Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Mastakiraka jaribu siku moja kuua mtu kisa amekupora simu yako.Ikiwa mtu huyo hana silaha.Jela inakuhusu.
 
Wanatusumbua sana hao,,, wanakaba wazi wazi kabisa alafu mama zao wanawatetea,,, mi nikajua labda huyo dogo anakaa mbezi, kumbe mabibo,, huyo kibaka tu,, maeneo kama mabibo,mburahati,kigogo, manzese, tandale, mwananyamala, Argentina na kagera mikoroshini haya ni maeneo korofi kwa tabia hizo za wizi vijana wadogo kabisa,,, na ndio maana raia wamechoka na kujichukulia maamuzi kwa kuwa hata wakipelekwa vituoni wazazi wao wanawawatetea,, sasa tutafanya kama tulivyofanya kipindi cha komando yosso,, msako nyumba hadi nyumba.
komandoo yosso walitutesa sana, fikiria mtaani mnalinda sungusungu watu 10 hadi 12 halafu wenyewe wanakuja 40 wana visu, mapanga bisibisi n.k...
 
Arovera nitajie kifungu Cha sheria kinachosema kibaka ambaye hana silaha anatembea barabarani auawe?
Wewe ulitaka akutwe na Silaha ndio auawe ilihali anajulikana ni kibaka? Vibaka wanafahamika sana mitaani mida yao ya kutembea na silaha ni usiku, siku mtaa ukimchoka unammaliza muda wowote katika mazingira yoyote. Vibaka wanalindwa sana na wanufaika wa matunda ya wizi wao haswa Wazazi na ndugu/jamaa wa karibu. Wewe mama unaamka asubuhi mtoto anakupa elfu 50 na unajua kabisa hajishughulishi na kazi yoyote unapokea tu unapeleka kwenye VICOBA ukiletewa taarifa mwanao ni mwizi mkanye wewe unaanza kumtetea unategemea wananchi wenye kutafuta riziki zao ki halali watamshughulikia vipi kijana wako kama sio kumuua?
 
Aisee hao vibaka wamburahati nihatari sana waogope, kwanza wao wenyew wanamazuna wakikutait ukileta mgomo hata kdg unaweza shangaa washapita na vidole na utaibiwa na hamna msaada wwte utakaopata
Hao mama zao wanajua tabia zao ila ndo hivo wanawatetea kwa sana wacha iwe fundisho kdg sababu walishajiona miungu watu yani watu wanakaba mchana kweupe as if ni jambo lakawaida.
Mama anatetea kwa sababu anajua Rejesho la Kikoba analipata akiwa amekaa tu
 
Mastakiraka una hoja dhaifu sana.Sheria za nchi zinasemaje?

Hivi kila mtu aamue kujichukulia sheria mkononi itakuwaje?

Muhimili wa mahakama una kazi gani?
 
Von wewe ni hakimu? Haya ndio kibaka... nioneshe kifungu cha sheria kinachowapa sungusungu wafanye mauaji? Tena kijana huyo hajakutwa eneo la tukio,hakuwa na silaha.... polisi,mahakama wana kazi gani?
Ww ndio mfadhili wa hao vibaka au?,mbona unawatetea sana as if una maslahi nao
 
mburahati ni kwetu ila watoto wa kule najuwa vizuri .
kuna kipindi ikifika saa nne au satano usipo kuwa na boda boda wakukufikisha mtaani imekula kwako.

maeneo yote kuanzia mburahati,tandale,mabibo sehemu chache na manzese.

vijana wengi ni mtihani japo ndo vijana wetu.

niliposikia jina la huyo dogo sijashangaa maana !
 
Unaniambia nina rejesho la vikoba...kwa hiyo uuwe mtu kisa kibaka,sheria ya wapi?
 
Mastakiraka jaribu siku moja kuua mtu kisa amekupora simu yako.Ikiwa mtu huyo hana silaha.Jela inakuhusu.
Kwahiyo umeamua kuhalalisha wizi ?, ukishakuwa kuwa kibaka haijalishi umekutwa na silaha au laah utaadhibiwa tuu
 
lady mwali, me naona hauna hoja ya msingi hapa yan unatupigia kelele tu humu.

kama unataka mambo ya sheria nenda mahakani.
 
Kuna Jamaa yetu aliuawa maeneo ya Mburahati GINE..alikatwa mfupa wa nyuma wa kisigino na hao hao Sungu Sungu..Nawachukia Sn Hao Wange.S.e.
Pale guinea hajawahi kuuliwa mtu ambaye sio mwizi,wa mwisho kuchomwa pale alipora simu akiwa na denda,denda akakimbia huyo akatiwa mkononi,na toka tukio lile yapata miaka hata 8 sasa hv na hakuna matukio ya kishenzi tena,kulikua akufai kule ila baada ya kuanza ile operesheni ya choma wezi kumetulia sasa hv
 
huyu dogo jumanne taarifa zilizo nifikia kuwa.mwizi wa pikipiki na kukaba watu.

kituo cha mburahati kilitoa baraka kwa kumchoka kwa matukio yake na popote hakipatikana kifo.

kesi imeshafungwa mburahati.

maaana RB nyingi hapo mburahati zimekuwa nyingi
 
Pale guinea hajawahi kuuliwa mtu ambaye sio mwizi,wa mwisho kuchomwa pale alipora simu akiwa na denda,denda akakimbia huyo akatiwa mkononi,na toka tukio lile yapata miaka hata 8 sasa hv na hakuna matukio ya kishenzi tena,kulikua akufai kule ila baada ya kuanza ile operesheni ya choma wezi kumetulia sasa hv
denda nowdays katulia..pamoja na Roja mtambo wote wapo Calm..mkuu unaweza ukawa jirani yangu ww.
 
Back
Top Bottom