Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Acheni kuropoka ropoka hovyo...hii nchi ya utawala wa sheria huyo Samwel na wenzake jela inawahusu .....haki ya huyo kijana itapatikana mahakamani....tabia hii lazima ikomeshwe ya kuua wananchi hovyo hovyo
 
Nani anaropoka? Watu wamewachoka na ukibaka! Nikuulize[emoji116][emoji116]
Je, alikuwa kibaka au si kibaka?
 
Watoto wengi wa uswahili Wana malezi mabovu sana wengi tu wanawatukana had wazazi wao kwa kifupi wanadekezwa sana na hata wakifanya wizi wazaz wanawatetea,
Sungusungu wengi ni vijana wenzetu wa mtaani wanamjua kibaka mmoja mmoja na machimbo yao,
Ushauri wangu ni kuwa wazazi muwalee watoto wenu vizuri maana hata ukiwazuia sungusungu wasiwauwe wapo wananchi wenye hasira kali watamchoma Moto siku moja.

Polisi wana tabia moja wakiskia Kuna kibaka kakamatwa mahali huwa wanachelewa makusudi siyo kwamba hawawez kuwahi ila wanafanya hivyo ili mmalizane nae wao waje wabebe maiti tu maana hata wao hizo kesi zimewachosha.
 
Leo nimegundua siri hii baada ya muda mrefu sana.
 
Acheni kuropoka ropoka hovyo...hii nchi ya utawala wa sheria huyo Samwel na wenzake jela inawahusu .....haki ya huyo kijana itapatikana mahakamani....tabia hii lazima ikomeshwe ya kuua wananchi hovyo hovyo
[emoji3][emoji3][emoji3]naona unatetea mitaji yako pole sana,jiandae unafuta wewe kuuwawa
 
Nyinyi waropokaji bado hamjanipa kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia sheria mkononi....kwa akili zenu fupi nini kazi ya Polisi ,mahakama na magereza?
 
Suchak ongea kwa hoja...sheria ipi inaruhusu sungu sungu waue?

Baada ya kuuawa Jongo utafuata wewe......
 
komandoo yosso walitutesa sana, fikiria mtaani mnalinda sungusungu watu 10 hadi 12 halafu wenyewe wanakuja 40 wana visu, mapanga bisibisi n.k...
Mkuu wala sio uongo hawa jamaa walitutesa sana, kulikuwa na kundi lingine linaitwa kambi ya jeshi,,, wanaofanya huo uhalifu ni watoto ambao wanajulikana isipokuwa wazazi wao wanawatetea,, ila wajue siku hizi zama zimebadilika na raia washachoka, matokeo yake ndo kama haya, alafu mtu anakuja kuleta malalamiko jf,,,
 
Duh,kwa hizi comments za humu ndani ni wazi hata huyo mama Samia anayeombwa aingilie kati atakuwa upande wa Sungusungu
 
Kwa akili zenu duni mnaowatetea hawa wapuuzi sungu sungu vyombo vya sheria tuvifute?

Tuwaache sungu sungu wakichukua sheria mkononi?

Kwa hiyo hata mafisadi,wauza madawa ya kulevya, majambazi,wahujumu uchumi tuwaachie sungu sungu wawaue?

Acheni ujinga na upumbavu...kwa sababu yoyote sungu sungu hawapaswi kuwa juu ya sheria.
 
Suchak ongea kwa hoja...sheria ipi inaruhusu sungu sungu waue?

Baada ya kuuawa Jongo utafuata wewe......
Pole kwa kufiwa na kibaka wako...wafundishe na wezi wengine kua mtaani wananchi wana torati yao. Toto liwe jizi alafu uje usumbue kuhusu sheria ? Kwani nduguyo huyo alikua anaiba kwa sheria zipi za nchi? Mtaani ukizingua watu watatumia torati ya mtaa. Malezi mabovu na kuendekeza anasa ndio yanafanya vijana wa hovyo kua na tabia za ajabu ajabu kama hizi.

N.B Vibaka wanaroho ngumu sana usiombe kukutana nao kwenye kona zao. Walimsababishia jamaa yangu ulemavu wa kudumu mpaka leo. Mtu unatafuta kwa jasho lako alafu wao(vibaka) waje kukushambulia kwa mali zako halali kabisa? Wacha wapigwe moto tu jamii itakua salama. Mambo yakuwapeleka polisi ndio yamepelekea kushamiri kwa vitendo hivyo...kibaka anapelekwa leo Polisi keshokutwa yupo mtaani anaendelea na tabia zake. Akifa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali ni funzo tosha kwa vibaka wenzie.

"Action speaks more louder than words"
 
Msakuzi huru kama una hasira sana nenda kaue mafisadi waliokufanya uishi maisha mabovu, au nenda kaue wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya wanaoharibu vijana wa Tanzania.

Acha ujinga.
 
Msakuzi huru kama una hasira sana nenda kaue mafisadi waliokufanya uishi maisha mabovu, au nenda kaue wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya wanaoharibu vijana wa Tanzania.

Acha ujinga.
Nijibu! Hivi ni kweli huyo kijana alikuwa kibaka? Au hakuwa kibaka?
 
Unatetea kwa sababu huo msiba umekugusa moja kwa moja yani ukiangalia kwa kina inaonyesha kabisa una kahusiano na huyo kibaka aliyestaafishwa lakini nikukumbushe tu hakuna watu wanakera na kurudisha watu nyuma kama hao,hivi uliwahi kuwaza wangapi wamebakwa,kuuawa,na kutiwa ukilema na hao unaowatetea?ushawahi hata kutoa msaada au ushauri au hata kuanzisha uzi humu kulaani tu? Jibu unalo na hapo mtaani kuna vijana wangap,kwanini target awe huyo unayemnadi hapa? Pole najua hakuna mtu mbaya katika familia najua unasikia uchungu sana kwa sababu una unasaba nae ila ungetaka kumsaidia ungemuonya na kumkanya tangu mwanzo wewe pia unapaswa kulaumiwa hapo.Pole sana dada
 
Hivi komando Yosso alikuwa nani hasa?
Komando yosso sio mtu bali ni kundi la vijana wakabaji liliotikisa miaka ya mwanzoni mwa 90s
Wengi wao wakiwemo vijana wa kutoka maeneo hayo ya mabibo mpakani,mburahati na manzese,,, kundi hili lilisambaratishwa baada ya kuingilia kati aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa kipindi hicho ndugu Augustin lyatonga mrema,,, yani hawa jamaa walikuwa wanakaba mchana kweupee
 
Nasemaje J4 kama anavojiita bado anawenzake watano ambao aliwataja nao watatafutwa mmoja baada ya mwingine wote wafe mabibo, manzese, madoto, firstinn, kigogo ruhanga, tanesco, hadi kigogo roundabout zibakie salama mambo yaanze upya hakuna kifungu wala nini lazima watembee wakivuja damu hao madogo
 
Back
Top Bottom