Kijana mwenye wazo la Biashara la mtaji wa Mil 5-10

Safi
 
Tupe sababu.

Na je ukweli ni upi?

Wana JF wanahitaji kujifunza toka kwako, Ukipewa mtaji wa 2.5M utaanzisha biashara gani itakayokupatia angalau TZS 100,000 kama faida.

Karibu, Nami pia Niko tayari kujifunza toka kwako.

Hakuna biashara ya mtaji 2.5M itaingiza faida ya laki moja kila siku. Kwa hapa TZ huo ni uongo.
 
Asiye na wazo achukue hapa. Tampa muongozo na mchanganuo. Yaani business plan yake.
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kuwatengeneza kucha wadada
 
Hakuna biashara ya mtaji 2.5M itaingiza faida ya laki moja kila siku. Huo ni uongo.
Sasa jifunze hili.
- 2.5M itakuwa converted na kuwa US $5,000 , Hii Dola $5,000 ambayo ni 5% Daily Drawdown ya $100,000 account utakayopewa ku_trade na prop firm utakayochagua.

Ukibadili $5,000 kuwa TZS utapata TZS 11,500,000, Yes 11.5M hiki ndicho kiasi unachopewa ku_trade kwa siku, maana hiyo ndio DD ya 5% ya $100,000 kwa account utakayopewa.

Angalia hapa baadhi ya Prop firm.
Code:
https://docs.google.com/spreadsheets/d/1U0M8mZBnGMa9NQoC6o6qaYphTbM58T28_2LgDbBVfrw/edit#gid=0

Ndugu Fernando Wolle , Kwa upande wako, jirekebishe na utumie busara, Ukiona kitu ambacho hakina maana kwako, badala ya kutumia neno "UONGO", omba ufafanuzi au maelekezo zaidi ili uweze kujifunza.

Trading ndio biashara pekee ambayo utatumia mtaji mdogo kuweza kupata faida kubwa, iwapo tu unafahamu nini unachotakiwa kufanya.
==
 
Kampuni ya Engineering (ipo active), ina-deals na engineering works. Kwa sasa inafanya kazi na baadhi ya mashirika, ila changamoto ipo kwenye running Capital. Once kazi 2 zikifanyika, Cap inakata hivyo hatuna budi kusubiri mpaka hela itakapolipwa ndio tuweze kufanikisha (kuomba kazi nyingine).

Hivyo nafasi ya Investors ipo wazi.

MY CV's
Proffesion: Mechanical Engineer
Works experience: 6+ yrs
 

Personal care gani mnaleta?
 
Tembea uone

Nanunua carton 450,000 within a few hours nimemaliza mzigo kwa 700,000 na hapo nauza Bei ya chini Ili mzigo utoke chapchap

Ni mwendo wa kucheza na fast moving products na wholesalers only
Hello Hornet, sijakuona siku nyingi kwenye jukwaa la biashara I hope you are doing fine. Happy women's day
 
Nipe notes mkuu kama itakupendeza, hiyo kampuni inafanya kazi za aina gani hasa na inajiendeshaje? Sina pesa ya kuweka ila naomba notes coz mi mecha kama wewe ila ni fresh from school.
 

Mwl.RCT achana nae hana hoja yyte.
 
Nipe notes mkuu kama itakupendeza , hizo kampuni inafanya kazi za aina gani hasa na inajiendeshaje? , sina pesa ya kuweka ila naomba notes coz mi mecha kama wewe ila ni fresh from school.
Kama ni fresh from school ushauri ninaoweza kukupa ni tafuta kwanza experience (Experience ndio gold huku nje) kwa kujitolea au kufanya kazi kwenye engineering company (kuna gap kubwa sana kati ya theory za darasani na mambo yalivyo huku nje). Kama unataka kujitolea nichek PM , sina uwezo wa kukuajiri kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…