Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Ukijadiliana na nyapara madhara ya ndoa.
Ukifanya uhalifu unashtakiwa kwa sheria.
Binafsi simtazami huyo kijana kama shujaa anayestahili tuzo kwa kutokufanya uhalifu baada ya kuadhibiwa kwa makosa yake ya kutoheshimu wazaza wa mchumba wake.
Halafu naye na wapambe wake wangeamua vinginevyo wakaanzisha vurugu na kuumizana wote humu mngekuja na maswali waziri au wizara ina mpango gani ukatili umezidi. Tukihamasisha utulivu na kudhibiti jazba kwa mifano hai napo hamtaki...
 
Halafu naye na wapambe wake wangeamua vinginevyo wakaanzisha vurugu na kuumizana wote humu mngekuja na maswali waziri au wizara ina mpango gani ukatili umezidi. Tukihamasisha utulivu na kudhibiti jazba kwa mifano hai napo hamtaki...
Katika hili sikusapoti Mh waziri ila hongera kwa kazi nzuri katika mengi unayoyafanya kwa nchi yako.

Mambo ni mengi unayofanya hili la tuzo kwa mlevi asiye na mipaka ni moja ukilinganisha na mengi mazuri mnayofanya hapo wizarani. Tusikae sana hapa kwa mlevi wetu, keshapokea tuzo yake.
 
Yule mwamba aliyenyimwa mke siku ya harusi kwa kisingizio cha kwenda kwenye send off akiwa chakari,amepewa tuzo.

Amepewa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na waziri Doroth Gwajima

Kwa kweli jamaa anastahiki tuzo kweli maana mimi mwanamke anikatae siku ya harusi nyumba yao ningeichoma moto

Hongera sana kwako mheshimiwa waziri

Hongera kwako mwamba uliyekataliwa siku ya harusi
Hiyo kitu si rahis kama watu wanavyodhani, especialy society yetu ambayo haina huruma na mwanaume akipatwa na matatizo

Nampongeza the guy jinsi ame handle hiyo heart break, else tungekuwa tunaongelea kesi zingine za mauji
 
Alafu mnaosema jamaa sijui alikua chakari mlimsikia yule mwanamke wakati anahojiwa? We mwanamke ana kiburi dunia hakuna alafu pembeni kuna mama yake ndio anamjaza maneno kabisaaa
Bora wewe unayefuatilia pande zote, tuendelee kuwavumilia watoa maoni kwa huku wamesikia upande mmoja tu. Ndiyo Dunia yenyewe imeshajiweka hivyo
 
Hiyo kitu si rahis kama watu wanavyodhani, especialy society yetu ambayo haina huruma na mwanaume akipatwa na matatizo

Nampongeza the guy jinsi ame handle hiyo heart break, else tungekuwa tunaongelea kesi zingine za mauji
Ingetokea Tarime kanda maalumu ingekuwa vita
 
Namnukuu maneno alivyozungumza baada ya kufanya sherehe ya harusi pekee yake bila bibi harusi kutokea alisema

"“Kupata na kukosa yote ni sehemu ya maisha, cha msingi sana ikiwa kama Mtu unaweza kusherehekea na kufurahia ukipata basi ni vizuri pia hata ukikosa pia usherehekee na kufurahia kwa sababu mpango wa Mungu yeye ndio anayejua” amesema Edward Futakamba.
 
Kweli kabisa ndugu yangu. Kitu alichofanyiwa ingekuwa wengine wale wanaotawaliwa na hasira, hekima haipo, mtakubaliana nami kuwa Leo tungekuwa tuna stori ingine.

Tunapoisihi jamii kuepuka ukatili wa kijinsia na walau mmoja akaishinda hasira kwa hekima, inapendeza Sana kumtia moyo na kutambua hekima yake. Huenda ikawa chachu ya mabadiliko kwa wengine 🙏🏽
Sas hiyo ni Tuzo au kifuta ‘machozi?’
Au Tuzo imepata tafsiri mpya?
Amepewa tuzo kwa kukimbiwa? Kwanini amekimbiwa?
Baada ya kukimbiwa alitakiwa achukue hatua ipi na yeye akachukua ipi? Je, ni kwa sababu ya ujasiri, maturity au udhaifu?
Kama alitarajiwa kuchukua hatua fulani lakini hakuichukua hatua hiyo na wewe ukamzawadia, tafsiri yake ni kwamba ndani ya jamii kuna tatizo kubwa sana. Je umefanya interventions zipi kama jitihada za kuiokoa jamii dhidi ya hilo tatizo? Au tutarajie utalitokomeza tatizo kwa njia ya Tuzo?
 
Kumbe wewe wasema ni mlevi na alilewa? Halafu akaishinda hasira? Na walevi wengi hushindwa na hasira na kufanya ukatili? Basi kumbe huyu ni Shujaa zaidi, anastahili PONGEZI zaidi.

Yani Waziri unatoa tuzo huku hujui kwamba mhusika alikuwa kalewa ? ?

Unawezaje kulivalia njuga suala ambalo hujapewa comprehensive briefing of all the relevant facts kabla ya ku act in behalf of government ?????

Do your homework, for one. And for two, badala ya tuzo kwa walevi eti wamedhibiti hasira tunataka u address the more substantive and pressing issues za ukatili wa kijinsia.

Afande aliye mastermind dada wa Yombo Dovya arepiwe mtungo bado yuko jeshini ? Tuanzie hapo kwanza.

If you got balls to fight gender cruelty mshauri Commander in Chief amwagize Chief of Defense Forces and Director of Public Prosecution wamlete mahakamani afande aliyeagiza the unspeakably brutish, caught-on-camera, nation-jolting gang rape and sodomy of the Yombo Dovya woman.

So far umesema nini kwenye hilo ? Least you could do is issue a categorical condemnation and promise to bring the dastardly criminal officers of JWTZ to justice.
 
Mh waziri shkamoo,bila kukuchosha naomba nijaalie chochote kwenye lipa namba ya tigo 7410514,sijatia kitu kinywani kwa saa 36 zilizopita,nawaza kujitoa roho tu,hata kazi ya kubeba tofali nanyimwa,natanguliza shukurani
Jifunze kudhibiti njaa mkuu! Kwani waziri asingekuja kucomment ungemuomba nani??
 
Mume mtarajiwa anaenda kwenye send off akiwa kalewa chakari! Hii sio dalili njema,ikiwa siku muhimu kama hiyo kalewa chakari,itakuaje huko kwenye maisha ya ndoa?

Hivi kuna mtu humu anaweza kumuozesha binti yake kwa mume aliyekuja kwenye send off akiwa kalewa chakari? Hiyo ni heshima au dharau kwa familia ya mke mtarajiwa?

Amepewa tuzo coz hili tukio limeangaliwa upande mmoja,ingekua ni mimi ndiye mwenye mamlaka,hiyo tuzo ningewapa familia ya mke mtarajiwa na sio huyo mlevi.
Kumuozesha kwa mlevi ni jambo la kwanza,. Jambo la pili ni mlevi kutokulipa kisasi kwa kunyang'anywa make,, hivo mlevi kapewa tuzo kwa kutokuruhusu pombe na hisia zimwendeshe Kisha amjeruhi bibi harusi na baba mkwe ,. ,,
 
Back
Top Bottom