Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Poleni.

Mimi nishavamiwa na vibaka mara tatu. Huwa nikiona watu wanamshughulikia kibaka nawaongezea na mafuta taa kabsa.

Vibaka walinipiga mabapa ya mgongoni home kwangu mpaka nikasanda. Usipowawahi wao hawana huruma.

Mnalea vibaka hatuishi kwa amani.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] polee mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekaa mabibo, luhanga, mburahati, vijana wengi ni watumiaji wa madawa na pombe..vikana wengi wapo kwenye makundi ya uhalifu, wengi ni wakabaji, kuna mitaa unakabwa mchana wa saa nane kweupee na ukileta ubishi wanakutoa utumbo.

Kuna vibaka wanaotumia bisibisi


Wapo wanaotumia nondo

Wapo wanaotumia sime ( panga )

Na wapo wanaotumia ngumi, hawa ndio noma zaidi, yaani unachezea ngumi mpaka mbavu changa zinaachana hata kutoa ukelele hautoki, kitakacho toka ni ulichonacho ama wanachokihitaji. Wakabaji wengi wanacheza boxer pande zile.

Kuna mauaji ya ajabu ajabu sana kigogo njia panda, mmbuyuni, na Luhanga, kukuta mtu amekufa kwenye mitaro ni jambo la kawaida sana..

Kuna mwaka fulani hao vijana walikuwa wanaafunga mtaa, ( watoto wa mbwa) kipindi kile cha ma camp, mabibo- mburahati, wanataka watu wote muwe ndani saa 9 mchana kweupee, ukikutwa kitaa ni panga hakuna maelezo,

Hao hao Sungu Sungu baada ya kupata kibali ilifanyika operation moja matata sana, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, kile kikosi kilikuwa kikiitwa wazee wa CUF, nadhani mliowahi kukaa maeneo yao mnafahamu kazi iliyofanywa na hao watu, kigogo ikatulia.



KUFA NI HAKI...KIBAKA ( MWIZI ) KIFO NDIO SULUHISHO PEKEE.
 
naona sasa umeshaanza kuelewa ivo punguza domo.

kuna siku natoka zangu maeneo ilikuwa mida ya saa mbili usiku nikakutana na hao unao watetea wakiwa watatu wakani,tight vzr tu nami nilipo taka kujitetea nikachomwa kisu cha karibu na jicho na akawa anakikandamiza ivo nikatulia.

baada ya kumaliza kazi yao mmoja akasema mpe kubwa, daah!!!

alafu uwez amini waliofanya hivyo nawajua.

hapo kosa langu lilikuwa nin na nao walitumia sheria gan kutenda hilo tukio???

nlipoteza vitu vyangu muhimu na dira kw week kwa sababu sikuwa na pesa tena ivo nyumban wakashinda na njaa nami nkiuguza majeraha.

hivyo nami NILIHAPA KWA MUNGU WANGU endapo ikitokea siku mmoja kati yao anapewa kichapo kwa ajili ya wizi wake basi mim ndie ntakuwa mtoa roho haki ya mungu.
 
Nyinyi ropokeni tu...kaeni mkijua mnachofanya ni unyama wa Hali ya juu...unawezaje kumuua binadamu mwenzako kama unaua paka?

Kama mna hasira nendeni kuua wauza madawa ya kulevya,wala rushwa na wahujumu uchumi.
Unakataza kuua vibaka ila unaruhusu kuuawa wahujumu uchumi,wauza madawa ya kulevya...!!

Kwenye kikao cha mtaa Kibamba raia waliwataja vibaka,mama mmoja alipinga hadharani kuwa mwanawe hawezi kujiingiza kwenye ujinga huo maana kwake kuna kila kitu.
Mwanajeshi akawa na hekima,akambeba mwanae akamtupa polisi Kibamba kwa wiki mbili,kijana akaomba msamaha na kuomba arudi shule, akaachiwa.
Miezi michache mtoto wa yule mama aliye pinga hadharani kuwa mtoto wake sio kibaka akakamatwa Kibwegere kwenye nyumba ya mtu saa nne usiku anang'oa tv ukutani,alipitia dirishani,raia wakamtambua,wakamtia ubatizo wa moto,saa saba usiku taarifa ikafika kwa mama. Hakuthubutu kuiremba sura yake nje hadi tumezika mwanae...

Walimwengu ndio walezi wa watoto wetu,tusiwatetee watoto kwa mambo tusiyo na uhakika nayo
 
Mkulungwa1 hata kama alikuwa kibaka sheria ipi inaruhusu apewe adhabu kubwa kiasi hicho na wahalifu ambao si mahakama?

Usijitoe ufahamu...acha hoja dhaifu...
Heeee! Ya kujitoa ufahamu yanakujaje? Nimeuliza swali na si vinginevyo? Hiyo hoja dhaifu umeiona wapi?
 
Binagsi nawapongeza sungusungu kwa kazi na ntakuwa natoa michango huyo kijana kasumbua sana mtaani nasikia alikuwa ni mwizi sana watu wamesherekea kifo chake hakuna anaelaum ukifanya utafiti wewe utakuwa ni miongoni mwa wenye watoto au ndugu vibaka
 
Nyinyi waropokaji bado hamjanipa kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia sheria mkononi....kwa akili zenu fupi nini kazi ya Polisi ,mahakama na magereza?
Kwani vibaka wanatumia kifungu gani cha sheria kinachoruhusu kuiba? Mimi siungi mkono kuua vibaka, lakini kuna wakati mwingine jamii inachoshwa. Ukiona mtaani kila mtu anakunyooshea kidole wewe ni kibaka mara nyingi huwa ni kweli. Hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia sheria mkononi, lakini vile vile hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia mali za watu. Mara nyingine ushenzi unatakiwa kijibiwa kwa ushenzi, unyama unatakiwa ujibiwe kwa unyama. Yeye si alijuwa anajifanya mjanja kuwa hawawezi kumfanya chochote kwa sababu hawana ushahidi au hawajamkamata? Basi nao wamemuonyesha kuwa wanajua kuliko yeye.
 
Kwani vibaka wanatumia kifungu gani cha sheria kinachoruhusu kuiba? Mimi siungi mkono kuua vibaka, lakini kuna wakati mwingine jamii inachoshwa. Ukiona mtaani kila mtu anakunyooshea kidole wewe ni kibaka mara nyingi huwa ni kweli. Hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia sheria mkononi, lakini vile vile hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia mali za watu. Mara nyingine ushenzi unatakiwa kijibiwa kwa ushenzi, unyama unatakiwa ujibiwe kwa unyama. Yeye si alijuwa anajifanya mjanja kuwa hawawezi kumfanya chochote kwa sababu hawana ushahidi au hawajamkamata? Basi nao wamemuonyesha kuwa wanajua kuliko yeye.

Hii inaitwa kujichukulia sheria mikononi.

Jeshi la polisi lililopo busy na wapinzani na kuacha majukumu yake ya msingi kama haya halifai na ni bora lisiwepo.

Sirro must go!
 
Back
Top Bottom