Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Huyo mlevi hajadhibiti hasira zozote hapo coz ametambua kosa alilolifanya,hata hao jamaa zake itakua waliondoka kwa fedheha kubwa sana huko ukweni,

Unakutwa na kosa ambalo na wewe unajua kua hili ni kosa umefanya,hizo hasira za kutaka kulipa kisasi zinatoka wapi?

Mtu aliyelelewa kwenye maadili mema au anayetoka kwenye familia inayojitambua,hawezi kwenda kwenye send off akiwa kalewa chakari,

Root cause ya yote hayo ni jamaa kwenda akiwa kalewa chakari full sto

Tuchukulie maoni yako yako sahihi, je baada ya pombe kwisha? Mbona sasa inawezekana kumbe kutawala hasira kisa aibu? Ingekuwa hivyo je hawa wanaozomewa kabisa kwa kosa moja na kesho wanafanya hilo hilo huwa inakuwaje? Eti...
 
Mwanangu hujambo? Maisha yanaanzia pale unapoamua kuachana na stress zisizo za lazima na kukubaliana na walimwengu wanavyokuona ingawa wao pia hawapendi uwaone unavyowaona, basi unajikuta na amani zako na wao na amani zao maisha yanaendelea😄
Hongera na pole na kazi mama. Nimefuatulia mjadala wote, kilicho ni furahisha ni vile umemudu kujibu kila comment Kwa upole na ustahimilivu, hata kwa zile zilizokuwa kinyume na mtazamo wako.
 
Hongera na pole na kazi mama. Nimefuatulia mjadala wote, kilicho ni furahisha ni vile umemudu kujibu kila comment Kwa upole na ustahimilivu, hata kwa zile zilizokuwa kinyume na mtazamo wako.
Ahsante Sana mwanangu. Mungu alishanipa neema ya ukomavu wa kuyabeba yote, nanyi nawaombea neema hiyo isiwapungukie. Niko kote na mijadala na jamii yangu, wakinipasua pasua na kunibomoa pasipo haki nawaombea tu napita zangu.

Dunia ya Leo tumuombe Mungu neema ya hekima na ustahimilivu. Vinginevyo unaweza jikuta mpweke Sana kwa kujitakia stress za maneno ya watu ambazo kimsingi inawezakana kabisa kuepuka ukabaki kwenye mstari.
 
Amina mama. Mungu na azidi kukuongoza, nikutakie kila lenye heri katika majukumu yako.
 
Unafikiri mwanamke hajui kama mchumba wake ni mlevi!?

Wameachanishwa,hawajaachana,naamini hivo , !?
Kwenye maisha ya Mwanaume na Mwanamke wanapoishi pamoja,hua kuna siri zao za ndani ambazo wao kama wao hua hawataki zitoke nje,kwenye ndoa kuna siri nyingi sana ambazo zinabaki kua ni siri za ndani,

Hata kama Mwanaume alikua mlevi,ila kitendo cha kulewa chakari siku ya send off hakuhalalishi ulevi wake wa siku zingine,

Tuchukulie mfano,wewe kama wewe,unaweza kua unalewa ila siku ya kwenda ukweni utajiweka kiheshima na kwenda ukiwa na akili zako timamu,

Huwezi kwenda ukweni ukiwa umelewa chakari au kwenda kwenye siku muhimu kama hiyo ukiwa umelewa!

Ni familia ya kijinga tu ndio inayoweza kumvumilia Mwanaume aliyelewa chakari siku muhimu kama hiyo.
 
Tuchukulie maoni yako yako sahihi, je baada ya pombe kwisha? Mbona sasa inawezekana kumbe kutawala hasira kisa aibu? Ingekuwa hivyo je hawa wanaozomewa kabisa kwa kosa moja na kesho wanafanya hilo hilo huwa inakuwaje? Eti...
Muheshimiwa weka swali lako vizuri,sijalielewa kabisa,kingine nakupongeza kwa kutilia maanani maoni yangu,Big up sana kwa hilo.
 
Hakuna mzazi atavumilia hiyo dharau. Unamkabidhi binti kwa mlevi? Serious? Kalewa chakari? Hata kuheshimu tu hiyo siku moja muhimu imeshindikana? Kama ni wazazi wameshinikiza Walikuwa sahihi kabisa. Kama wanapendana sana wakafunge ndoa bila hizi taratibu za sendoff.
Kulewa ni "involuntary action"...zimemzidia bahati mbaya na inatakiwa tutambue kwamba kulewa sio kosa suala inatakiwa ni kuji-control kabla hujanywa, ukute huwa anapiga bia mbili tatu anakuwa fresh ila siku hiyo ya harusi mwili ukakataa.

Tutamhukumu tu kama kwenye hiyo sendoff hakukuwa na kilevi lakini kama kilevi kilikuwa ni mojawapo ya kinywaji Kwa wageni waalikwa basi itoshe kusema kwamba mtu yoyote inaweza kimtokea hiyo Hali ya kuzidiwa kilevi
 
siri zao za ndani
Hizi Siri ndio zitasababisha waendelee kimyakimya, wazazi Wana nafasi ,ila linapokuja swala la kupendana hekima inahitajika sana, kama Binti aliamua mwenyewe ni sawa ,ila naamini ni kwa kiasi kidogo sana, pakubwa wameamua ndugu,, , kwenye kuachana ,anayeachwa ndio Huwa na reaction ya hatari kuliko anayeacha, inaweza Kuta jamaa tuzo akachukua alafu baada ya muda akachanganyikiwa na kuchanganyikiwa, so kumpa moyo ni muhimu bila kuangalia alipokosea,mana Tayari kashakosea ,Sasa ukiendelea kumlaumu anaweza akaamua kufa kabisa , ,,,,,kwa ufupi Upendo ni neno Pana sanasana ! Upendo huvumilia,. Upendo hufariji, na Upendo unakuja kuwa na maana zaidi huku kwetu Duniani kwa sababu si makazi ya malaika,. Ukute mi na wewe tulitakiwa tuwe tulishaachwa kwa sababu tuna kasoro Fulani,
 
Ahsante Sana mwanangu. Mungu alishanipa neema ya ukomavu wa kuyabeba yote, nanyi nawaombea neema hiyo isiwapungukie. Niko kote na mijadala na jamii yangu, wakinipasua pasua na kunibomoa pasipo haki nawaombea tu napita zangu.

Dunia ya Leo tumuombe Mungu neema ya hekima na ustahimilivu. Vinginevyo unaweza jikuta mpweke Sana kwa kujitakia stress za maneno ya watu ambazo kimsingi inawezakana kabisa kuepuka ukabaki kwenye mstari.
Mh Waziri, sasa huyo mwanaume kwanini asilipwe na familia ya mwanamke kwa kupotezewa muda na kutozwa mahari isiyofanya kazi?
 
Back
Top Bottom