Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Kuachana ni sawa kama kuna mmoja hafurahishwi, hafurahii na hajivunii hayo mahusiano.
Maisha ni mafupi.

Ila kumwambia sababu ndio haikuwa Sawa
 
Kla mtu anamaanuzi yake kwa mila na desturi zetu yuko sawa kwan hii tabia ya kuangalia walemavu ndan ya familia kbla ya kuoa au kuolewa ni utaratibu ulokuepo ata kwa wazazi wetu na babu zetu pia walifanya ivyo

Bila unafiki akuna anayependa kuleta mattzo ndan ya familia au ukoo na ulemavu tangu zaman ilijulikana ni ttzo na watu weng hawakk tyr kuleta au kupeleka mattzo kwao

Ukwel utabakia kua ukwel ata hao wanaosaport kuolewa au kuoa kwa walemavu wanajitoa tu akili ila ukwel wanaujua
Akuna alotayali kuleta matahira ukooni kwao akuna alotayali kuleta na albino kwa ukoo wao akuna alotayali kuleta walemavu wa viungo kwa ukoo wao labda km itatokea kwa bahati mbaya

Mapenzi ni upofu labda km unampenda sana uwezi ona ivyo vtu
 
Usahihi au kutokuwa sahihi ni yeye anaweza kulipima hilo.

Kikubwa Mwambie tu akaombe toba kwa imani yake.

Uzi mchungu huu, poleni wenye changamoto ya kuuguza.
 
Yuko sahihi, ukiweka hisia pembeni swala la kuoa lapasa kutumia chaguzi zinazoratibiwa na akili zako ingawa approach aliyotumia si nzuri sana.
 
Bado ana utoto huyo
Anajua anapoenda kuoa sasa
Au yeye anaijua kesho yake
Sasa si bora huyo, mbona nyie mnakimbia kuolewa na wanaume makapuku?😂
Kuna usaliti mmbaya zaidi ya huo???
 
Ety nimekuacha kisa kwenu walemavu sio ubinadamu huu.
Yuko sahihi ila approach ameikosea tu. He would have choosen another path ya kumaliza mahusiano ambayo iko effective sana nayo ni kumkatia mirija ya pesa tu 😂😂😂 kwa wanawake wa ki Tanzania ukiwa stingy hawawezi kuku kueep.
 
Hujafa Hujaumbika .....huku kwetu Kuna maza jirani yake kulikuwa na Albino ......so yule Kwa yule maza wale watoto albino wakija pale kwake kucheza ....

Wakila chakula ...vyombo alikuwa anavitenga + kutupa

At the end of the day....naye kapata mimba ....kuzaa mtoto ni albino

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Mungu amejibu maombi😂
 
Binafsi mimi naona kijana kakosea, huenda alikuwa sahihi kumuacha ila namna alivyomuacha alikosea, ilibidi amuache kivingine, mkasa huu hapa nawapeni.

Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Hapa sasa nitaongea zaidi kama yeye mwenyewe alivyojitetea, ndipo penye kuamua kazingua au lah, twendeni pamoja.

Kijana ni kama alipata mstuko akataka kumuacha binti kienyeji ila alishindwa, ikabidi amuweke wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, alimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata ulemavu muda wowote maana hujafa hujaumbika, pia mtu yoyote anaweza kupata mtoto mlemavu maana hakuna anaemuumba mtoto atakavyo lakini yeye anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi endapo wao wakipata mtoto kwa kuhofia kwamba ulemavu wa wanafamilia ni magonjwa ya kurithi, hivyo hata kama binti ni mzima yawezekana karithishwa genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu, sababu ya zaida ambayo hakumwambia binti ni kwamba anahofia kuna mambo ya kiafrika kwenye mila au matambiko yaliyowahi kudanyika huko zamani yanarithishwa,

Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.

Je, ni sawa?
Yupo sahihi 100%
 
Back
Top Bottom