mbona mahari ya mlevi wameila!! ??

Acha chapombe apewe tuzo, na bila shaka tuzo inakua na kipozeo kidogo, hicho akitumie kugida lager nyingine akili ikae sawa
Kama uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo,basi endeleeni tu kutoa tuzo kwa walevi ili kujenga jamii iliyo bora na yenye maadili mema.
 
Pole Sana na hongera Sana kwa hekima, PM au sms 0765345777
Mimi swala langu Huwa ni Moja,kazi hasa ya Wizara hii ya Makundi maalumu Huwa ni ipi?

Ukirejea Mitaani Kuna maelfu ya walemavu hawajatambuliwa,Wagonjwa wa Magonjwa Sugu wanatembea na kadi na barua za Ustawi wa Jamii kuomba omba ,

Watoto wa Mitaani(hapa I can spare).

Ushauri: Nyie Wizara ya Ustawi wa Jamii Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,fanyeni kuratibu Zoezi la kuwatambua watu wote wenye ulemavu wa kudumu,watu wote wenye magonjwa Sugu na wasio na uwezo wa matibabu then mlete gharama za kuwatibu,mpange Bajeti na mlete kwenye jamii kuchangia kama vile zile kampeni za Madaktari wanawake,Mabenki nk wanavyofanya kupata hela za kusaidia wasiojiweza.

Hii ya kuwapa watu barua wanazunguka unakuata ana uvikbe mkubwa anasaiidiwa buku buku hamuwasiadii,chukua huu ushauri utakuja kunishukuru.
 
Kama uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo,basi endeleeni tu kutoa tuzo kwa walevi ili kujenga jamii iliyo bora na yenye maadili mema.
Hatutoi tuzo kwa walevi, hiyo ni content yako wewe. Sisi tunatoa ya "...bila jazba inawezekana"

Wewe hiyo content ingine yako tu ndugu yangu sisi huko hatupo. Uwe na asubuhi njema.
 
Mimi swala langu Huwa ni Moja,kazi hasa ya Wizara hii ya Makundi maalumu Huwa ni ipi?

Ukirejea Mitaani Kuna maelfu ya walemavu hawajatambuliwa,Wagonjwa wa Magonjwa Sugu wanatembea na kadi na barua za Ustawi wa Jamii kuomba omba ,

Watoto wa Mitaani(hapa I can spare).

Ushauri: Nyie Wizara ya Ustawi wa Jamii Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,fanyeni kuratibu Zoezi la kuwatambua watu wote wenye ulemavu wa kudumu,watu wote wenye magonjwa Sugu na wasio na uwezo wa matibabu then mlete gharama za kuwatibu,mpange Bajeti na mlete kwenye jamii kuchangia kama vile zile kampeni za Madaktari wanawake,Mabenki nk wanavyofanya kupata hela za kusaidia wasiojiweza.

Hii ya kuwapa watu barua wanazunguka unakuata ana uvikbe mkubwa anasaiidiwa buku buku hamuwasiadii,chukua huu ushauri utakuja kunishukuru.
Hujambo? Changamoto yako moja husomi taarifa za wizara na hujaelewa wizara zenyewe ziko ngapi. Kwanza ufahamu kuwa, kuna wizara rasmi ya wenye ulemavu inaitwa wizara ya kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu. Iko ofisi ya Waziri mkuu na waziri wake yupo, nenda ka google.

Ukishafanya hilo, nenda kasome hotuba ya bajeti yetu tarehe 17 Mei, 2024. Utaona wizara hii ukubwa wake na majukumu yake na mipango yake na mikakati yake na mafanikio yake.

Baada ya hapo, soma na hotuba za bajeti za wizara mbalimbali, kisha uje sasa tujadili hoja kwa hoja tafadhali.
 
Kwakweli mama hongera sana mimi siko kwenye hii mada ya leo ila nakupongeza kwa ujasiri wa kuwa mitandaoni kwa uwazi bila kujificha huku ukipokea maoni yote hata yale mabaya. Tunao mawaziri wengi humu ila wengi akiandika uzi ndio harudi tena kujibu.Hongera sana
Hujambo? Ahsante Sana kwa Pongezi. Mimi nipo na nitaendelea kuwepo hata baada ya uwaziri kwani ni vizuri kushirikiana na jamii daima.

Kwa sasa jamii yangu ninayoihudumia kuanzia wale wa ardhini hadi wa humu online wote ni saiti zangu za kazi.

Hata mtu akipanga kuniudhi, kwanza nitamuombea kwa Mungu wa mbinguni na kumjibu kwa haki tu. Akinisingizia jambo nitamfafanulia ukweli ulivyo na mengine ya kunitoa mstarini nitamkwepa na kumwachia yeye ahangaike nayo.

Mwenyezi Mungu ni mwema wakati wote, tuendelee kushirikiana 🤝
 
Yule mwamba aliyenyimwa mke siku ya harusi kwa kisingizio cha kwenda kwenye send off akiwa chakari,amepewa tuzo.

Amepewa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na waziri Doroth Gwajima

Kwa kweli jamaa anastahiki tuzo kweli maana mimi mwanamke anikatae siku ya harusi nyumba yao ningeichoma moto

Hongera sana kwako mheshimiwa waziri
Hio tuzo ina thamani ya kiasi gani ama ni maneno matupu😂
 
Back
Top Bottom