Kijana katuambia anataka kufanya harusi (kuoa) yeye kaandaa laki moja tu, anaomba aongezewe pesa iliyobaki

Hii ni kwa msajili kama ndoa ya kiserikali
Hapo Mkuu Utakuwa Unachua Vyeti Viwili Kwenye Alter
Wewe Na Mwenzako Mbadunda Kwa Step Taratibu Mnakwenda Kuvifanyia Lamination
 
Kwetu huyu anaitwa kwenye kikao anaulizwa kiasi alichonacho, akitaja pungufu hata ya 100 tu kwenye jambo lake lote kabla hata hajachangiwa kikao kinakufa bila kuambiwa chochote , akisumbua kuuliza, jibu ni moja tu kwa kila mwanafamilia, Huyo mke unayeoa ni wa familia au wa kwako mwenyewe? Hatuchangii furaha tunachangia matatizo tu, kaoe kwanza kwa hela yako ukipata matatizo kwenye ndoa tutakuchangia.
 
msiwe na bajeti kubwa (msifanye sherehe). muongezeeni laki moja nyingine - laki mbili zinatosha. Kufunga ndoa na sherehe ya ndoa ni mambo mawili tofauti.
Mkuu naomba muongozo kidogo Kwa hiyo Laki mbili unafanyajefanyaje mpaka kufungwa ndoa 🤔
 
Kijana kaomba aongezewe pesa iliyobaki ili aweze kufanya sherehe kabambe.

Wakuu mtu kama huyu anasaidiwa vipi huko kwenu?
kWANI 100,000 haitoshi kma ni mkristo aende kanisan afunge ndoa watawanyike, joni awaite wazazi wa binti na wazazi wake wale dinner , salan 12,000 na Maji imetoka iyo
 
Tumuulize mchengerwa ana uzoefu na ukweni
 
Kijana kaomba aongezewe pesa iliyobaki ili aweze kufanya sherehe kabambe.

Wakuu mtu kama huyu anasaidiwa vipi huko kwenu?
Mbona pesa nyingi hiyo kama mtaiplan vizur
Yan hapo mchele = 40,000/=
Maharage: 10,000/=
Nyama kilo mbili (kwa ajili ya wageni muhmu)= 16000/=
Viungo na mafuta =14000/=
Hapo anabakiwa na elf 20,000/= ya honeymon

Najua bwana harusi hawezi kosa sabufa la kuchangamsha shughuli
 
....mbongo mnapotezana miaka nenda rudi yaani hamuwasiliani, baadae unashangaa amepata contact zako. mnawasiliana muda mchache tu ikiwemo kukumbuka ukaribu wenu wa enzi hizo, haujakaa sawa anakuambia anajambo lake la harusi tena haraka ndani ya ule mwaka.

anakuomba vilevile uwe mwanakamati wake..hapo tambua ulitafutwa ili umchangie. anakutafuta ukamilishe mipango yake na sio kudumisha urafiki wenu.

binafsi nachingia, lakini ukinitafuta na nikajua unataka nikufurahishe hunipati. wa kuchangiana wale tuko sambamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…